Euro 2024: Nyota 24 chipukizi wa kuwatazama

DC
    • Author, Chris Bevan
    • Nafasi, BBC

Ni miaka 20 tangu Wayne Rooney kutoka Uingereza, alipotangaza kipaji chake kwa ulimwengu kwenye michuano ya mataifa ya Ulaya 2004.

Nani mwingine atakuwa nyota chipukizi katika michuano ya Ulaya msimu huu wa kiangazi kati ya wachezaji wote 622?

BBC Sport na wachambuzi wa soka wanakupa orodha ya wachezaji wachanga wa kutazamwa msimu huu wa joto huko Ujerumani.

Martin Baturina - Croatia

vc

Chanzo cha picha, getty images

Maelezo ya picha, Baturina ameichezea Croatia mechi tatu hadi sasa.

Ana umri wa miaka 21. Mchezaji kiungo wa klabu ya Dinamo Zagreb na raia wa Crotia. Ni maarufu nchini kwake na amepewa jina la 'The Next Modric'!

Timu yake ni washindi wa ligi ya Crotia, na hawataweza kudumu muda mrefu zaidi baada ya Euro, kwani Juventus na Arsenal ziko zinamtaka na sio wao pekee.

Warren Zaire-Emery - Ufaransa

Ana umri wa miaka18, anacheza kiungo katika klabu ya Paris St-Germain.

Amefanya vizuri akiwa na Paris St-Germain msimu huu na kupata Tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi wa Mwaka na na mkataba mpya hadi 2029.

Benjamin Sesko - Slovenia

Umri ni miaka 21, ni mshambuliaji wa klabu RB Leipzig ya Ujerumani.

Sesko ni mshambuliaji mwenye mwenye futi 6 na inchi 5 ambaye mashabiki wa Arsenal wanamfahamu kwa sababu kumekuwa na mazungumzo kuhusu uhamisho wa pauni milioni 50 kutoka RB Leipzig.

Aliondoka Red Bull Salzburg kwa mkopo hadi Leipzig. Aliifungia Salzburg mabao 18 mwaka 2022-23.

Brian Brobbey – Uholanzi

k

Chanzo cha picha, getty images

Maelezo ya picha, Brobbey amepewa jina la utani 'Brobbeast' tangu siku zake za awali akiwa Ajax.

Ana umri wa miaka 22 ni mshambuliaji klabu ya Ajax ya Uholanzi.

Brobbey ameifunga Ajax mabao 22 katika mashindano yote. Katika kampeni ambayo wababe hao wa Uholanzi walikuwa chini kabisa za jedwali, mchango wake uliwafikisha kufika nafasi ya tano ya ligi.

Na tayari ameonja mafanikio katika ngazi ya kimataifa, akishinda mara kwa mara Mashindano ya Ulaya ya Vijana chini ya miaka 17 2018 na 2019.

Florian Wirtz - Ujerumani

Ana umri wa miaka 21, anachezea nafasi ya katika klabu ya Bayer Leverkusen ya Ujerumani.

Ni moja wa vijana wawili wa umri wa miaka 21 katika timu ya Ujerumani ambao wanajulikana sana na mashabiki wa Uingereza kutokana na ushujaa wao katika klabu.

Wirtz amekuwa mbunifu katika timu ya Leverkusen iliyotwaa ubingwa chini ya Xabi Alonso, ingawa alikosa kucheza Kombe la Dunia nchini Qatar kutokana na jeraha la goti.

Ameanza mechi saba kati ya nane tangu Julian Nagelsmann achukue usukani mwaka jana, haswa akiwa upande wa kushoto wa washambuliaji watatu.

Giorgi Mamadashvili - Georgia

c

Chanzo cha picha, getty images

Maelezo ya picha, Mamadashvili

Umri wake ni miaka 23, ni kipa wa klabu ya Valencia ya nchini Spain. Anachukuliwa na wengi kuwa kipa bora kijana katika soka la Ulaya.

Mamardashvili amekuwa chaguo la kwanza kwa nchi yake, na kacheza mechi 13 za mwisho za kimashindano ya kimataifa.

Johan Bakayoko - Ubelgiji

Ana umri wa miaka 21, ni mshambuliaji wa kulia wa timu ya PSV Eindhoven ya Uholanzi. Alihamia PSV Eindhoven akiwa na umri wa miaka 16 kutoka Anderlecht na amefanya vyema akiwa na PSV kwa kushinda taji akiwa na mabao 16 na pasi za mwisho 14.

Majira ya joto yaliyopita ilisemekana anatakiwa na Brentford na Burnley, mwaka huu ni Bayern, Arsenal na Liverpool - inaweza kuwa vigumu kwa PSV kukataa.

