Watu ambao hupata 'mzio' kutokana kwa wanadamu wenzao

Chanzo cha picha, Getty Images
Baadhi ya watu ni mzio kwa wengine - lakini siri ya jinsi hili linavyotokea inafafanuliwa
Maura anaamini kondomu ziliokoa maisha yake.
Akiwa sasa ana umri wa miaka 43 na makazi wa jimbo la Ohio, Marekani, Maura anasema tatizo hilo lilianza katika miaka yake ya ishirini, lilipomjia polepole. "Niligundua kuwa sehemu zangu za siri ziliungua baada ya ngono [bila kinga]," anasimulia.
Hatimaye aliachana na mtu aliyekuwa mpenzi wake, na akaanza kushiriki ngono na mwingine ambaye alikuwa amejitolea kutumia kondomu. "Halikuwa tatizo hadi usiku mmoja wakati tulipokuwa tumelala kitandani baada ya ngono nikahisi ulimi wangu ulianza kuvimba ghafla," Maura anasimulia.
"Mwenzangu alipoona kinachotokea, akapiga kelele, 'Unakosa hewa!' na akashika inhaler ([kifaa cha kujiongezea pumzi] yangu... Aliweza kuingiza inhaler yangu kwenye kona ya mdomo wangu, na akaanza kuniongezea hewa ya pumzi. Kwa bahati nzuri, bado nilikuwa nikipumua vya kutosha kuweza kupokea dawa kwenye mapafu yangu."
Maura, ambaye pia ana maradhi ya pumu na mizio kadhaa, anaamini kuwa kondomu siku ile ilikuwa imevuja. Yeye na mwenzi wake wa muda mrefu sasa wako waangalifu zaidi kuhusu matumizi ya kondomu. Hadi ilipomtokea, hakujua inawezekana kuwa na mzio wa mbegu za kiume, anasema.
Ingawa ni nadra sana, watu wengine hupata athari kali za kinga ya miili ya watu wengine. Tatizo hili ambalo mara nyingi halieleweki linaweza kuathiri sio tu afya, bali pia kazi, uhusiano na kwa ujumla jinsi mtu anavyoishi ulimwenguni. Lakini jinsi athari hizi zinavyotokea, na ni nini husababisha, bado ni ya kushangaza.
Je, ni mzio wa kweli, au kitu kingine chochote? Wanasayansi wanapoanza kukusanya vidokezo, majibu haya ya kushangaza yanafunua maarifa juu ya kemia ya miili yetu na mambo ya kushangaza ya mfumo wa kinga wa binadamu.
Kutoka kwa ngozi
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Mara nyingi, kuathiriwa kwa mwili wa mtu mwingine kunahusiana na bidhaa za nje zinazojitokeza katika mwili huo. Kwa mfano, ngozi inaweza kubeba manukato ya aina fulani , ikiwa ni pamoja na deodorant na losheni zinazopakwa baada ya kunyoa ndevu aftershave). Zaidi ya manukato 150 yanahusishwa na mzio wa mgusano wa mwili.
Kinachochochea mzio sio wazi mara zote. Mwanamke mmoja wa Marekani aliye na aina kali ya ugonjwa wa uanzishaji wa seli za kipekee ambapo seli za kupambana na maambukizi hufanya kazi vibaya, alipata athari ya kudhoofisha mzio kwa harufu ya mumewe.
Sabine Altrichter, daktari katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Kepler nchini Austria, anasema kwamba ingawa kiungo hicho hakijathibitishwa, baadhi ya wagonjwa walio na matatizo ya seli za aina hii wanashuku kuwa ni athari kwa harufu asilia ya mwili au kemikali zinaweza kutibiwa na ngozi ya watu wengine.
