Droni hatari ya "Lancet": Je silaha hii ya ajabu ilitoka sehemu gani ya Urusi?

.

Chanzo cha picha, OLEKSANDR SLADKOV

Maelezo ya picha, Ndege isiyo na rubani ya Lancet iliharibu meli ya M777 ya Jeshi la Wanajeshi la Ukraine, Novemba 16, 2022. Picha iliyochukuliwa kwenye skrini ya video

Katika wiki za hivi karibuni, Urusi imeanza kutumia kikamilifu ndege zake zisizo na rubani yaani (drone) dhidi ya wanajeshi wa Ukraine.

Matumizi makubwa ya droni mpya zaidi za kamikaze za "Lancet" husababisha furaha maalum katika vyombo vya habari vya Kirusi.

Tayari wanasema ni sababu ambayo "itabadilisha sana hali ya siku za usoni".

"Lancet" (katika tiba, hili ni jina la mfano wa kisu kidogo cha upasuaji - zana kali ya kupasua jipu) - ni silaha za mashambilizi, droni zinazoweza kuzunguka kwenye hewa kwa muda mrefu, kufuatilia mlengwa na kushambulia na kupiga mbizi kwa kasi chini kabisa.

Ndege isiyo na rubani ilipata jina lake kutoka kwa chombo cha matibabu kwa "usahihi wa upasuaji".

Kasi ya juu ya droni ya kamikaze ya hivi karibuni ("Lancet-3") ni 110 km/h wakati wa safari ya kasi ni 300 km/h inapoangazia mlengwa.

Idadi kubwa ya video za matumizi ya mafanikio ya droni za ‘’Lancet’’ kwenye uwanja wa vita huko Ukraine ilianza kuonekana katika mtandao wa Telegram wa wanablogu wa kijeshi wa Kirusi na waandishi wa habari mwishoni mwa Oktoba na mwanzo wa Novemba mwaka huu.

Aidha, Wizara ya Ulinzi ya Urusi katika ripoti zake pia inasisitiza "mafanikio" ya silaha hii na kuitaja kama ‘’UAV‘’ ya Kirusi yenye ufanisi zaidi.

Amri ya Jeshi la Wanahewa la Ukraine pia anakubali kwamba hivi karibuni droni kama hizo zilionekana Ukraine katika ‘’matumizi mapana’’ tu.

.

Chanzo cha picha, ZALA AERO

Maelezo ya picha, Droni ya "Lancet" iliwasilishwa tu mnamo 2019, na hakuna habari kuhusu utengenezaji wake nchini Urusi hata kidogo.

Silaha mpya ya ajabu?

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Ni wazi kwamba droni za Kirusi hupata majina mazuri zaidi kutoka kwa waangalizi wa kijeshi na wataalam wa Urusi.

Kwa hivyo, kanali wa zamani Mykhailo Khodaryonok moja kwa moja anasema kwamba droni ya ‘’Lancet’’ ni bora zaidi kuliko ya Marekani – ‘’Switchblade-600 barrage drone’’.

Hasa, kutokana na sehemu yake isiyo ya kawaida ya mbawa (kuna umbo la X katika droni ya Kirusi, sio moja kwa moja), inaonekana kuwa na faida katika uendeshaji na kupiga mbizi.

Mtaalam wa Kirusi anatoa tahadhari kwamba droni ya kamikaze mara nyingi hutumiwa kwa kushirikiana na uchunguzi wa Orlan ya Kirusi. Imaamua lengo, na droni ya ‘’Lancet’’ huipiga.

Hivi ndivyo jeshi la Urusi hujaribu kuzima mifumo ya makombora ya kupambana na ndege ya adui (SAMS).

Anaamini kuwa kwa njia hii Urusi itaweza kushinda ulinzi wa anga wa Ukraine katika siku za usoni.

"Bila shaka, idadi fulani ya mifumo ya ulinzi wa anga bado imehifadhiwa katika Jeshi, na hii inasababisha usumbufu kwa marubani.

Lakini kuongezeka kwa droni za Lancet na Cube UAV ama karibuni au baadaye kutafanya kazi yao kuwa ya kipekee.

Mrusi ana uhakika kuwa utumiaji mzuri wa ndege zisizo na rubani na Urusi ndio ‘’tatizo kubwa’’ kwa Kyiv sasa.

