Ni uhalifu gani wa kivita ambao Urusi inashutumiwa katika Ukraine?

Chanzo cha picha, Reuters
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, anasema vikosi vya Urusi huenda vilitekeleza zaid ya makosa 400 ya uhalifu wa kivita katika Kherson kabla ya kuondoka katika mji huo.
Kulingana na Ukraine , takriban uhalifu wa kivita upatao 34, 000 huenda ulitekelezwa na vikosi vya Urusi kuanzia mwezi wa Februari.
Uhakifu wa kivita ni nini?
"Hata vita huwa vinakuwa na sheria", kama kamati ya kimataifa msalaba mwekundu Red Cross inavyosema.
Sheria hizi huwekwa katika mikataba inayoitwa makubaliano ya Geneva – Geneva Conventions pamoja na sheria nyingine za kimataifa na makubaliano.
Vikosi vya kijeshi haviwezi kuwashambulia raia – au miundo mbinu ambayo ni muhimu kwa maisha yao ya kila siku.
Baadhi ya silaha zilipigwa marufuku kwa kutoweza kubagua maeneo au watu wanaolengwa au kwa maafa makubwa zinazoweza kusababisha - kama vile, mabomu ya kutegwa ardhini ya anti-personnel na silaha za kikemikali pamoja na za kibaiolojia.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Wagonjwa na majeruhi wanapaswa kuhudumiwa wakiwemo wanajeshi waliojeruhiwa , weny haki kama wafungwa wa vita.
Makosa makubwa kama vile mauaji, ubakaji na utekaji nyara au mauaji ya wkundi la watu wengi kwa pamoja hufahamika kama "uhalifu dhidi ya binadamu" au katika hali fulani huitwa "mauaji ya kimbari"- (genocide).
Rais Zelensky anasema kuwa wachunguzi katika jimbo la Kherson region tayari wamekusanya taarifa za makosa ya uhalifu wa kivita 400 uliotekelezwa na vikosi vya Urusi wakati wauvamizi wao.
" Miili ya raia waliouawa na wanajeshi imekuwa ikipatikana," alisema, katika hotuba yake iliyotangazwa kwenye televisheni. "Jeshi la Urusi liliacha nyuma maasi kama yali lililoyaacha wakati lilipoingia kwenye majimbo mengine nchini ."
Wakazi katika baadhi ya maeneo ya jimbo la Kherson lililovamiwa na vikosi Urusi wamekuwa wakiwaambia waandishi wa habari kuhusu mauaji ya vikosi vya Urusi nautekaji nyara wa raia, lakini BBC haikuweza kuthibitisha ripoti za aina hiyo kwa duru huru.
Urusi inakanusha kwamba vikosi vyake vilitekeleza maasi katika maeneo vilivyoyavamia.
Ni uhalifu gani mwingine ambao Urusi inasemekana kuutekeleza katika Ukraine?
Mwendesha mashitaka mkuu wa Ukraine, Andriy Kostin, alisema mwezi septemba kwamba ofisi yake ilikusanya taarifa kuhusu uhalifu 34, 000 ambao huenda unaweza kuwa uhalifu wa kivita uliotekelezwa na vikosi vya Urusi , na unaweza kuwa kesi ya mauaji ya kimbari.
Makaburi ya watu wengi yamepatikana katika maeneo kadhaa ya Ukraine ambayo awali yalivamiwa na vikosi vya Ukraine, mkiwemo baadhi ambayo yana miili ya raia inayoonyesha ishara za mateso.
- Mwezi Aprili, zaidi ya miili 400 ya raia ilipatikana katika Bucha, mji uliopo viungani mwa Kyiv.
- Katika Septemba, miili 450 – mingi kati yake ikiwa ni ya raia – ilipatikana katika kaburi la watu wengi katika Izuium, katika jimbo la Kharkiv.
- Mwezi Machi , vikosi vya Urusi vilifanya shambulizi la anga katika ukumbi wa maonyesho katika Mauripol ambao ulikuwa unatumiwa kama maficho ya watoto
- Hospitali katika Mariupol pia ilishambuliwa mwezi Machi.
Ukraine inasema nini kilitokea katika Kherson?

Chanzo cha picha, Reuters
Je uhalifu unaweza kushitakiwa vipi?
Mahakama za Ukraine tayari zimemshitaki mwanajeshi mmoja wa Urus.i
Kamanda mmoja wa kikosi cha vifaru wa Urusi mwenye umri wa miaka 21- Vadim Shishimarin alifungwa kifungo cha maisha jela kwa kumpiga risasi raia mwenye umri wa miaka 62, Oleksandr Shelipov, kaskazini -mashariki mwa Chupakhivka ambaye hakuwa na silaha, siku chache baada ya kuanza kwa uvamizi.
Inaweza kuwa rahisi sana, hatahivyo, kuwashitaki wanajeshi binafsi kwa uhalifu wa kivita kuliko makamanda au maafisa wa ngazi ya juu wa kisiasa.

Chanzo cha picha, Reuters
Hugh Williamson wa Human Rights Watch anasema kubaini "viongozi wa vita"ni muhimu sana kwa ajili ya kesi zozote zijazo – ikiwa ni pmaoja na kubaini iwapo kiongozi wa aliagiza au aliidhinisha maasi – au kuyafumbia jicho.
Mahakama ya kimataifa ya jinai (ICC) inachunguza uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu uliotendeka kuanzia mwaka 2013 katika Ukraine, kabla hata bado Urusi haijalitwa jimbo la Crime kutoka kwa Ukraine.
Mwendesha mashitaka wake, wakili Muingereza Karim Khan, anaamini kuna sababu za kimsingi za kuamini uhalifu wa kivita ulifanyika.
Hatahivyo, ICC haina mamlaka ya kuwakamata washukiwa, na Urusi haikutia saini makubaliano ya kuanzishwa kwa mahakama hiyo - kwahiyo huenda isiwapeleke washukiwa katika mahakama mahakama hiyo.
Kwa ujumla ICC huchukua mashitaka ya uhalifu wa kivita kutoka kwa nchi ambapo mifumo ya mahakama ni dhaifu sana kuweza kuendesha mashitaka hayo zenyewe.
Hadi sasa, inaonekana mahakama za ukraine zimekuwa zikikusanya kesi zake zenyewe. Kudikia mwisho wa Agosti, mwendesha mashitaka wake mkuu, alikuwa amewashitaki washukiwa 135 wa uhalifu wa kivita.

Chanzo cha picha, Getty Images
ICC inaweza kuanzisha mashitaka dhidi ya viongozi wa kisiasa kwa "kufanya vita vya uchokozi". Hii ni pamoja na uvamizi usio na sababu au mzozo ambao haukutokana na msingi wa kujilinda.
Hatahivyo Profesa Philippe Sands, amtaalamu wa sheria za kimataifa katika chuo kikuu cha London, anasema ICC haiwezi kumshitaki rais wa Urusi Vladimir Putin kwa hili – pia , kwasababu nchi yake haikusaini makubaliano ya kuanzishwa kwa mahakama ya ICC.
Katika nadharia,Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linaweza kuiomba mahakama ya ICC kuchunguza ihalifu huu. Lakini Urusi inaweza kulipigia kura ya veto.
Prof Sands anasema viongozi wa dunia wanapaswa kuanzisha mahakama ya kushitaki uhalifu wa uchokozi katika Ukraine















