Kwa nini Messi ni kiongozi wa kweli wa Argentina?

Pablo Zabaleta, Mchambuzi

messi

Chanzo cha picha, Getty Images

Nyote mmeona mvutano na wasiwasi tuliopata wakati wa mchezo wetu (Argentina)dhidi ya Mexico hadi tukafunga bao, na pia ahueni baada ya kipyenga cha mwisho baada ya ushindi wetu wa 2-0. 

Kulikuwa na shinikizo kubwa kwetu baada ya kufungwa na Saudi Arabia na ahueni hiyo ilikuwa kwa kila mtu - kwa timu nzima na mashabiki wetu wote hapa, lakini haswa kwa Messi. 

Ungekuwa mwisho mbaya na mchungu kuona Argentina ikitolewa katika hatua ya makundi katika Kombe la dunia ambalo pengine linaweza kuwa la mwisho kwa Messi. 

Bado hatuko katika hatua ya 16 bora. Inabidi tushinde tena - wakati huu dhidi ya Poland - ili kuhakikisha kuwa tunavuka. 

Haitakuwa rahisi, na timu bado inahitaji kuimarika zaidi, lakini tuna matumaini na imani baada ya kuifunga Mexico. 

Tunae Messi, bila shaka. Tumemtegemea mara nyingi sana huko nyuma, na tunajua tunaweza kumtegemea tena Qatar.

Itakuwa ngumu kwetu kufika mbali katika mashindano haya, tunalijua hilo. Lakini angalau tunaweza kuota kuhusu timu hii ya Argentina tena - na hiyo ni kwa sababu yake. 

Najua Kombe la Dunia lina maana gani kwa Messi'

messi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mbali na kushinda pamoja kombe la dunia kwa vijana chini ya miaka 20, Zabaleta na Messi walishinda pia pamoja medali ya dhahabu ya Olimpiki wakiwa na Argentina huko Beijing mwaka 2008
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Nimeshuhudia safari ya mwanzo Messi na Argentina na ninatumai sana kwamba anaweza kuimaliza kwa kuibeba Kombe hili la Dunia.

Tangu mara ya kwanza nilipomuona akigusa mpira kwenye mazoezi ya kwanza tuliyofanya pamoja kwa timu ya vijana chini ya miaka 20, nilijua atakuwa mchezaji wa kipekee sana.

Bila shaka, tuliwahi kusikia kuhusu Messi akiwa Barcelona kabla ya kukutana naye, lakini hiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kuichezea Argentina. Hakusema mengi wakati huo, lakini tulimkaribisha kwa uchangamfu katika timu na haraka tukagundua jinsi alivyokuwa mzuri.

Alikuwa nasi kwenye Kombe la Dunia la Vijana chini ya umri wa miaka 20 mwaka wa 2005 nchini Uholanzi alipokuwa na umri wa miaka 17.

Nilikuwa nahodha wa Argentina na tulishinda mashindano yale pamoja – ukweli tulishinda, lakini, ilikuwa zaidi jitihada zake!

Najisikia mwenye bahati sana kuwa sehemu ya kizazi chake; kufurahia kutazama na kucheza pamoja naye na kushiriki nyakati nyingi nzuri na yeye, kama mchezaji mwenzangu wa timu ya taifa na kama rafiki.

Najua namna alivyojitolea na nyakati ngumu ambazo amepitia. Usisahau, alikuwa na umri wa miaka 13 tu alipohamia Uhispania.

Messi lazima ashinde Kombe la Dunia

Messi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Argentina celebrate after winning the 2021 Copa America. It was Messi's first senior international tournament victory, at the age of 34.

Huko nyumbani kuna mapenzi mengi kwa Messi, lakini si mara zote imekuwa hivi. Baada ya kupoteza fainali ya Kombe la Dunia 2014, tulipoteza fainali zingine mbili - Copa America mnamo 2015 na 2016.

