Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 01.08.2024

Chanzo cha picha, Getty Images
Joe Gomez bado anataka kuondoka Liverpool, Marseille wana bei ambayo wako tayari kulipa kumpata Eddie Nketiah, Palace wako tayari kumruhusu Jordan Ayew kuondoka.
Beki wa Liverpool na England Joe Gomez, 27, yuko tayari kuondoka msimu huu wa joto baada ya uhamisho wa kwenda Newcastle kugonga mwamba mwezi uliopita. (Mail)
Marseille wako tayari kulipa takriban euro milioni 17 kumpata mshambuliaji wa Arsenal Muingereza Eddie Nketiah, 25, huku mazungumzo yakitarajiwa kuendelea kati ya klabu hizo siku zijazo. (Telegraph)
Crystal Palace wameonyesha nia ya kumruhusu mshambuliaji Jordan Ayew mwenye umri wa miaka 32 kuondoka msimu huu wa joto, huku Leicester wakipania kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Ghana. (Standard)

Chanzo cha picha, Getty Images
Everton wanavutiwa na mshambuliaji wa Paraguay Ramon Sosa, 24, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Nottingham Forest katika jitihada zao za kumsajili kutoka CA Talleres. (Team talk)
Chelsea huenda wakalazimika kupunguza bei yao ikiwa wanataka kukubaliana na Atletico Madrid kuhusu mauzo ya kiungo wa kati wa Uingereza Conor Gallagher. Klabu hizo zimetofautiana kwa £20m katika tathmini zao. (Mail)
Leeds wametoa ofa ya pauni milioni 2.5 kwa winga wa Fenerbahce Muingereza Ryan Kent, 27. Jose Mourinho ana nia ya kumsajili mchezaji huyo wa zamani wa Rangers. (Haber Ekspres - kwa Kituruki)
Paris St-Germain wamekubali kumsajili kiungo wa kati wa Benfica na Ureno Joao Neves, 19, kwa euro nilioni 60, pamoja na nyongeza ya euro milioni 10, huku kiungo wa kati wa Ureno Renato Sanches, 26, akihamia njia upande mwingine kwa mkopo. (Fabrizio Romano)
Nottingham Forest inatazamiwa kumsajili winga wa Ureno mwenye umri wa miaka 24 Jota Silva kutoka Vitoria Guimaraes kwa euro milioni saba, katika mkataba ambao pia unajumuisha nyongeza ya hadi euro milioni tano. (Sky Sports)

Chanzo cha picha, Getty Images
Wolves na Fulham wamejiunga na kinyang'anyiro cha kumsajili beki wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 21 Isaak Toure kutoka Lorient. (Football Insider)
Fulham wamekubali dili la kumsaini beki wa Uhispania Jorge Cuenca, 24, kutoka Villarreal. (Fabrizio Romano)
Coventry City wamejizatiti katika mpango wa Hull City wa pauni milioni 2.5 kumsaini mshambuliaji wa Ghana Brandon Thomas-Asante, 25, kutoka West Brom. (Telegraph)
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi na kuhaririwa na Yusuf Jumah












