Je, Karafuu ina faida gani katika miili yetu

Muda wa kusoma: Dakika 5

Karafuu hutumika sana katika mapishi kama kiungo cha la kuongeza ladha ya chakula na vinywaji kama vile chai na vinginevyo, lakini kiungo hiki kinaweza kuwa ni zaidi ya ladha yake ya kuvutia.

Karafuu, inayojulikana kisayansi kama Syzygium aromaticum na ambayo mmea wake unaitwa mti wa karafuu, ina faida nyingi za kiafya na thamani kubwa ya lishe.

Ni viungo vyenye madin kama vile chuma, kalsiamu, magnesiamu na antioxidants (kulinda kuvamiwa kwa seli za mwili) .

Pia Karafuu kwa muda mrefu imekuwa ikitumika katika dawa za jadi kutibu magonjwa ya kupumua, ikiwa ni pamoja na koo na kikohozi.

Alipoulizwa kuhusu umuhimu wa karafuu, mtaalamu wa lishe katika Kliniki ya Tiba ya Lishe ya NFS-Togo Dkt Mathieu Tobossi, aliiambia BBC Afrique kwamba mara nyingi anapendekeza kwa wale ambao wanaoathiriwa na shughuli za kutengeneza bidhaa za vyuma, kutokana na kuvuta hewa yenye chuma.

"Tunapendekeza matumizi ya kila siku ya karafuu kwa watu hawa."

Sifa na thamani ya lishe ya Karafuu

Karafuu ni kiungo chenye Ladha na harufu nzuri ya kuvutia ambayo ina virutubisho.

Madini ya chuma ni moja ya virutubisho vinavyopatikana katika Karafuu .

Kwa mfano, gramu 100 ya karafuu ina gramu miligramu 11 ya chuma. Pia ina kalsiamu na potasiamu, virutubisho muhimu katika kuimarisha mishipa na mfumo wa misuli.

Pia, vitamini E iliyopo kwenye karafuu husaidia kulinda mfumo wa kinga.

Viungo pia vina antioxidant au kiungo cha kupambana na kuzeeka. Katika kiwango hiki, hasa . "Wale ambao huonekana kuwa wadogo kuliko umri wao."

Madhara ya kiafya

Karafuu ina faida nyingi za afya:

Dhidi ya saratani: athari ya antioxidant ya karafuu hupunguza mwanzo na maendeleo ya aina fulani za saratani, kulingana na Dk Tobossi. Kwahiyo kiungo hiki hufanya kazi katika kupunguza seli za saratani.

Kwa wazi zaidi, kulingana na mtaalamu, kuna watu fulani ambao hufanya shughuli ambazo zinaweza kusababisha marekebisho ya vinasaba (DNA).

"Kwasababu wanavuta hewa yenye chuma maumbile yao ya vinasaba hubadilika, na watoto wanakuja kuwapata baadaye na matatizo au magonjwa ya ajabu."

Anawazungumzia wachuuzi wa mitaani katika taa za barabarani au kando ya barabara katika miji ya Afrika ambako magari yanatoa moshi.

Daktari anaendelea kwa kusisitiza kwamba anawashauri watu hawa kutumia karafuu kila siku, ambayo inakabiliana na shughuli zinazohusiana na vyuma.

Athari kwenye otolaryngology : viungo hivi pia vina faida kwenye sikio, pua, koo kwa kupambana na mafua na homa .

Karafuu ina mafuta yanayoitwa eugenol ambayo hufanya kama ya kupambana na mafua na antiseptic katika eneo la ENT ( mfumo wa koo).

Kwa kifupi, inaweza kutumika katika matibabu ya kikohozi, bronchitis na mafua, kusaidia kupunguza kuvimba kutokana na kuwa na kiungo cha kupambana na maambukizi ya bakteria. Ni nyongeza ya kutibu maambukizi ya kupumua yanayosababishwa na bakteria.

Shughuli za Odontostomatology : karafuu ni kipengele katika kupambana na hali ya gingivitis ambayo ni kuvimba kwa ufizi kunakotokana na usafi duni wa kinywa.

Inaweza kutumika kwa njia ya chai kwa ajili ya kuosha kinywa.

"Ikijumuishwa na turmeric (manjano) na tangawizi . Mchanganyiko huu pia ni mzuri dhidi ya maumivu, "anasema daktari.

Digestion (usagaji wa chakula) : Ni kiungo cha viungo, lakini wataalamu wa lishe wanapendekeza kuchukua karafuu mbili kwa siku ili kuwa na ufanisi katika usagaji wa chakula-digestion "katika kiwango cha tumbo hadi kiwango cha matumbo."

Inaboresha usagaji wa chakula wa tumbo na udhibiti wa usafirishaji wa utumbo, kuchochea kazi ya enzymes( au vimeng'enyo) vya utumbo.

Aphrodisiac: ni dawa nzuri ya kupambana na upungufu wa nguvu za kijinsia. dondoo yake huongeza hamu ya tendo la ndoa

Maandalizi

Kuna njia tofauti za kuandaa karafuu naili kupata faida zake kulingana na mtaalamu wa lishe. Inaweza kupondwa, kuongezwa kwenye maji yaliyochemshwa na kuachwa itulie kwa angalau dakika 5 kabla ya kunywa.

Unaweza pia kuchemsha gramu 10 za karafuu kwa dakika 15, acha iwe baridi na uinywe. Poda ya kiungo hiki inaweza kuwekwa katika maji na kuchukuliwa mara mbili hadi tatu kwa siku.

Inaweza pia kutengenezwa kuwa mafuta muhimu ambayo yanapaswa kutumika kwa maeneo yaliyoathiriwa ya ngozi.

Imependekezwa kwa uhifadhi wa chakula

Mbali na faida hizi, karafuu zilitumiwa katika uhifadhi wa asili wa vyakula na mimea.

"Kilo 1 ya karafuu kwa kilo 100 ya kile unachotaka kuhifadhi inaruhusu bidhaa kubaki katika asili yake kwa muda mrefu. Ni hifadhi nzuri sana kwa wale walio katika mfumo wa chakula cha kilimo," anashauri Dk. Mathieu Tobossi.

Kumbuka kuwa karafuu, ni kiungo kinachopambana na maambukizi, huzuia saratani, hupunguza maumivu, huchochea hamu ya ngono, huondoa harufu mbaya, huwezesha usagaji mzuri wa chakula mwilini, hutuliza misuli na kupambana na uchovu, hupunguza shinikizo la damu na kufukuza mbu na wadudu.

Lakini kuwa mwangalifu...

Ni bora kushauriana na daktari wako kabla ya kutumia karafuu katika matibabu ya magonjwa yaliyoorodheshwa hapo juu. Inaweza kuingiliana na dawa fulani kama vile za matibabu ya kisukari (antidiabetics).

Viungo vyake vinawezakuifanya kuwa na sumu kwa afya ikiwa itatumiwa kwa kiasi kikubwa. Inaweza pia kusababisha kuwasha kwa ngozi na utando kwenye mfumo wa vimeng'enyo wa chakula kwa watu fulani.

Usiitumie ukiwa na vidonda vya tumbo. Inashauriwa karafuu isitumiwe kwa wanawake wajawazito, wanawake wanaonyonyesha na watoto wenye chini ya umri wa miaka 6.

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi