Calafiori: Mfahamu mchezaji mpya wa Arsenal

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Riccardo Calafiori, ambaye alianza uchezaji wake Roma, ameichezea nchi yake mechi tano
Muda wa kusoma: Dakika 5

Wakati klabu ya Bologna ilipotangaza kuwasili kwa Riccardo Calafiori kutoka FC Basel mwishoni mwa Agosti mwaka jana, saa chache tu kabla ya kumalizika kwa dirisha la uhamiaji la wachezaji soko wachache sana walikisia jinsi hatua hiyo ingefanikiwa.

Kufuatia kuwasili kwa Jose Mourinho huko Roma mwaka 2021, jiji la nyumbani la Calafiori na klabu aliyokulia, nafasi na wakati wa kucheza vilikuwa adimu kwa beki huyo.

Hilo lilimtia moyo kukubali uhamisho wa kudumu kwenda kwa wababe wa Uswizi Basel katika msimu wa 2022.

Licha ya kuwa mara kwa mara katika timu za vijana za Italia, Calafiori alianza kuteleza kutoka kwenye rada ya soka ya Ulaya kabla ya mkurugenzi wa kiufundi wa Bologna Giovanni Sartori alipomnyatia.

Ilimchukua miezi 11 kabla msimu wa kwanza kamili wa Calafiori katika ligi ya Serie A kulimalizika kwa kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa, kabla ya kuthibitishwa kuwa mchezaji bora wa Italia kwenye Euro 2024 na thamani yake sokoni kuongezeka mara 12.

Sio wachezaji wengi kote barani Ulaya wanaweza kudai ongezeko kama hilo ndani ya kipindi kifupi kama hicho - na imemfanya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 kuhamia Arsenal kwa ada ya hadi £42m ikiwa ni pamoja na nyongeza.

Pia unaweza kusoma

Je, Calafiori ni nani?

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Riccardo Calafiori alikuwa sehemu ya timu ya Bologna iliyofuzu kwa Ligi ya Mabingwa msimu uliopita

Calafiori amekuwa akizingatiwa kuwa mchezaji mwenye talanta.

Roma ilipomuuza kwa euro 2.5m kwa Basel miaka miwili iliyopita, walijumuisha kifungu cha 40% cha mauzo katika mkataba wake.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kifungu cha 50% cha mauzo kilijumuishwa pia na Uswizi alipohamia Bologna kwa euro 4m mwaka mmoja baadaye.

Akiwa ameshinda jeraha baya la kano ya goti alipokuwa na umri wa miaka 16, na kukosa takriban mwaka mzima, Calafiori nyuko imara kiumbo na ana urefu wa 188cm.

Ni mchezaji mwenye nguvu ambaye anachukua fursa ya hatua zake ndefu uwanjani lakini pia ni mzuri na mwenye kipawa cha kiufundi.

Ana nguvu angani na katika hali ya mtu mmoja-kwa mmoja, anageuka kuwa kiungo katika umiliki wa mpira, akipanda mita chache ndani ya uwanja na kusaidia kuwa kiungo mchezeshaji.

Anaona fursa zilizo wazi mbele yake na anajua jinsi ya kuziingia, kama vile pasi zake tano za mabao msimu uliopita zilivyothibitisha.

Akiwa na kipawa cha mguu wa kushoto, unaomwezesha kupiga pasi ndefu na za masafa mafupi, akiwa Bologna mara nyingi alivuka uwanja akitafuta winga wa kulia au kupiga pasi katikati ya uwanja ili kuwazidi wapinzani.

Calafiori ni mchezaji mahiri ambaye alikua kama beki wa pembeni wa kushoto.

Kocha wa zamani wa Bologna Thiago Motta mara moja alimweka katika nafasi ya kati zaidi ambapo angeweza kutumia muda wake mzuri, kuzuia mipira, kuwakabili wapinzani na kuanza kuanzisha mchezo kutoka nyuma.

"Tangu siku ya kwanza alipojiunga na Bologna, Thiago Motta aliniambia angetumia uwezo wangu wote kama beki wa kati," Calafiori alisema Mei mwaka jana wakati wa mahojiano.

Je, Calafiori atailetea nini Arsenal?

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Calafiori kushoto

Bologna ilimaliza msimu huo kwa kushindwa mara sita pekee, ikiwa na safu ya tatu bora ya ulinzi katika Seria A nyuma ya Inter na Juventus - na sifa nyingi zinakwenda kwa Calafiori.

Muitaliano huyo sasa atalazimika kutafuta nafasi yake kwenye safu ya ulinzi ya Arsenal ambayo imekuwa safu ya ulinzi isiyoweza kupenyeka katika kampeni za mwisho za Ligi Kuu, ikiruhusu mabao 29 pekee.

Akilinganishwa na William Saliba, Gabriel Magalhaes na Ben White, Calafiori ana sifa tofauti.

Mchezo wake hufanya kazi kvizuri timu inaposhambulia lakini pia akisubiri fursa ya kufungua mchezo. Atawapa Gunners chaguo jingine la kuaminika wakati wanapoanzisha mchezo kutoka nyuma.

Anaweza kucheza upande wa kushoto au kama beki wa kati wa kushoto katika safu ya ulinzi ya watu wanne na pia safu ya nyuma ya watu watatu kama alivyofanya kwenye Euro 2024.

Calafiori amekuwa na msimu mmoja pekee katika kiwango cha juu zaidi cha soka, ambapo alianzishwa mara 26 katika ligi kuu akiichezea Rossoblu ambao walimaliza wa tano msimu uliopita.

Hatahivyo, hiyo ilitosha kumshawishi bosi wa Italia, Luciano Spalletti kumuanzisha katika mecho zote za Azzurri , ambapo alionesha umahiri wake na kuvutia klabu kubwa za Ulaya .

Kwa usaidizi wa Motta, Calafiori alifaulu bila tatizo hatua ya kuhamia kutoka Basel hadi Bologna.

Mikel Arteta atalazimika kumsaidia kufanya vivyo hivyo ikiwa anataka kupata ubora zaidi kutoka kwake London.

Ni hatua kubwa aliopiga na Muitaliano huyo atahitaji muda kuzoea. Kandanda ya Ligi Kuu ya Uingereza ina kasi zaidi kuliko Serie A, wachezaji wana muda mchache wa kufanya maamuzi na kucheza idadi kubwa ya mechi zinazohitaji sana a nguvu kimwili.

Hata hivyo, Calafiori ana kila kitu kinachohitajika ili kufanikiwa: ujuzi mzuri wa kiufundi, maarifa, nguvu za kimwili, ujuzi wa mbinu na unyenyekevu.

Atafaidika na mtindo wa uchezaji wa timu yake mpya – wanaocheza kama ya Bologna.

Kwa kiwango cha juu juu zaidi, taswira yake kwenye Euro ilifanana sana na ile ya watangulizi wengi mashuhuri wa Azzurri kama Paolo Maldini, Fabio Cannavaro na Alessandro Nesta, na hii haikuonekana bila kutambuliwa na wale wanaopenda urembo.

Na ikiwa taaluma ya Calafiori itakua sawa na watangulizi hao, waumini wa Gunners wanaweza kujigamba kwa miaka michache ijayo.

Pia unaweza kusoma

Imetafsiriwa na kuchapishwa na Seif Abdalla