Kwanini wanyama wa jamii ya mbwa hugagaa kwenye kinyesi?

fv

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mbwa anaweza kugagaa kwenye kinyesi, kwa furaha au ulinzi.
    • Author, Richard Gray
    • Nafasi, BBC
  • Muda wa kusoma: Dakika 5

Mbwa wana mvuto wa ajabu wa kupenda kuzunguka katika vitu vyenye harufu mbaya. Na ndicho alichokishuhudia mtafiti Simon Gadbois kila alipomchukua mbwa wake, Collie Zyla katika safari zake za utafiti.

Wakati akiwafuatilia wanyama wa porini huko Nova Scotia, Canada, mbwa wake Zyla alisimama ghafla, akanusa pua yake chini, na kabla Gadbois hajafanya chochote, alibingiria kwenye uchafu hadi harufu ikamuingia.

Hali hii inaweza kuonekana kuwa ya kawaida kwa wamiliki wengi wa mbwa; mnyama wako pendwa anarudi nyumbani akiwa na harufu mbaya baada ya kuviringika kwenye kinyesi.

Pia unaweza kusoma

Tafiti za Wataalamu

Binadamu walianza kufuga mbwa mwitu miaka 23,000 iliyopita, na tangu wakati huo tulianza kuishi nao.

Mbwa mwitu huzunguka kwenye kinyesi cha wanyama wengine, na hata kwenye mizoga ya wanyama.

Uchunguzi wa 1986 kutoka nchini Canada, waliwaweka mbwa mwitu kwenye harufu tofauti tofauti. Kwa mshangao, watafiti waligundua mbwa-mwitu hawakupenda kujiviringisha kwenye kinyesi cha wanyama walao majani kama vile kondoo au farasi. Pia hawaku jiviringisha kwenye chakula.

Badala yake, harufu waliyopenda zaidi ni manukato na harufu ya mafuta ya gari. Kwa mnyama ambaye anataka kuficha harufu yake, kuchagua kunusa kitu kigeni mbali na mazingira yake ya asili ni jambo lisilo shangaza.

Lakini watafiti pia waligundua, harufu ya pili iliyopendwa na mbwa mwitu ni kinyesi cha wanyama wengine wanaokula nyama kama vile simba na dubu.

Pat Goodmann, mfugaji mwenye uzoefu wa wanyama katika hifadhi ya Wolf Park huko Indiana, Marekani, ametumia miaka mingi kujifunza harufu ya mbwa mwitu, ameona tabia kama hiyo kati ya mbwa mwitu aliowasoma.

"Hapa Wolf Park, mbwa mwitu wako tayari kujipaka harufu wasioijua. Hili linaleta uwezekano kwamba wanaweza pia kujipaka kinyesi cha wanyama wanaowinda," anasema.

Ni aina ya ulinzi

f

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mbwa mwitu mara nyingi huzunguka kwenye harufu ya wanyama wengine wanaokula nyama.
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Tabia hii inaweza kuwafichua kutoka kwa mawindo yao, lakini inaweza kuwasaidia kuepuka wanyama wanaokula wenzao.

Wazo hilo linaungwa mkono na utafiti uliochapishwa mwaka 2016 na Max Allen, mwana-ikolojia na mhadhiri wa zamani wa Chuo Kikuu cha Wisconsin huko Madison na sasa anafanya kazi katika Chuo Kikuu cha Illinois Urbana-Champaign.

Allen, kwa usaidizi wa kamera, alinasa mfululizo wa tabia zisizo za kawaida za mbweha wanaoishi katika eneo la Santa Cruz huko California.

Mbweha walitembelea mara kwa mara eneo la puma wa kiume, ili kupata harufu yao. Picha hizo zilionyesha mbweha hao wakisugua pua zao chini kwenye alama ya mkojo wa puma.

Allen anaamini mbweha walitumia harufu iliyoachwa na wanyama hawa wakubwa kama njia ya kujificha kutoka kwa wanyama wengine wakubwa kama vile mbwa mwitu.

