Sababu ya nyani jike kupenda nyani dume wenye pua kubwa

Nyani wenye pua kubwa ni mojawapo ya nyani wanaotambulika zaidi duniani.
Katika siku za nyuma, ilisemekana kwamba pua zao zilikuwa kubwa sana, walipaswa kuzishikilia kwa upande mmoja ili waweze kula, lakini hii si kweli. Wanakula vizuri tu.
Wanapatikana katika kisiwa cha Borneo Kusini-mashariki mwa Asia, nyani hawa wa Ulimwengu wa Kale ni wa kijamii na wanyenyekevu. Wanaishi katika makundi; Kundi la majike huwa na dume mkubwa, anayetawala na majike na watoto wao.
Huishi msituni kando ya vijito na mito, ambapo hutafuta matunda, mbegu na majani. Matunda ambayo hayajaiva hupendelewa kwani kiwango cha juu cha sukari katika matunda yaliyoiva kinaweza kusababisha matumbo yao ambayo tayari ni mazito kutanuka zaidi.

Watoto wa tumbili aina ya proboscis huzaliwa wakiwa na nyuso za samawati angavu na manyoya meusi, ambayo hubadilika polepole na kuwa rangi ya watu wazima wanapokua
Ndio nyani pekee wanaojulikana kurejesha chakula chao na kukitafuna mara mbili na kuwa na tumbo mithili ya ng'ombe lenye vizimba vingi. Bakteria wa Symbiotic wanaoishi kwenye chemba husaidia kuvunja na kuondoa sumu ya chakula chao ambacho ni kigumu kusagwa.
Kila kitu kuhusu nyani hawa ni kikubwa. Tumbo lao ni kubwa, linajumuisha hadi robo ya uzito wa mwili wao.
Wana miguu na mikia mirefu. Wao ni wakubwa kimwili, madume wanaweza kuwa na uzito wa hadi 24kg (karibu 52lbs).
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Na bila shaka, pua zao ni kubwa na maumbo makubwa, wanavyoonekana, kama wale wa wakoloni wa Uholanzi waliokwenda Borneo katika karne ya 19, na kuwafanya watu wa eneo la Malai kumpa jina la utani tumbili huyo 'Orang Belanda'.
Nyani jike aina ya proboscis hupenda nyani wenye pua kubwa, ambayo ni maalum madume na inakua na hadi urefu wa 17cm (6.5in), ni sifa iliyochaguliwa yenye kuvutia kingono. Majike wanapendelea madume wenye pua kubwa na sayansi husaidia kueleza kwa nini.
Uchunguzi unaonesha kwamba madume wenye pua kubwa wana miili na korodani kubwa, na kwamba ukubwa wa pua huathiri ubora wa sauti za madume. Pua zao zina ashiria ufanisi katika masuala ya uzazi na, kwa kuzingatia hii, madume wenye pua kubwa huwa na majike wengi zaidi katika himaya zao.
Tumbili dume hutumia pua zao kubwa kuinua sauti na kuvutia wenzi.
Cha ajabu, madume wenye pua kubwa pia huwa na meno madogo mithili ya mbwa. Hili ni jambo lisilotarajiwa kwa sababu madume wa aina nyingine za nyani mara nyingi hutumia meno kwa ajili ya kupigana na kujilinda.