Huko Argentina hiyo haitoshi. Kwa baadhi ya watu na kwa sehemu za vyombo vyetu vya habari, kufika fainali tu hakukubaliki. Kulikuwa na ukosoaji mwingi dhidi ya Messi kwa sababu hatukuwa tumeshinda kila kitu kama alivyokuwa akifanya akiwa na Barcelona wakati huo.

Alikata tamaa baada ya hapo na kuchukua mapumziko ya kuichezea timu ya taifa ili kujiongezea nguvu, lakini aligundua haraka namna ilivyokuwa muhimu kwake kuwa sehemu ya timu ya taifa.

Messi ameshinda kila kitu katika soka la ngazi ya klabu, lakini alikuwa na hamu ya kurudi na kutusaidia kushinda kitu pia Argentina. Kwa hivyo ilikuwa jambo kubwa na kufurahisha kumuona akishinda taji lake kuubwa la kwanza katika kiwango cha kimataifa, kwenye Copa America mwaka jana.

Tulishinda kwa kuifunga Brazil katika uwanja wa Maracana, ambayo ilikuwa kitu cha pekee sana, na nilipenda jinsi kila mtu alimkimbilia Messi kwenye filimbi ya mwisho ili kumkumbatia.

Ushindi huo uliondoa presha kidogo kwake, na kuwazuia watu kumsema kwamba hakujitoa kwa ajili yetu kama alivyoichezea klabu yake (Barcelona) - lakini bado watu wanatarajia mengi kutoka kwake kwenye Kombe la Dunia. Kushinda kombe la dunia.

Nini kimebadilika? Messi amekomaa

Messi

Chanzo cha picha, Getty Images

Katika Kombe la Dunia la 2018, nilikuwa mchambuzi wa BBC nchini Urusi na, hata kwa mbali, niliweza kumuona Messi akionekana kuwa na msongo wa mawazo, jambo ambalo lilikuwa la wasiwasi sana. Kikosi hakikuwa mahali pazuri na tulitolewa mapema.

Ilikuwa tofauti kabisa mnamo 2014 nilipokuwa naye katika kikosi cha Argentina kilichofika fainali huko Brazil. Alikuwa akiongoza timu, na alikuwa akiipenda.

Kabla ya michuano ya mwaka huu kuanza, nilimsikia Leo akisema kuna mfanano kati ya hisia alizokuwa nazo wakati huo na mazingira ya kikosi kwa sasa. Hiyo ni ishara nzuri sana kwa sababu inamaanisha kuna umoja na pia kwamba anafurahi.

Wakati Messi anazungumza, kila mtu anasikiliza. Ilikuwa vivyo hivyo mnamo mwaka 2014 - lakini kila wakati alikuwa kimya na hakusema mengi wakati huo.

Alikuwa nahodha wetu lakini Javier Mascherano alichukua nafasi hiyo badala yake, kwa sababu ya uzoefu wake na tabia yake. Yeye ndiye aliyekuwa akiongea sana kwenye chumba cha kubadilishia nguo, akitutayarisha kabla ya michezo.

Sasa, ni Messi mwenyewe anayefanya hivyo.

Sio tu mchezaji wetu bora, ni kiongozi wa kweli wa timu - hata meneja Lionel Scaloni amesema hivyo mara nyingi - na atakuwa akiwasaidia katika mwanzo huu mgumu kwa njia hiyo pia, sio tu kwa kufunga mabao na uongozi pia.

Ni jambo zuri. Imekuwa safari ndefu kwake hadi wakati huu. Bila shaka, kila mtu anaweza kubadilika nje ya uwanja na kujifunza mambo tofauti. Messi sasa, mwenye umri wa miaka 35, amekomaa zaidi, ana uzoefu zaidi na ni mtu wa familia - lakini bado ni mwanasoka wa ajabu pia.

Ikiwa atashinda Kombe hili la Dunia basi astaafu mara moja kwa sababu atakuwa amepata kila linalowezekana. Hakutakuwa na chochote kitakachobaki kwake kushinda.

Pablo Zabaleta alikuwa akizungumza na Chris Bevan huko Doha, Qatar