Ngozi hutoa hutoa kemikali nyingi ambazo huchangia harufu ya mwili. Gesi hizi za ngozi zinaweza kujumuisha kemikali kama toluini, ambayo hutokea katika mafuta yasiyosafishwa na hutumiwa kutengeneza bidhaa ikiwa ni pamoja na rangi na plastiki.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kundi moja la watu ambao wanaweza kutoa mwanga juu ya athari kwa wanadamu wengine ni wale wanaougua hali ya kushangaza mzio wa PATM.. PATM ni jambo lisilo la kawaida na la kipekee ambapo wengine mara nyingi hupata dalili za aina ya mzio, kama vile kukohoa na kuhisi kupaliwa
Mnamo 2023, Yoshika Sekine, profesa wa kemia katika Chuo Kikuu cha Tokai cha Japani, na wenzake walichunguza gesi za ngozi zinazotolewa na wale wanaoripoti dalili za PATM. Kati ya gesi 75 za ngozi ambazo timu ilizifanyia uchunguzi, toluene ilikuwa na uwezekano mkubwa wa kuwepo miongoni mwa watu hao. Watu katika kikundi cha PATM walitoa mara 39 zaidi ya kemikali hii, kwa wastani, kuliko wale wasio na hali hiyo.
"Toluene huvutwa kupitia hewa wakati wa kupumua. Kwa kawaida hutengenezwa na ini na kutolewa kwenye mkojo," Sekine anaelezea. "Hata hivyo, wagonjwa wa PATM wana uwezo mdogo wa kuvunja toluini, na kusababisha mkusanyiko wake katika damu na kutolewa baadaye kupitia ngozi," anasema.
Sekine anabainisha kuwa dhana yenyewe ya PATM bado haijatambuliwa sana, na hakuna vigezo vya uchunguzi wake.
Wakati huo huo, mzio wa jasho kwa ujumla unahusishwa na jasho la mtu binafsi, badala ya wengine. Kuhusu nywele, katika hali nadra ambapo mzio unaohusiana na nywele za binadamu umerekodiwa, mmenyuko haujasababishwa na mzio katika nywele zenyewe, bali mzio katika vitu vya nje: kwa mfano, protini ya paka ambayo huingia kwenye nywele za wamiliki wa paka
Kutoka kwa majimaji ya mwili
Athari za mzio pia zinaweza kuchochewa na kitu maaluu kinachousababisha ambacho kimebebwa katika maji ya mwili. Katika kisa kimoja cha Uingereza, mwanamke aliye na mzio wa karanga za Brazil alipata upungufu wa kupumua baada ya kufanya ngono na mwanamume ambaye alikuwa amekula karanga zilizochanganywa masaa machache mapema, ingawa alikuwa amesafisha meno yake, kucha na ngozi. Karanga pia zimesababisha athari ya mzio wakati wa kubusu kwa watu walio na mzio mkali.
Ingawa karanga ndizo allergen inayoripotiwa sana inayoleta shida wakati wa kubusu, mate pia yamesababisha athari za mzio kufuatia ulaji wa matunda, mboga mboga, dagaa na maziwa. Wanawake walio na mzio wa viuavijasumu wameonekana kuathirika vibaya baada ya kufanya tendo la ngono ya uke na (ikiwezekana) ya mdomo na watu ambao walikuwa wametumia dawa hizo.
Lakini zaidi ya vitu hivi vya nje ya mwili vinavyosababisha mzio, protini ndani ya maji fulani ya mwili yenyewe zinaweza pia kusababisha athari. Maji maji ambayo matabibu wengine wanayafahamu, ingawa bado kuna mapungufu makubwa katika ufahamu, ni shahawa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mzio wa shahawa, au mzio wa ute wa seminal, unahusiana na kupata dalili kuanzia upele wa ngozi , muwasho wa mzio ambao unaweza kutishia maisha, baada ya kuathiriwa na majimaji ya watu wawili.
Imerekodiwa hasa kwa watu walio na umri wa miaka 20 na 30, ingawa kumekuwa na visa chini ya 100 vilivyorekodiwa kwa jumla, kulingana na utafiti wa mwaka 2024. Allergen inayohusishwa mara nyingi huu ni antijeni maalum ya kibofu, dutu ambayo inaweza kusababisha mwitikio wa kinga, katika ute wa mwili (plasma).
