Mzio wa mbegu za kiume: Fahamu athari za maradhi haya miongoni mwa wanawake

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 5

Pranathi mwenye umri wa miaka 26 jina limebadilishwa kutoka Visakhpatnam alipata mpenzi na kufunga naye ndoa. Lakini maisha yake ya ndoa hayakwenda kama alivyotarajia. Kutoka usiku wa kwanza , muda tu baada ya kushiriki tendo la ndoa na mumewe , alianza kuhisi kuwashwa na kujikuna katika sehemu zake za siri. Hakujua la kufanya.

Nilipowaambia nyumbani walipinga kwamba kitu kama hiki ni cha kawaida kwa wanandoa wapya. Hakuna tatizo la kuwa na wasiwasi, alisema. Lakini alianza kuogopoa kushiriki tendo la ndoa hali ya kwamba aliamua kutoroka nyumba yake.

Hali ya Pranathi imegeuka na kuwa mbaya zaidi. Anasema kwamba hata mumewe hakuelewa hali yake iliyokuwa inamkabili na alikuwa akimwambia kwamba hapendi kushiriki naye tendo la ndoa.

Siku chache tu baada ya ndoa yake , alienda mjini London na mumewe. Tatizo linalomkabili limeongezeka na halijapungua.

Hata baada ya kumuona daktari mjini London, alitibiwa maradhi ya maambukizi katika njia ya mkojo. Licha ya kupokea dawa za kila aina kutibu tatizo lake , hali yake haikubadilika.

Nimefikia katika uamuzi kwamba maisha ya ndoa niyasahau, alisema.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

"Ni shida ambayo siwezi kumwambia mtu yeyote. Hata nikijadiliana na marafiki zangu, haina maana. Hakuna mtu karibu nami ambaye amewahi kupata shida kama hiyo hapo awali," alielezea.

 "Nilizungukwa na maswali mengi. Kwa upande mmoja, hofu kwamba mume ataenda kwa mtu mwingine kwa ajili ya raha ya tendo la ndoa, kwa upande mwingine, msongo wa mawazo na kimwili kutokana na matatizo ya afya," alisema.

"Badala ya kumbukumbu tamu ya maisha mapya ya ndoa, alama za uchungu pekee ndizo zimesalia kutokana na matatizo ya kiafya," alieleza.

Tatizo lilipozidi kuwa kubwa siku baada ya siku, aliondoka kwenda India ili kupata matibabu ya tatizo hili.

Madaktari walifanya vipimo vyote na kuhitimisha kwamba lazima iwe "vaginitis" au "mzio wa mbegu za kiume". Alishtuka kusikia jambo hili kwa mara ya kwanza.

Kesi kama hii imeripotiwa hivi karibuni na madaktari huko Hyderabad. Madaktari wanasema hiki ni kisa cha kwanza huko Hyderabad na kinaweza kuwa kisa cha sita nchini India.

Mzio wa mbegu za kiume ni nini?

Dk. Apparao, profesa wa biolojia katika Chuo Kikuu cha Andhra na mkuu wa zamani wa KGH Immunology, alielezea BBC kuhusu mzio wa mbegu za kiume.

"Mzio wa mbegu za kiume au hypersensitivity ya semeni ya binadamu ni protini iliyopo kwenye mbegu za wanaume. Ni mzio unaotokea wakati uke unapoguswa. Inaweza kuitwa antibody, mmenyuko wa antijeni. Hufanyika sana kwa wanawake," alisema.

.

Chanzo cha picha, Thinkstock

Je dalili zake ni zipi?

.

Chanzo cha picha, Thinkstock

Watu wenye mzio huu wana dalili fulani kwenye njia ya uke.

Uwekundu, uvimbe, maumivu, kuwasha, kuungua kwa ngozi karibu na uke wakati wa kujamiiana. Dalili hizi huanza kuonekana ndani ya dakika 10-30 baada ya tendo hilo.

Katika kesi iliyoripotiwa huko Hyderabad, inajulikana kuwa athari mbaya huonekana ndani ya dakika 30 hadi saa 6 baada ya kujamiiana.

Dalili hizi sio tu kwa eneo la uke Dk. Apparao alieleza kwamba ikiwa mbegu zitaanguka kwenye sehemu yoyote kama mikono, mdomo, kifua, kuna uwezekano wa mzio.

Watu wengine wanaweza pia kupata shida nyingine kama homa na kupiga chafya.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Kwa wale walioathirika pakubwa na mzio huu…

Inasemekana kuna hatari ya kupata matatizo kama vile kupumua kwa shida, kikohozi, uvimbe wa ulimi na koo, kupungua kwa mapigo ya moyo, kizunguzungu, kichefuchefu, kutapika na kuhara.

Unajuaje kuna tatizo?

Mzio wa mbegu za kiume hujulikana tu wakati wa kufanya tendo la ndoa na wenzi kwa mara ya kwanza. Lakini, madaktari wanasema, watu wengi wanafikiri ni maambukizi ya mkojo au vaginitis.

Je, mzio wa mbegu za kiume hutegemea mtu ?

Mwanamke ambaye ana mzio na mumewe anaweza asipate mzio anapojamiiana na mwanaume mwingine. Wakati kama huo, historia ya afya ya mume inapaswa pia kuchunguzwa na matibabu sahihi kufanyika," Apparao alisema.

Kwa ujumla, matatizo kama hayo hutibiwa kama vaginitis.

Kulingana na Kliniki ya Mayo, vaginitis pia husababisha kuvimba kwa uke, kuwasha, kuungua, na kutokwa na maji. Tatizo hili hutokea kutokana na maambukizi katika uke.

Lakini, mzio huu hutokana na tendo la kujamiiana. Ili kujua kama kuna mzio , mbegu huwekwa kwenye mwili wa mwenzi na kupimwa kama mzio.

Mzio wa mbegu za kiume sio ugonjwa wa zinaa.

Je, ni matibabu gani yanayotumika kutibu mzio wa mbegu za kiume?

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mipira ya Kiume

Dk. Apparao alisema iwapo mzio wa mbegu za kiume ni wa kiwango cha juu, suluhisho la haraka ni kutumia kondomu.

Alipendekeza kutumia dawa aina ya antihistamine kabla ya kushiriki tendo hilo. Hata hivyo, inasemekana kwamba inapaswa kutumika kulingana na ushauri wa daktari baada ya uchunguzi wa matibabu.

Tatizo la mzio linapaswa kutambuliwa katika ngazi ya msingi na kushauriana na daktari, alisema. Inashauriwa kufanyiwa uchunguzi wa mzio na kushauriana na wataalamu husika au wataalamu wa chanjo.

Dk Apparao alieleza kuwa kiwango cha mzio hakifanani kwa kila mtu na pia inategemea mfumo wa kinga ya mtu.

"Watu wenye tatizo hili wanapaswa kushauriana na daktari wa magonjwa ya wanawake au daktari wa mzio wakati wa kupanga kupata watoto. Au ni bora kuchukua ushauri wa wataalamu wa uzazi kwa njia mbadala," alipendekeza Apparao.

Maelezo zaidi:

Imetafsiriwa na Seif Abdalla