Ndani ya meli ya kifahari ya Urusi anayoshikiliwa na Uingereza

Chanzo cha picha, BBC/David Wilkins
- Author, Alexey Kalmykov
- Nafasi, BBC News Russian
- Author, Peter Ball
- Nafasi, WS News
- Muda wa kusoma: Dakika 5
Phi, meli ya kifahari ya Urusi ambayo thamani yake ni pauni milioni 38, iliundwa kutalii katika bahari ya Mediterrania na Caribbean.
Lakini badala ya kuendelea na shughuli zake chombo hicho kilicho na urefu wa mita 59 kimezuiliwa jijini London kwa zaidi ya miaka mitatu tangu kilipofanya safari yake ya kwanza.
Ni mojawapo kati ya makumi ya meli za kifahari za urusi zilizoshikiliwa tangu nchi hiyo ilipoivamia Ukraine, lakini baadhi ya meli hizo zimeziacha serikali zinazohusika nazo na shida kubwa za kisheria na kifedha.
"Kuzuiliwa kwa meli hizo, kuliangaziwa sana kwneye vyombo vya habari," anasema Tom Keatinge, mkurugenzi wa Kituo cha Uhalifu wa Kifedha na Mafunzo ya Usalama katika Taasisi ya Huduma za Umoja wa Kifalme.
"Lakini hatua hiyo ambayo ililenga kuishinikiza Urusi kusitisha operesheni yake ya kijeshi nchini Ukraine haikufikia malengo yake kwani zimeziacha serikali na matatizo ambayo hayakutarajia."
Jumanne wiki hii Mahakama ya Juu zaidi nchini Uingereza itatoa uamuzi ikiwa meli ya Phi itaachiwa huru ama itaendelea kushikiliwa katika katika bandari ya South Dock huko Canary Wharf.

Chanzo cha picha, BBC/David Wilkins
"Karibu katika meli ya Phi," anaseama kapteni Guy Booth, "hapa London na sio mahali ambapo ningelipenda kuwa."
Meli hiyo ya kifahari ina vitu vya kuvutia, ikiwa ni pamoja na kidimbwi cha kuogelea. "Tunaweza kuiweka katika umbali wowote unaotaka, kina chake kinaweza kufikia urefu wa mita 1.7," anasema.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Karibu na hapo kuna gesi ya kupikia, sehemu ya mapumziko ambayopia inaweza kugeuzwa ukumbi wa sinema, huku nyumba ya mmiliki wa meli hiyo ikijivunia kuwa na ngazi ya ya kipekee ya kuifikia.
Tangu mwezi Machi mwaka 2022, meli ya kifahari imezuiliwa chini ya sheria ambayo inai inaiwezesha serikali ya Uingereza kuzuilia meli zilizo na uhusiano na Urusi kwa lengo la kumshinikiza Rais Vladmir Putin kukomesha vitendo vyake vya kichokozi dhidi ya Ukraine.
Lakini mmiliki wa wa meli meli hiyo ya Phil, kapteni Booth na mfanya kazi wake, Sergei Naumenko, hawako tayari kuruhusu hili kwenda bila kupingwa.
Tajiri huyo wa Urusi amewasilisha msururu wa kesi dhdi ya idara ya uchukuzi ya Uingereza katika juhudi za kushinikiza meli yake kuachiwa huru, na makabiliano ya kisheria yameendelea kutoka mahakama ya juu, mahakama ya rufaa hadi mahakama ya juu zaidi.
Mawakili wake wanahoji, kwa kuwa Bw Naumenko hajawahi kuwekea vikwazo vya kiuchumi na Uingerez ana hana uhusiano wowote na Rais wa Urusi Vladimir Putin, kuzuiliwa kwa meli yake ya kifahari ni ukiukaji wa haki yake ya kisheria ya kufurahia mali yake kwa amani.
Lakini serikali imefaulu kuishawishi mahakama kwamba ina haki ya kuzuilia mali ya matajiri wa Urusi ili kuishinikiza serikali ya Urusi kokomesha harakati zake nchini Ukraine.
Sio meli ya Phi pekee iliyojipata katika hali kama hiyo.
Kote duniani meli za kifahari za Urusi zinazozuiliwa zimezitumbukiza baadhi ya serikali katika mzozo wa kisheria na kugharamia bili za makumi ya mamilioni ya dola kudumisha utendakazi wa meli hizo.

