Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 21.06.2024

Chanzo cha picha, Getty Images
Liverpool wanavutiwa na Arda Guler, Fulham warudi mezani kwa Trevoh Chalobah, Manchester United wako tayari kumaliza harakati zao za kumnasa Jarrad Branthwaite.
Liverpool wanamfuatilia kiungo mshambuliaji wa Uturuki mwenye umri wa miaka 19 Arda Guler kutoka Real Madrid (Teamtalk)
Fulham wamefufua nia yao ya kumnunua beki wa Chelsea , 24, Muingereza Trevoh Chalobah. (Standard),
Manchester United itaachana na mazungumzo na Everton kwa ajili ya kumnunua mlinzi wa Uingereza Jarrad Branthwaite, 21,endapo The Toffees hawatapunguza bei yao ya £70m (ESPN)
Everton wanazidi kujiamini kusalia na beki huyo wa kati msimu huu. (I Sport)

Chanzo cha picha, Getty Images
Beki wa Lille Leny Yoro, 18, anapendelea kuhamia Real Madrid badala ya Liverpool au Manchester United . (Marca kwa Kihispania)
West Ham wanahofia winga wa Ghana Mohammed Kudus, 23, ataomba kuondoka katika klabu hiyo msimu huu wa joto. (Football Insider)
Aston Villa wameuliza kuhusuuwezekano wa kumsajili kwa kiungo wa kati wa Argentina Matias Soule, 21, lakini Juventus wanasema hauzwi. (Sky Sports)
Chelsea wako kwenye mazungumzo na Boca Juniors kuhusu dili la kumnunua beki wa Argentina mwenye umri wa miaka 19 Aaron Anselmino. (Athletic-Usajili unahitajika)
Manchester United wanajiandaa kutumia kipengele cha kuachiliwa kwa pauni milioni 33.8 katika kandarasi ya mshambuliaji wa Bologna Mholanzi Joshua Zirkzee, 23. (Telegraph - usajili unahitajika)

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo wa kati wa Paris St-Germain na Uholanzi Xavi Simons, 21, ndiye anayelengwa na Bayern Munich . (Bild - kwa Kijerumani)
Kocha wa zamani wa AC Milan Stefano Pioli ni miongoni mwa wanaowania kuwa meneja wa Al-Ittihad . (Fabrizio Romano)
Arsenal wamewasilisha ombi la kumnunua beki wa pembeni wa Fenerbahce Ferdi Kadioglu, 24. (Ajan Spor - kwa Kituruki)
Southampton na Brighton wametoa ofa kwa IFK Gothenburg kumnunua kiungo wa kati wa Mali, 18, Malick Yalcouye. (Caught offside)
Imetafsiriwa na Yusuf Jumah












