Kwa nini Singapore ndio nchi pekee duniani inayouza nyama iliyokuuzwa kwenye maabara
Na Nick Marsh
Mwandishi wa Biashara ,Asia

Inaonekana kama kuku, ina harufu ya kuku na, na pia ina ladha ya kuku.
Huwezi kamwe kukisia kwamba kipande cha nyama kilicho mbele yangu hakikutoka shambani. Ilitengenezwa katika maabara kwenye eneo la viwanda maili chache tu kutoka hapa nilipo.
Niko katika mkahawa wa Huber's Butchery and Bistro nchini Singapore, ambao ndio mkahawa pekee duniani ambao una kile kinachoitwa nyama ya kukuuzwa kwenye maabara katika menu yao.
Maoni kutoka kwa wateja yamekuwa "ya kushangaza", kulingana na mmiliki wa mkahawa huo.
Mtayarishaji wa nyama - Eat Just ya California - anasema ni ya kimaadili, safi na ya kijani - bila kuathiri au kupunguza ladha. Mabilioni ya dola yanamiminwa kwenye tasnia hii, lakini alama za maswali kubwa hutegemea uwezekano wake kama kitu chochote zaidi ya jambo jipya.
Tangu burger ya kwanza iliyokuzwa katika maabara - ambayo iligharimu $330,000 tu (£263,400) kuunda - ilizinduliwa London mnamo 2013, kampuni kadhaa ulimwenguni zimejiunga na harakati za kuleta nyama ya bei nafuu sokoni.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Kufikia sasa, ni kampuni ya Eat Just pekee ambayo imeweza kuidhinisha bidhaa yake kuuzwa kwa umma baada ya wasimamizi nchini Singapore - nchi pekee duniani kuruhusu nyama iliyokuuzwa kwenye maabara kuuzwa- kuwapa kuku wake mwanga wa kijani mnamo Desemba 2020.
Lakini mambo yanaonekana kukwama tangu wakati huo. Vipande vya kuku zilizokuzwa zilijumuishwa kwa muda mfupi kwenye kilabu cha wanachama wa kibinafsi mnamo 2021.
Ushirikiano huo ulikomeshwa baada ya miezi michache na mwaka huu Huber's imeanza kutoa sandwich ya kuku na sahani ya pasta ya kuku kwa umma - ingawa mara moja tu kwa wiki na nafasi ndogo za kulia zinapatikana.
"Nyama ya kukuuzwa kwenye maabara ni nyama halisi, lakini sio lazima kuchinja mnyama," anasema Josh Tetrick, afisa mkuu mtendaji wa Eat Just, ambaye alizungumza na BBC kutoka San Francisco. "Njia hii ya kula ina maana kwa siku zijazo," anasema.
Tofauti na vibadala vya mimea, nyama inayokuuzwa kwenye maabara ni nyama halisi. Mchakato huo unahusisha kutoa seli kutoka kwa mnyama, ambazo hulishwa na virutubisho kama vile protini, sukari na mafuta.
Seli hizo zinaruhusiwa kugawanyika na kukua, kabla ya kuwekwa kwenye chembechembe kubwa ya kibaolojia ya chuma, ambayo hufanya kama tangi ya kuchachusha.
Baada ya wiki nne hadi sita, nyenzo 'huvunwa' kutoka kwa kinu cha kibaolojia. Protini fulani ya mboga huongezwa, kisha hutengenezwa, kupikwa na kuchapishwa kwa 3-D ili kuipa sura na ulaini unaohitajika .
Vipande vilivyotokana vya kuku wa kukaanga kwenye sahani yangu ya pasta hakika vilionja kama nyama halisi ya kuku , ikiwa umechakatwa kidogo. Labda aina ya kuku unayoweza kula katika mgahawa wa chakula cha haraka.
"Ni nyama - ni kamilifu!" Anasema Caterina, mwanafunzi wa Kiitaliano aliyekuja hapa hasa kujaribu kuku wa kukuuzwa kwenye maabara. Kwa kawaida, kwa sababu za kudumu, asingekula nyama lakini Caterina anasema angekula hii.
Shida yake pekee? Kuila kuku na pasta, ambayo kwa kawaida haifanyiki nchini Italia.
Mteja mwingine kutoka Singapore anasema alishangazwa na jinsi ilivyofanana na nyama halisi.
"Ni halali", anasema. "Nisingejua ilitoka wapi. Wasiwasi wangu pekee ungekuwa gharama."
Sahani ya tambi ya kuku niliyoagiza ilikuwa S$18.50 ($13.70; £11), lakini hiyo imepunguzwa sana ikilinganishwa na gharama ya sasa ya kuzalisha nyama hiyo.
Eat Just haitasema ni kiasi gani hasa inachotumia kutengeneza kuku wake wa kukuuzwa kwenye maabara, lakini kwa sasa uwezo wa uzalishaji wa kampuni hiyo unatoa tu 2kg (4.4lb) au 3kg kwa wiki nchini Singapore.
Unapolinganisha hilo na kilo 4,000 - 5,000 za kuku wa kawaida inayouzwa kila wiki - huko Huber pekee - inakupa hisia ya ukubwa wa kazi iliyo mbele yako. Kwa ufupi, watahitaji kuongeza uzalishaji kwa kiasi kikubwa ili kuepuka kupata hasara kwa kila kipande cha kuku.
Eat Just inasema tayari imepata punguzo la 90% la gharama tangu 2018 na kampuni hiyo ilinipa ziara ya kituo chake kipya cha uzalishaji cha mamilioni ya dola nchini Singapore, ambacho inatumai kitafunguliwa mwaka ujao.
Jozi ya chuma kinachong'aa cha galoni 1,320 (lita 6,000) kwa hakika inawakilisha ishara ya dhamira, lakini kwa kweli ni sehemu ndogo ya mamilioni ya tani za kuku ambazo zingehitajika kuzalishwa ili kuendana na bei ya kuku aliyechinjwa.