Chanzo cha picha, Sabri Kesen/Anadolu Agency via Getty Images
"Masuala ya kisheria yanayohusiana na utunzaji wa meli hizo, ni mambo ambayo serikali zote zilizochukua hatua ya kuzizuilia hazikutarajia," anasema Alex Finley, afisa wa zamani wa CIA, ambaye alihudumu Ulaya na ambaye amekuwa akiangazia meli kubwa za Urusi na vikwazo.
Gharama ya utunzaji wa meli hizo za kifahari, kwa kawaida 10% ya thamani yake kwa mwaka. Hii inaweza kumaanisha ada ya kila mwaka ya mamilioni au hata zaidi ikiwa chombo husika ni kubwa zaidi.
"Inagharimu pesa nyingi baadhi ya serikali," anasema Bi Finley.
Kwa kuwa mmiliki wa Phi hajawekewa vikwazo vya kiuchumi, analipia utunzaji wake.
Lakini kimataifa baadhi ya meli kubwa zilizozuiliwa ni za watu waliowekewa vikwazo vya kifedha kumaanisha kwa mujibu wa sheria za ndani hawawezi kutoa pesa kulipia gharama ya matunzo ya meli zao.
Nchini Italia mamlaka inaripotiwa kulipa zaidi ya £23m tangu Machi 2022 kudumisha meli ya Sailing Yacht A ya thamani ya $600m, ambayo mmiliki wake anakabiliwa na vikwazo vya kifedha.
Nchi zinashikilia meli ndogo ndogo pia.
Nchini Marekani, kushikiliwa kwa meli ya Amadea yenye urefu wa 106m kumegharimu serikali zaidi ya $30m.

Chanzo cha picha, EUGENE TANNER/AFP via Getty Images)
Mamlaka katika eneo la San Deigo huko Marekani ilikuwa imepanga kuuza meli ya kifahari ya Urusi inayozuiliwa ili kurejesha gharama yake na kupata fedha za kusaidia juhudi za vita za Ukraine.
Lakini hatua hiyo imekumbwa na mvutano wa kisheria baada ya mzozo kuibuka juu ya ni nani hasa mmiliki halisi wa chombo hicho.
Ukraine pia imejipata katika hali hiyo kwa muda sasa. Tangu 2022, nchi hiyo imeshindwa kuuza meli ya kifahari ya Urusi kwa jina Royal Romance ambayo imkuwa ikizuiliwa nchini Croatia.
Ni meli moja tu ndio imeuzwa kwa ombi la serikali inayoishikilia.
Alfa Nero iliripotiwa kuzigharimu mamlaka za Antigua na Barbuda takribani dola 28,000 kwa wiki kulipia ada ya matunzo wakati mataifa hayo ya visiwani yalipoamua zilipoamua kuiuza.
Ilinunuliwa na bilionea wa Uturuki kwa kima cha dola milioni 40 za Kimarekani.
Lakini mmiliki wake mpya na serikali ya Antigua zimeshtakiwa na binti wa mfanyabiasha wa Urusi aliye wekewa vikwazo kwa kifedha ambaye anasema meli hiyo ilikuwa yake.
Tom Keatinge anahisi hatua ya kushikilia meli hizo huenda ilizifanya mataifa ya magharibi kutochukua hatua madhubuti ambazo zingelemaza uwezo wa jeshi la Urusi.
"Je ilikuwa sawa kuwaandama matajiri wa Urusi? Naam huenda ilikuwa sawa. Lakini je, kulikuwa na haja ya kugeuza mzozo wa Ukraine kuwa suala la watu hao wenye ushawishi? Bila shaka hapana. Tulihitaji kuangazia mambo ambayo yalikuwa ya muhimu kuanzia mwanzo."
Utata wa kisheria unaozunguka meli za kifahari za Urusi huenda zikwafanya watu ambao walikuwa na nia ya kununu meli hizo zilizozuiliwa kuwa na wasiwasi, has ikizingatiwa umili wake ambao sio rahisi kutambuliwa na mataifa yasiyo rafiki.
"Inawezekana," anasema Benjamin Maltby, wakili mkuu wa meli za kifahari Keystone Law, "kwamba meli ambayo imeuzwa inaweza kufikishwa katika eneo la mamlaka nyingine na mamlaka ya bandari kumgeuka mmiliki na kusema: 'Wewe si mmiliki'."
"Kutekeleza sheria," anaongeza, "kunahitaji utashi wa kisiasa na matakwa ya wanasiasa wenyewe."

Huko Uingereza Kapteni Booth anasema ana wasiwasi kwamba kuzuiliwa kwa Phi katika Doksi ya Kusini, ambayo haina bandari sahihi au vifaa vya baharini, kumeiacha meli ya juu katika hali mbaya.
"Hali mbaya zaidi itakuwa moto wa umeme kwenye bodi," anasema, akiongeza kuwa bado ana matatizo ya meno baada ya safari yake ya kwanza.
"Moto unaweza kuzuka wenyewe na kusambaa haraka sana," anaongeza. "Alumini huwaka kwa 3,500C."
"Au hata meli inaweza kuzama, hapa Canary Wharf."
Ilipoulizwa juu ya hatari ya kushikilia Phi huko Canary Wharf, Idara ya Usafiri ilitoa taarifa ikisema "haiwezi kutoa maoni juu ya madai yaliyotolewa na Kapteni Booth kwa sababu ya kesi zinazoendelea mahakamani".
Mamalaka inayosimamia Mfereji na Mt, inasema: "Mkuu wa Bandari anaendelea kutafuta ufafanuzi kutoka kwa Wizara ya Uchukuzi (DfT) kuhusiana na hadhi ya chombo hiki. Kipaumbele chetu kinasalia kuwa operesheni salama na usalama wa mabandari."
Mustakabali wa Phi unaweza kuamuliwa na Mahakama ya Juu Jumanne.
Lakini hatima ya meli za zingine za kifahari za Urusi, huenda isijulikane hivi karibuni.