Haya ni majimaji mbali na manii, ambayo hutengeneza shahawa nyingi, na mzio hupatikana kutokana na protini ndani yake, badala ya manii yenyewe.
Visa vya mzio wa vinaweza kuwa vya ndani au vya kimfumo zaidi. Lakini katika ripoti moja ya kisa cha Uhispania, mwanamke ambaye hakuwahi kupata athari ya mzio baada ya ngono ya uke alipoteza fahamu na kupata dalili zingine za anaphylaxis kufuatia ngono ya kuingiliwa nyuma.
Aligunduliwa na kuathiriwa kutokana na majimaji ya shahawa. Mwanamke mmoja nchini Marekani pia alipata uvimbe na upele katika hali isiyo ya ngono, wakati ngozi yake ilipogusana wa kujamiiana.
Dalili za ndani zinaweza kujumuisha maumivu makali na kuhisi kuungua mara baada ya kujamiiana. "Ni [inaripotiwa] kama asidi," Bernstein anasema. Mmoja wa wagonjwa wake aliielezea kuhisi kama "kama sindano elfu moja zinazokwama kwenye uke wako."
Mtu anaweza kuathiriwa kwa shahawa za wenzi wengi au mmoja tu, Bernstein anabainisha. Utambuzi kawaida huhusisha jaribio la ngozi kwa kutumia sampuli mpya ya maji ya shahawa kutoka kwa mwenzi wa ngono.
Katika majaribio yakee, Bernstein kawaida huwaona wanawake katika uhusiano wa mke mmoja na wanaume, mara nyingi wanapojaribu kupata mimba. Watu wengine husafiri umbali mrefu kushauriana naye, kwani hakuna mamlaka nyingi zinazoshughulikia tatizo la mzio utokanao na shahawa.
Wagonjwa wengi hupuuzwa kando au huanza kutumia matibabu makali ya steroid kwasababu wataalamu wa matibabu hawajui la kukabiliana nao, Bernstein anasema.
Hata hivyo, Bernstein anaeleza kuwa majaribio yake yanaweza kumsaidia karibu kila mtu aliye na mzio wa shahawa.
Kuna kutokuwepo kwa data kuhusu mzio wa shahawa kati ya wanaume wanaofanya ngono na wanaume.
Bernstein anasema hajawahi kuona kisa hiki, ingawa haijulikani ni kwanini. Alijiuliza ikiwa dalili zinaweza kuhusishwa na hali fulani ndani ya uke, ingawa hii haielezi kisa ambacho kilitokea baada ya ngono ya kuingiliwa nyuma kati ya mwanamume na mwanamke.

Chanzo cha picha, Getty Images
Bernstein na wenzake waligundua kuwa iliripotiwa kuwa ilikuwa salama na yenye ufanisi sawa kuweka matibabu, kwa utaratibu wa wakati mmoja wa masaa mawili. Kwanza, walitenganisha manii kutoka kwa majimaji ya mbegu za kiume. Kisha wakapunguza maji hayo hadi sehemu moja katika milioni au moja kati ya milioni kumi, kulingana na jinsi athari za mgonjwa zilivyokuwa kali. Kisha, kwa vipindi vya dakika 15, waliingiza majimaji hayo kwenye uke wa mgonjwa.
Hatua kwa hatua walitumia viwango vikali vya maji, ili mgonjwa aendeleze uvumilivu mkubwa. Wakati wote, waliendelea kumfuatilia mgonjwa. Walifuatilia kama , "hawana athari nyingi za kimfumo na wanaweza kuvumilia kujamiiana bila kinga baadaye" na angalau mwenzi mmoja , Bernstein anasema.
Kwa ujumla, kuathiriwa na shahawa mara nyingi ni jambo ambalo limesalia kutoeleweka. Kuna habari chache zaidi kuhusu maji mengine yanayoambukizwa wakati wa ngono.