Anathibitisha nadharia yake na habari kuhusu Ujerumani kutoa mifumo ya kupambana na droni mnamo Novemba 16 kwa jeshi la Ukraine.

‘’Ikiwa tutaanza kukagua kwa ndani (misaada kutoka Ujerumani), tunaweza kuhakikisha kwamba ‘ving’amuzi 10 na vifaa vingine kwa ajili ya ulinzi dhidi ya mfumo wa UAV ziliombwa. Hii ina maana kwamba "Gerani" (Droni za Shahed za Iran, ambazo Urusi inaziita "Geranium" , - Ed. ) na zile za "Lancet" zinaipa Kyiv kichwa kuuma."

Karibu kila siku, video inayoonesha matumizi ya ‘’lancet’’ inafundishwa na kamanda wa kijeshi wa Kirusi wa VDTRK Oleksandr Sladkov.

Yeye ni mmoja wa waenezaji wa juu wa vita nchini Urusi na, haswa, alihusika katika kuhojiwa kwa wafungwa wa vita wa Ukraine.

Kupitia mtandao wa Telegraph, ambao una zaidi ya watumizi milioni 1, tangu mwanzoni mwa Novemba, mara kwa mara huchapisha video na droni za mashambulizi za Urusi.

Sladkov anaonyesha kuwa hivi karibuni maudhui kuhusiana na matumizi ya droni aina ya ‘’Lancet’’ yameongezeka kwa kiasi kikubwa.

Voenkor pia inasisitiza kwamba ndege hizi zisizo na rubani huharibu vifaa vya Wanajeshi.

Chaneli ya Telegramu inayoungwa mkono na serikali ya Urusi "Rybar" ilihesabu kuwa katika mwezi (kutoka Oktoba 13 hadi Novemba 12) inadaiwa kwamba droni za "Lancet" ziliharibu viboreshaji 11 vya Ukraine, mizinga 7, mitambo 7 ya kujiendesha yenyewe, magari 6 ya kivita, mifumo 4 ya ulinzi wa anga, rada 5, vizinduzi 3 vya mifumo ya S- 300 na boti moja ya kivita.

Kuhusu hatua dhidi ya droni hizi, Wizara ya Ulinzi ya Urusi inatangaza kwa kujiamini kuwa hii haiwezekani: "kutokana na ulinzi wa kukabiliana na leza, inakuwa ni kana kwamba haiwezekani kuzuia au kuharibu droni za UAV."

.

Chanzo cha picha, STRATCOM OF THE ZSU

Maelezo ya picha, Droni ya "Lancet" ilidunguliwa mnamo Julai 17 huko Zaporizhzhia

Hata hivyo, vikosi vya wanajeshi vya Ukraine vina maoni tofauti.

Vikosi vya Ukraine vilidungua mfano wa kwanza wa droni ya UAV huko Zaporozhye mnamo Julai na kuweka ushahidi wa picha mtandaoni.

Ndege nyingine isiyo na rubani ya kamikaze ya Urusi ilidunguliwa wiki moja baadaye katika Jimbo la Mykolaiv ilipokuwa ikijaribu kushambulia kituo cha rada.

Mnamo Oktoba, jeshi la anga la vikosi vya wanajeshi wa Ukraine liliripoti kwamba waliweza kudungua droni za Lancet 2 kwa msaada wa ndege ya kivita.

Je, ni hatari hivyo kweli?

"Hali imebadilika. Leo hatuna tena ndege zisizo na rubani zile nzuri kabisa. Hasa katika zile zinazoshiriki mashambulizi. Na hapa suala sio ubora, lakini wingi", - hivi ndivyo kamanda wa kitengo cha uchunguzi wa anga wa Kikosi cha wanajeshi wa Ukraine, mtaalamu wa ndege zisizo na rubani, Yuriy Kasyanov, alielezea hali hiyo mwanzoni mwa Novemba.

Shida, kwa maoni yake, ni uhaba mkubwa wa droni za UAV, haswa zile zinazoshiriki mashambulizi, katika jeshi la Ukraine.

Na hii, kwa upande wake, inahusishwa na ukweli kwamba huko Ukraine, tofauti na Urusi na Irani, mchakato wa uzalishaji mkubwa wa droni haukuwahi kuzinduliwa.

