Tetesi za soka Ulaya Jumatatu: Real Madrid na Barcelona wamtaka Rodri wa ManCity

Muda wa kusoma: Dakika 1

Manchester City itakabiliana na pambano la kutaka kumbakisha kiungo wa kati wa Uhispania Rodri msimu huu, huku Real Madrid na Barcelona wakimtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29. (Bild - In Germany)

Matumaini ya Liverpool kumsajili beki wa Roma Zeki Celik yameongezeka baada ya wakala wake kukataa uwezekano wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uturuki mwenye umri wa miaka 29 kujiunga na Juventus. (Mirror)

Arsenal na Chelsea wanaisukuma Barcelona katika kumsaka mshambuliaji wa Atletico Madrid na Argentina Julian Alvarez, 26. (TeamTalks)

Juventus wamemtambua mlinda lango wa Tottenham mwenye umri wa miaka 29 Guglielmo Vicario kama shabaha kuu msimu huu, lakini watakabiliwa na ushindani kutoka kwa Inter Milan. (Gazzetta dello Sport - In Italy)

Newcastle itamuuza mshambuliaji wa Ujerumani Nick Woltemade msimu huu wa joto ikiwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 atataka kuondoka katika klabu hiyo. (Football Insider)

Arsenal wako mbele ya Manchester City na Newcastle katika kinyang'anyiro cha kumsajili beki wa Sporting raia wa Uhispania Ivan Fresneda, 21. (Fichajes - In Spanish)

Kuwasili kwa Fresneda kunaweza kumfanya beki wa Uingereza mwenye umri wa miaka 28 Ben White kuondoka Arsenal. (TeamTalks)

Manchester United na Arsenal wanapewa nafasi kubwa ya kumsajili beki wa Eintracht Frankfurt, 22, Nathaniel Brown msimu huu wa joto. (Caughtoffside)

Chelsea inaweza kumruhusu mlinzi wa Uingereza Trevoh Chalobah, 26, kujiunga na Aston Villa msimu huu wa joto ikiwa The Blues wanaweza kusajili mbadala wake. (Football Insider)