Hakuna utafiti uliochapishwa kuhusu uwezekano wa mzio wa maji ya kizazi yanayotolewa na seli za nyonga na uke, ambayo husaidia kulainisha eneo hili na kutoa ulinzi kutoka kwa vimelea vya magonjwa. Hata hivyo, Marek Jankowski anaamini kwamba ameona angalau mtu mmoja aliye na hali hii. Jankowski, profesa msaidizi wa ngozi katika Chuo Kikuu cha Nicolaus Copernicus n
chini Poland, anasema aliwahi kumtibu mgonjwa ambaye alikuja kwake baada ya kuonana na madaktari wengine wengi. Mgonjwa aliripoti kwamba kama dakika 30 baada ya kujamiiana ukeni, sehemu zake za siri huwaa nyekundu na kuwasha. Uso wake pia ulimuwasha. Kwa mgonjwa, hii ilionekana kama mzio, lakini madaktari walipinga wazo hili, anasema Jankowski.
Hata hivyo, Jankowski aliweka akili wazi, akitafuta visa vingine vya uwezekano wa mzio wa maji ya nyonga yanayotolewa na wanawake wakati wa shughuli za ngono. "Hatimaye mgonjwa alipata matibabu yaliyofana ya dawa ya mzio ya antihistamines," anaripoti. Kisa hicho pia kilimsukuma Jankowski na wenzake kufanya utafiti, uliochapishwa mnamo 2017.
Watafiti walichunguza madaktari wengine wa ngozi pamoja na watu ambao wanaweza kuwa na hali hii. Moja ya tano ya madaktari wa ngozi waliojibu walikuwa wameshuhudia visa kama hivyo, waliripoti, ingawa madaktari wengi walibaki na shaka kwamba hali hiyo ilikuwepo.
''Athari za kihisia zinaweza kuwa ngumu, kwa wagonjwa na wenzi wao''
Kulingana na utafiti huu, wagonjwa waliripoti uwekundu, kuwasha, kuhusi kuungua, na uvimbe kufuatia mgusano wa mwili na watu wengine. Ripoti zao zilisababisha Jankowski na wenzake kukadiria kuwa mzio wa maji ya nyonga yanayotolewa na wanawake wakat iwa kujamiiana, ulikuwa wa kawaida kama mzio wa shahawa, ambao unadhaniwa kuathiri angalau makumi ya maelfu ya watu nchini Marekani pekee.
Hata hivyo, "kiwango cha sasa cha ushahidi wa hali ya mzio wa maji ya nyonga husababishwa hasa na kimazingira tu na utafiti zaidi katika uwanja huu utahitajika," Jankowski anaelezea.
Tofauti moja kati ya mzio wa shahawa dhidi ya maji ya mbegu za kiume za uzazi kwamba kondomu hazitawezekana kupunguza dalili za mzio wowote , kwani kondomu haziwezi kulinda uke na korodani.
Lakini tiba ya mzio ya dawa za antihistamines ilionekana kusaidia wahojiwa wa utafiti na mzio wao wa maji ya kizazi, kulingana na matokeo ya uchunguzi wa Jankowski na waandishi wenzake.
Kwa watu ambao wana mzio wa kipengele fulani cha wenzi wao, matokeo yanaweza kuwa makubwa. Maura anaamini kwamba uelewa waathari za shahawa ulichangia katika uamuzi wake na wa mwenzi wake wa kutopata watoto, kwasababu anatarajia kwamba ingekuwa ghali kupata suluhisho ambalo lilimuwezesha kuepuka kuathiriwa na shahawa.
Athari za kihisia zinaweza kuwa ngumu, kwa wagonjwa na wenzi wao. Ingawa uhusiano wa Maura uko salama na mpenzi wake anafurahi kutumia kondomu, "aliniambia kwamba alichukizwa na wazo kwamba nilikuwa na mzio wa shahawa yake," anasema. "Hanilaumu kwa hilo."
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi












