Sayansi: Kipimo cha damu kinavyoweza kugundua mawazo ya kujiua

gb

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

    • Author, Nikolay Voronin
    • Nafasi, BBC

Sonona na mawazo ya kujiua vinaweza kutambuliwa kwa kipimo rahisi cha damu, wanasema wanasayansi wa Chuo Kikuu cha California, San Diego School of Medicine (USA).

Waligundua kuwa msongo wa mawazo, sonona na mawazo ya kujiua vinaweza kuathiri metaboliki ya mwili, kama vile magonjwa ya kuambukiza na saratani.

Mabadiliko ya metaboliki husababisha mabadiliko katika muundo wa kemikali za damu, ambapo kemikali maalumu huonekana zenye kuashiria uwepo wa shida fulani katika mwili.

Kila ugonjwa una dalili zake ambazo zinaweza kugunduliwa wakati wa kipimo cha damu. Hii ina maana kwamba - kipimo kinaweza kuonyesha mgonjwa ana msongo wa mawazo au na hata mawazo ya kujiua.

"Sababu za matatizo ya akili na athari zake kwenye mwili haziathiri ubongo pekee," aeleza Robert Navio, profesa katika idara ya dawa na ugunduzi wa magonjwa katika Chuo cha Tiba cha San Diego.

Katika baadhi ya kesi, sonona haiwezi kutibika. Wengi wa wagonjwa hawa hupata mawazo ya kujiua, na mmoja kati ya watatu hujaribu kujiua angalau mara moja.

Ili kugundua dalili, wanasayansi walipima damu ya mamia ya wagonjwa walio na sonona sugu na kulinganisha na matokeo ya idadi sawa ya watu wasiokuwa na sonona.

Ilibainika kati ya mamia ya kemikali katika damu, tano zinaweza kutumika kama dalili ya uwepo wa sonona sugu na mawazo ya kujiua kwa mgonjwa.

Tiba zinaweza kusaidia

rgfv

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Njia za matibabu za ugonjwa wa sonona zinajulikana. Matibabu ya sonona yanaweza kupunguza tatizo hilo au kuzuia lisiendelee na kufanya mawazo ya kujiuwa kupotea.

Matatizo ya akili ni mengi sana - kutoka uraibu wa dawa za kulevya hadi magonjwa ya akili ya kuchanganyikiwa. Magonjwa hayo yamegunduliwa kwa karibu watu bilioni 1 duniani kote.

Ambayo ni maarufu zaidi ni matatizo ya wasiwasi na sonona - hugharimu uchumi wa dunia karibu dola trilioni 1 kila mwaka, ni sawa na Pato la Taifa la Uturuki au Saudi Arabia.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), katika kipindi cha miaka 20 iliyopita, idadi ya watu wanaojiua imekuwa ikipungua kwa kasi - hata nchini Urusi - ambayo iko katika orodha ya nchi tatu za mwanzo zenye tatizo hilo.

Zaidi ya watu laki saba hujiua kila mwaka. Wanaume hujiuwa karibu mara mbili kuliko wanawake. Nchini Urusi wanaume hujiuwa mara nane.

Kujiuwa ni sababu ya nne ya vifo kwa vijana wa jinsia zote wenye umri wa miaka 15-30. Ingawa matukio ya kujiuwa yanazidi kupungua hata kwa vijana.

Imetafsiriwa na Rashid Abdallah na kuhaririwa na Dinah Gahamanyi