Sekta hiyo inahimiza uvumilivu, lakini wanasayansi wengi tayari wameona vya kutosha.
"Masimulizi yaliyowasilishwa na makampuni haya ni ya nguvu sana", anasema Ricardo San Martin, mkurugenzi mwenza wa Alt: Meat Lab katika Chuo Kikuu cha California, Berkeley.
"Lakini simulizi hilo lazima lilinganishwe na sayansi," anasema. "Pitia takwimu, angalia kila karatasi ya kisayansi iliyoandikwa na watu ambao hawana maslahi kwenye hili na utaona jibu liko wazi."
"Je, unaweza kufanya hili, kwa kiwango, kwa gharama nzuri? Hapana. Je, unaweza kuzungumza juu ya kuokoa ulimwengu na hili? Tena, hapana. Makampuni haya yanapaswa kuwa na uaminifu.
Sio tu kwamba kuna mashaka juu ya kuongeza uzalishaji, pia kuna kutokuwa na uhakika juu ya sifa za kijani za tasnia hii, ambazo zimetiliwa shaka na wanasayansi.
Kinadharia, kupunguza utegemezi wa dunia wa ardhi na mifugo kwa ajili ya uzalishaji wa nyama kunafaa kupunguza utoaji wa kaboni, lakini kwa sasa teknolojia ya hali ya juu inayohitajika kuunda nyama ya kukuuzwa ina nguvu nyingi sana hivi kwamba inaghairi faida yoyote.
Utafiti mmoja wa Chuo Kikuu cha California, Davis hata ulikadiria kuwa mchakato huo hutoa kati ya mara 4 na 25 zaidi ya kaboni dioksidi kuliko nyama ya kawaida ya ng'ombe. Hata hivyo, East Just imeuita utafiti huo "una dosari".
Alipoulizwa na BBC kama mradi mzima unaweza kuishia bila mafanikio, Josh Tetrick kutoka Eat Just alijibu: "Kwa hakika".
Lakini bado hajakata tamaa: "Kutengeneza nyama kwa njia hii ni muhimu na hakuna uhakika," anasema.
"Sio moja kwa moja. Ni vigumu. Haina dhamana na inaweza isifanyike. Lakini chaguo lingine kwetu ni kutofanya chochote. Kwa hivyo tuliamua kuchukua dau na kuichukua hatua hii."
Wawekezaji wengi wameamua kufanya dau kama hilo. Kufikia mwaka huu, inakadiriwa $2.8bn imetumika katika kuendeleza nyama ya kilimocha aina hii.

Chanzo cha picha, Just Eat
Hata hivyo, ikiwa nyama iliyokuuzwa kwenye maabara itakuwa kitu chochote zaidi ya kuwa mbadala kwa watu walio na uwezo katika ulimwengu ulioendelea, basi kutegemea uwekezaji kutoka kwa biashara za kibinafsi kunaweza kuwa haitoshi.
Serikali, Bw Tetrick anasema, zitahitaji kuweka "fedha nyingi za umma" katika nyama ya kukuuzwa kwa njia hii ili kushindana na nyama iliyochinjwa kwa kawaida.
"Hii ni kama mpito kwa nishati mbadala... Ni mradi wa maisha - labda mradi wa maisha mengi," anasema.
Kwa sasa ingawa hakuna nchi nje ya Singapore iliyoidhinisha uuzaji wa nyama ya kukuuzwa kwenye maabara , kando na kujitolea kwa uwekezaji mkubwa.
Kulingana na Ricardo San Martin kutoka UC Berkeley, ufadhili wa kibinafsi na wa umma kwa makampuni ya nyama ya kilimo utakauka ikiwa "hawataangalia kioo" hivi karibuni na kuwasilisha utabiri wa kweli kwa wawekezaji.
"Isipokuwa kuna njia wazi ya mafanikio wakati fulani katika siku zijazo, wawekezaji na serikali hawatataka kutumia pesa kwa kitu ambacho hakijathibitishwa kisayansi".












