Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 20.06.2024

TH

Chanzo cha picha, Getty Images

Lazio ni miongoni mwa vilabu vya Italia vinavyomtaka Mason Greenwood, Arsenal wanaweza kutoa ofa ya kumtoa mchezaji pamoja na pesa ili kumsajili Bruno Guimaraes na Liverpool wajiunga na na kinyang'anyiro cha kumnunua Michael Olise.

Lazio wameanza mazungumzo na Manchester United kuhusu uhamisho wa pauni milioni 30 kumnunua mshambuliaji wa zamani wa Uingereza Mason Greenwood, 22. (Mail).

Juventus na Napoli pia wanapambana katika harakati za kumsajili Greenwood. (Independent)

Arsenal wanaweza kutafuta ofa ya kumtoa mchezaji pamoja na pesa ili kumnunua kiungo wa kati wa Newcastle na Brazil Bruno Guimaraes, 26. (Football Transfers)

TH

Chanzo cha picha, Getty Images

Unaweza Pia Kusoma

Liverpool inalenga kuzishinda Chelsea na Manchester United katika kumsajili winga Mfaransa Michael Olise, 22, kutoka Crystal Palace . (Football Transfers)

Tottenham wamewatangulia Aston Villa katika harakati za kumsajili kiungo wa kati wa Marekani Weston McKennie, 25, kutoka Juventus . (Football Insider)

Winga wa Athletic Bilbao wa Uhispania Nico Williams, 21, anaendelea kushikilia uwezekano wa kuhamia Barcelona , ​​licha ya kuwa na mazungumzo na Villa , Arsenal , Liverpool na Newcastle United . (HITC)

Matty Cash wa Villa tayari anafuatiliwa na AC Milan lakini sasa wapinzani wao Inter Milan wanamfikiria beki huyo wa kulia wa Poland, 26, kama anayeweza kuziba nafasi ya mlinzi wa Uholanzi Denzel Dumfries, 28. (Sky Sport Italia - kwa Kiitaliano).

Kiungo wa kati wa England Keira Walsh, 27, anakaribia kuhama kutoka kwa mabingwa wa Ulaya Barcelona kwenda Arsenal . (90min)

Chelsea wanavutiwa na mshambuliaji wa Atletico Madrid Mhispania Samu Omorodion na mshambuliaji wa Aston Villa wa Colombia Jhon Duran, lakini watamsajili mmoja tu wa wachezaji hao wenye umri wa miaka 20. (Fabrizio Romano)

Manchester United inaongeza kasi ya kutafuta wachezaji wa kumairisha kikosi cha huku mshambuliaji wa Lille raia wa Kanada Jonathan David, 24, akilengwa.(inews)

TH

Chanzo cha picha, Getty Images

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Manchester United haitaongeza mkataba na Bruno Fernandes kama jambo la kipau mbele msimu huu licha ya kiungo huyo wa kati wa Ureno, 29, kuhusishwa na Bayern Munich na Inter Milan . (Manchester Evening News)

Mazungumzo yalikuwa katika hatua za juu kuhusu uhamisho wa mlinzi wa Ufaransa Jean-Clair Todibo, 24, kutoka Nice hadi Manchester United lakini mkataba huo haujakamilika kwa sababu ya sheria za Uefa kuhusu umiliki wa vilabu vingi. (Fabrizio Romano)

Kiungo wa kati wa Morocco Sofyan Amrabat, 27, ameiambia Fiorentina kuwa hataki kurejea katika klabu hiyo baada ya kukaa kwa mkopo Manchester United msimu uliopita . (Athletic-Usajili unahitajika)

West Ham wanakabiliwa na vita vya kusalia na Mohammed Kudus huku klabu ya Saudi Arabia ya Al-Ittihad ikimtaka winga huyo wa Ghana, 23. (ESPN).

Leicester City na Fulham wanamtaka Edoardo Bove wa Roma lakini wapinzani wa Premier League Everton na Bournemouth wako katika hatua ya juu zaidi katika harakati zao za kumnasa kiungo huyo wa kati wa Italia, 22. (HITC).

Southampton ndio waliokatika nafasi nzuri kumsaini Flynn Downes kwa mkataba wa kudumu baada ya kuwa na kiungo huyo wa England , 25, kwa mkopo kutoka West Ham msimu uliopita.(GiveMeSport)

Unaweza Pia Kusoma

Imetafsiriwa na Yusuf Jumah