Mtaalam anaita kauli za maafisa wa Ukraine kuhusu Moscow kutokuwa na uwezo wa kuzalisha silaha za aina hii bila umeme wa kigeni kuwa dhihirisho la ‘’uzalendo wa kutisha’’ na mtazamo mkali kwa adui.

‘’Tumepoteza mpango wa kutumia ndege zisizo na rubani. Adui tayari ameanza kutumia kwa wingi ndege zisizo na rubani za kamikaze za aina za Cube na Lancet, na tunafanya kila kitu kwa kuchelewa,’’ alieleza BBC.

.

Chanzo cha picha, OLEKSANDR SLADKOV

Maelezo ya picha,  Kombora la Ukraine kwenye lenzi ya ndege isiyo na rubani ya upelelezi ya Urusi. Ndani ya sekunde moja tu, itapigwa na ndege isiyo na rubani ya Lancet

Kulingana na yeye, tangu mwanzo wa vita, jeshi la Ukraine kwa kweli limesheheni ndege zisizo na rubani ambazo zimeundwa upya kwa madhumuni ya kijeshi.

Lakini wanajaribu kuzindua uzalishaji wa viwandani wa UAV maalum za kushambulia tu sasa hivi.

Pia kuna usaidizi mdogo kutoka kwa washirika wa Magharibi kwenye hili.

Israeli, ambayo hutengeneza droni za UAV zinazofanana, kimsingi haitoi silaha za kuua kwa Kyiv, na Marekani haina idadi inayohitajika kutoa droni nyingi za UAV.

Kuhusu ufanisi wa droni za Kirusi za kamikaze, mtaalam huelekeza angalizo kwa zile ndogo na za masafa mafupi.

Hata hivyo, inasemekana kuwa droni za UAV hazipaswi kulinganishwa, kwa sababu zinafanya kazi tofauti kimsingi.

Ikiwa ndege isiyo na rubani ya Irani itatumika kuharibu miundombinu mikubwa katika kina cha eneo la adui, basi droni za "Lancet" ni za vitani na zinafanya kazi kwenye rada za kibinafsi au mifumo ya ulinzi wa anga moja kwa moja karibu na vitani.

Haya ni matabaka tofauti kabisa. Ni kama kulinganisha kombora na ndege ya kivita inayoendeshwa na mtu. Hizi ni silaha tofauti kabisa na mbinu tofauti kabisa za vita zinatumika.

Kuhusu ushawishi wa ndege zisizo na rubani za Kirusi za kamikaze wakati wa vita nchini Ukraine, mhojiwa wa BBC ni mwangalifu sana katika tathmini zake.

Droni za Lancet za Urusi zimetoka wapi?

Ukweli kwamba ndege zisizo na rubani zilionekana nchini Urusi hata kidogo ni matokeo ya shughuli ya kibinafsi ya kampuni ya ZALA Aero, ambayo imekuwa ikijihusisha na droni tangu katikati ya miaka ya 2000.

Hata hivyo, walijishughulisha na silaha za uvamizi tu katika miaka ya 2010.

Kama mtaalam wa Kirusi, ambaye alitaka asitajwe, aliiambia BBC, Wizara ya Ulinzi ya Urusi haikupendezwa na ndege kama hizo, na makampuni ya kibiashara, yalipotambua kuwa wanajeshi hawatapendezwa nayo, hawakuhusika katika maendeleo kama hayo.

ZALA Aero, ambayo sasa ni sehemu ya kundi la makampuni ya Kalashnikov, ilianza kutengeneza silaha za kivita, ikitegemea uuzaji nje ya nchi.

Droni za ‘’Lancet’’ sio bidhaa yao ya kwanza, kabla ya kutolewa kwa ndege isiyo na rubani ya ‘’Kub’’, ambayo sasa inatumiwa pia na jeshi la Urusi.

Mnamo mwaka wa 2019, droni aina ya ‘’Cube’’ iliwasilishwa kwenye maonyesho huko Abu Dhabi.

Na droni ya ‘’Lancet’’ ikaonyeshwa katika msimu wa joto wa 2019 kwenye maonyesho ya ‘’Jeshi’’ katika mkoa wa Moscow, na yalikuwa maonyesho makubwa.

Hata hivyo, kama mtaalam wa Urusi alivyosema, jeshi la Urusi lilipendezwa na ndege zisizo na rubani za kamikaze baada tu ya kujaribiwa huko Syria.