"Mbwa mwitu ni wakubwa zaidi kuliko mbweha wa kijivu, na wanaonekana kutaka kuwaondoa mbweha kwani wanashindania rasilimali," anasema Allen.

"Mbweha hawawezi kupambana nao, kwa hivyo hutumia harufu ya puma kupata ulinzi wa aina fulani. Kwa kunusa harufu ya puma hupata wakati wa kutoroka."

Lakini hilo halielezi kwa nini wanyama wengine wa jamii ya mbwa, kama vile mbwa mwitu, pia hujipaka harufu iliyoachwa na wanyama wengine wanaowinda.

Mwingiliano wa kijamii

df

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ulinzi na mbinu za uwindaji ni baadhi ya sababu.

Linapokuja suala la mbwa wako, inawezekana kuna sababu ya kijamii kwa tabia hii.

Uchunguzi wa fisi waliofungwa uligundua kwamba wanyama hao walipobeba harufu ya mzoga kwenye ngozi zao, walinuswa na kusogelewa zaidi na wanyama wengine wa kikundi chao. Lakini walipopakwa harufu ya kafuri, mwingiliano wa kijamii ulipungua

Uhusiano na chakula

Goodmann anasema kugaagaa katika harufu kunahusiana na chakula, harufu kubaki mwilini inaashiria mbwa anataka kurudi kwenye chanzo cha harufu.

Goodman aliona mbwa mwitu wakila vipande vya nyama ya kulungu mdogo na kisha kugaagaa juu ya nyama ya kulungu mwingine.

Utambulisho wa kikundi

df

Chanzo cha picha, Getty Images

Gadbois anasema katika makundi ya mbwa mwitu aliowatafiti huko Canada, mnyama anayeongoza kundi huwa wa kwanza kuzunguka kwenye harufu kali, akifuatiwa na wengine.

"Inaweza kuwa hii ni kuanzisha harufu ya kundi. Katika mbwa mwitu nilio wasoma, kiongozi wao akianza kusugua kitu kama mzoga wa kulungu, kundi nzima litafuata na kuisugua. Hii pia nimeiona kwa mbwa mwitu na mbweha wa porini. Ndio huwa ni harufu ya kila mnyama kwenye kikundi," anasema.

Wazo hili la kugawana harufu ili kuongeza hisia za "pamoja" pia limeonekana katika mbwa mwitu wa Kiafrika, ambapo wa kike hujigaragaza kwenye mkojo wa mbwa dume wa kikundi wanachotaka kujiunga.

Vile vile, mbwa mwitu wa Kiafrika mara kwa mara husugua tezi za wengine kwenye kundi ili kuchukua harufu yao.

Hii inaunga mkono wazo kwamba wanyama wanaoishi katika makundi, kama vile mbwa mwitu na mbweha, wanaweza kuitumia kama njia ya kutambuana wenyewe katika kikundi.

Inaweza pia kuwa ni njia ya wanyama kuboresha hali zao za kijamii. Kwa kujijaza harufu ya mnyama mzee, wanaweza kuongeza hadhi yao.

Uchunguzi wa hivi karibuni ulioongozwa na Roberto Cazzolla Gatti, mwanabiolojia katika Chuo Kikuu cha Bologna, Italia, unasema "Tabia ya kunusa inaweza kuwa na kazi nyingi; kuiga, urafiki na utambulisho.”

Dalili ya Furaha

c

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mbweha wa kijivu wanaweza kugaagaa katika harufu ya wanyama wanaowinda wakubwa kuliko wao wenyewe.

Inaweza pia kuwa wanyama wanafurahia tu kugaagaa katika harufu kali. Kitabu cha mtaalamu wa tabia za wanyama Michael Fox, cha 2007: Dog Body, Dog Mind, anasema, mbwa wanaweza kuwa wanajipaka harufu kwa ajili ya kujifurahisha, kwa njia ile ile ambayo wanadamu hujipulizia manukato.

Wanyama wa jamii ya mbwa sio pekee wanaojipaka harufu, paka pia wanajulikana kwa tabia hii.

Pia unaweza kusoma

Imetafsiriwa na Rashid Abdallah na kuhaririwa na Seif Abdalla