Faida za kiafya za kushiriki tendo la ndoa mara kwa mara

Chanzo cha picha, getty Images
Tendo la ngono ni tukio la kufurahisha, iwe unalifurahia peke yako au na mtu mwingine, hasa wakati kuna mvuto wa kina kati yako na mtu unayeshiriki naye au mtu muliye na uhusiano wa karibu.
Inaweza pia kuwa njia isiyo ya kawaida ya mawasiliano, kusaidia kuwasilisha hisia nzito na kuimarisha uhusiano.
Kwa kuwa ni sehemu muhimu ya maisha, mengi yameandikwa kuhusu jinsi na wakati wa kutenga muda wa kushiriki tendo hili.
Walakini, hakuna jibu moja: karibu kila wakati inategemea mtu binafsi, mshirika na muktadha. Ukweli pekee ni kwamba inahitaji maelewano kati ya wahusika, ambao lazima wajisikie vizuri na kuridhika katika matarajio yao ya pande zote.
Tukijua kwamba kila mtu ni mtu yuko tofauti katika mahitaji na maadili yake, hapa tunaeleza kwa undani faida ambazo ntendo la gono linaweza kuleta linapotekelezwa mara nyingi na kadri kila muhusika anavyoona kuwa linafaa.
Inaboresha hisia
Wakati wa kujamiaana ubongo hutoa homini za endorphins, ambazo huzalisha msisimko, kuridhika na ustawi.
Homoni hiyo uhusiana na furaha na utulivu kabla na baada ya kufika kilele .
Hatahivyo licha ya kutufanya tuhisi vyema, ngono haiwezi kusemwa kwamba inaweza kutumika kama tiba ya mfadhaiko.
Ndiyo, inaweza kutupa nyakati chanya ambazo, zikiongezwa kwa wengine, huongeza hisia zenye kupendeza. Lakini dalili za unyogovu zinahitaji mbinu ngumu zaidi na mara nyingi za matibabu.
Mwishowe, ngono hurahisisha kulala, ambayo ina athari chanya kwa kukosa usingizi ambayo mara nyingi huambatana na shida za afya ya akili.
Huondoa msongo wa mawazo
Uzoefu wa kibinafsi wa mfadhaiko usio na dhiki hutokea tunapohisi kulemewa na mahitaji ya maisha ya kila siku na kuvuruga hisia zetu na hamu yetu ya tendo la ngono.
Tunapoishi kwa muda mrefu na hali zinazotuzidi kimaisha, hamu ya mara kwa mara ya kutaka kushiriki katika tendo la kujamiana hushuka, wakati mwingine unaweza kutafsiri kuwa kuridhika kidogo na wapenzi wetu.
Hii inaweza kutokana na viwango vya cortisol, homoni muhimu ya kukabiliana na mahitaji ya maisha, lakini inadhuru wakati mkusanyiko wake katika mwili unaongezeka sana au kwa muda mrefu sana.
Kwa maana hii, ngono inaweza kutusaidia kupunguza msongo wa mawazo unaohusishwa na kuzidiwa na maisha, ingawa msongo wa mawazo wenyewe kwa njia ya kushangaza hupunguza hamu ya ngono.
Jambo la kustaajabisha ni kwamba wanandoa wenye furaha zaidi huwa na tabia ya kutafuta mahusiano ya ngono siku zinazofuata siku yenye mkazo. Pia ndio wanaofaidika zaidi na athari chanya za ngono.
Huimarisha mfumo wa kinga
Kujamiana mara kwa mara huimarisha ulinzi wetu wa kisaikolojia dhidi ya virusi, bakteria na pathogens nyingine.
Kuna tafiti zinazoonyesha kuwa kufanya mapenzi mara tatu kwa mwezi kunaweza kutulinda dhidi ya virusi vya corona. Ugunduzi huo unaenea, bila shaka, kwa magonjwa mengine ya kuambukiza.
Faida kwenye mfumo wa kinga haitegemei umri na aina ya shughuli za ngono, ambayo mtu yeyote anaweza kuipata kwa nyakati tofauti za maisha yake.
Kwa kifupi, ushahidi unaonyesha kwamba tunapojamiiana mara kwa mara, mfumo wetu wa kinga unakuwa sugu zaidi kwa vitisho.
Hupunguza shinikizo la damu na maumivu
Tendo la ngono husaidia mfumo wa moyo na mishipa. Inajulikana kuwa kujamiiana kama wanandoa huongeza shinikizo la systolic na diastoli, ambayo huimarishwa wakati wa kufika kilele na kupungua muda mfupi baadaye.
Katika vijana, kujamiiana mara moja hutafsiriwa katika takriban visawa sita vya kimetaboliki, yaani, matumizi ya nishati mara sita zaidi ya ile inayotumiwa wakati wa kupumzika.
Utafiti mwingine wa hivi majuzi unapendekeza kwamba kudumisha tendo la ngono wakati wa uzee hupunguza tukio la matatizo ya moyo na mishipa, na kusaidia kupunguza maumivu.
Huimarisha uhusiano na uhusiano wa kihisia
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Ngono ni muhimu kwa ajili ya kujenga na kudumisha uhusiano kati ya wanandoa .
Hii inahusiana na uzalishaji wa oxytocin, homoni inayochangia kuimarisha aina zote za mahusiano (ikiwa ni pamoja na ule wa mama na mtoto wakati wa kunyonyesha).
Oxytocin husaidia kudhibiti tabia za kijamii na kihisia na ni msingi kwa ustawi. Pia hurekebisha hofu, wasiwasi na mafadhaiko; zinazozalishwa hasa nyakati za kufanya mapenzi kama vile kukumbatia, kubembeleza na kupiga busu.
Hii inaonyesha umuhimu wa ngono kutoishia kwenye sehemu za siri pekee, bali kujumuisha aina nyingine, fiche zaidi za mwingiliano. Ingawa kufikia kilele ndio sehemu ya juu ya mwitikio wa ngono, uhusiano wa karibu haupaswi kuzunguka au kueleweka kama haujakamilika ikiwa haujafikiwa.
Kwa kifupi, ngono huleta faida kadhaa. Kipaumbele kinapaswa kuwa kuzoea mahitaji ya watu wanaohusika, ili kuitengea wakati mzuri na wa utulivu.
Kuweka shinikizo kwa nguvu au marudio mara nyingi kunapingana. Kujua na kuheshimu mahitaji yetu ya pamoja ndio siri.















