Je, mfumo wa Phoenix Ghost Drone unaopelekwa Ukraine ni nini?

Chanzo cha picha, US ARMY AMRDEC PUBLIC AFFAIRS
Phoenix Ghost ni aina ya silaha zinazotembea kumaanisha kwamba husalia angani kwa muda mrefu kabla ya kupata shabaha.
Marekani inatuma zaidi ya ndege 500 za Phoenix Ghost kwenda Ukraine kama sehemu ya kifurushi chake cha dola milioni 270 ambazo Idara ya Ulinzi ya Marekani ilitangaza Ijumaa.
Tovuti ya Defense Express ilinukuu taarifa zilizotolewa na mshauri wa ofisi ya Rais wa Ukraine, Oleksii Arestovysch, ambaye alielezea ndege isiyo na rubani ya Phoenix Ghost kama "wijeti nzuri."
Ndege isiyo na rubani hutoshea ndani ya mkoba na inaweza kuning'inia hewani kwa saa sita. Ina mwongozo wa ‘infrared’, kumaanisha kuwa inaweza kufanya kazi usiku na kuharibu shabaha za silaha za wastani.
"Mia tano na themanini ya vitengo kama hivyo ni sawa na malengo 350 yaliyoharibiwa kwa nyuma," alisema.
Kulingana na Defence News, Phoenix Ghost, ambayo ilitengenezwa na Marekani mahususi kwa matumizi nchini Ukraine, inafanya kazi kwa njia sawa na AeroVironment Switchblade.
Kama vile Switchblade, ndege isiyo na rubani ya Phoenix Ghost ni aina ya silaha inayoteleza, kumaanisha kwamba inasalia hewani kwa muda mrefu kabla ya kupata shabaha.
Uwezo wa Phoenix Ghost

Chanzo cha picha, Getty Images
Tangazo la Biden la msaada wa kijeshi ni la 16 kutoka kwa orodha ya idara ya Ulinzi DoD kwa Ukraine ambayo Utawala wa Biden umeidhinisha tangu Agosti 2021," Idara ya Ulinzi ilisema katika taarifa yake Ijumaa.
Silaha hiyo ilundwa na Aevex Aerospace huko California, Phoenix Ghost inafaa dhidi ya magari ya kivita ya wastani, Politico ilimtaja mjumbe mstaafu wa bodi ya Aevex Lt. Jenerali David Deptula akisema.
Phoenix Ghost ina uwezo wa kuruka wima, inaweza kufuatilia lengo kwa hadi saa sita na inaweza kufanya kazi usiku kwa kutumia vitambuzi vya infrared, Deptula aliiambia Politico.
Ingawa Switchblade inaweza kuruka kwa chini ya saa moja pekee, Phoenix Ghost inaweza kusalia angani kwa muda mrefu zaidi.