Georgiy Sudakov - Ukraine

Umri wake ni miaka 21, ni mchezaji kiungo wa Shakhtar Donetsk ya Ukraine.

Shakhtar Donetsk ilikataa ombi la kumnunua la Napoli mwezi Januari, lakini Sudakov anasema ni wakati wa kuiondoa familia yake kwenye vita na huenda akaenda London kwani amekuwa akihusishwa na Arsenal, Spurs na Chelsea.

Jamal Musiala - Ujerumani

dcx

Chanzo cha picha, getty images

Maelezo ya picha, Musiala amepewa jina la utani 'Bambi' kwa sababu ya uwezo wake wa ajabu wa kupiga chenga

Ana umri wa miaka 21, nafasi yake ni kiungo katika klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani.

N¬¬diye nyota mwingine mchanga wa Ujerumani. Inashangaza kwamba Musiala, ambaye alikulia London na kuiwakilisha Uingereza chini ya umri wa miaka 21, tayari yuko kwenye michuano ya tatu kwa Ujerumani.

Alianza kucheza Euro 2020 akiwa na umri wa miaka 18.

Joao Neves - Ureno

Umri wake ni miaka 19. Kiungo wa klabu ya Benfica. Hakukosa hata dakika moja ya msimu uliopita akiwa Benfica, alicheza kila sekunde katika michezo 12 ya Ulaya.

Alipata nafasi baada ya Enzo Fernandez alipoondoka Lisbon na kwenda Chelsea 2023. Benfica wanataka zaidi ya pauni milioni 80 kumuuza.

Ikiwa atafanya vizuri kwenye Euro 2024, kunaweza kuwa na foleni ya vilabu kubisha hodi kwenye mlango wa wakala Jorge Mendes.

Strahinja Pavlovic - Serbia

Umri wake ni miaka 23. Ni beki wa kati wa klabu ya Red Bull Salzburg. Pavlovic amekaa kwa misimu miwili Red Bull Salzburg baada ya kusajiliwa kutoka Monaco.

Ana uwezekano wa kuanza upande wa kushoto wa safu ya kati ya wachezaji watatu wa Serbia watakapomenyana na England Jumapili.

Leopold Querfeld - Austria

c

Chanzo cha picha, getty images

Maelezo ya picha, Querfeld, anayeonekana hapa akimkabili mshambuliaji wa Serbia, Aleksandar Mitrovic, amekuwa akihusishwa kujiunga Crystal Palace, Rangers ama Celtic.

Ana umri wa miaka 20. Ni beki wa kati wa Rapid Vienna. Kwa jina la utani 'Ukuta wa Austria.'

Querfeld amekuwa beki mzuri kwa Rapid Vienna katika misimu miwili iliyopita, na alicheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa mwezi Machi.

Arda Guler - Uturuki

Umri wake ni miaka 19. Anacheza kama kiungo katika klabu ya Real Madrid.

Alijiunga na Real kutoka Fenerbahce msimu uliopita wa joto na lakini akajeruhiwa vibaya, na hakucheza mechi yake hadi mwishoni mwa Januari.

Akiwa na mabao sita katika mechi 12 za kwanza alizochezea akiwa na Madrid. Kocha wa Uturuki Vincenzo Montella lazima ashawishike kumwanzisha kwenye michuano ya Ulaya.

Xavi Simons - Uholanzi

Umri wake ni miaka 21. Ni mshambulizi wa PSG. Alifanya vyema akiwa kwa mkopo katika klabu ya RB Leipzig kutoka PSG msimu huu.

Alikuwa mchezaji aliyechezewa vibaya zaidi katika Bundesliga msimu huu - na anapenda kuwa mtoa huduma kwa wachezaji wenzake, akimaliza nafasi ya pili kwa pasi za mwisho katika ligi kuu ya Ujerumani.

Zeno Debast - Ubelgiji

v

Chanzo cha picha, getty images

Maelezo ya picha, Debast amekuwa katika timu ya Anderlecht tangu 2010

Umri wake ni miaka 20. Ni beki wa Anderlecht/Sporting. Amekuwa Anderlecht tangu 2010, akijiunga na akademi hiyo akiwa na umri wa miaka sita, lakini alitangaza wiki hii: "Nimeamua kuichezea Sporting Club de Portugal msimu ujao."

Debast alikwenda kwenye Kombe la Dunia 2022 na kupata uzoefu wa mashindano, ingawa hakucheza sana.

Mario Mitaj - Albania

Umri wake ni miaka 20. Ni beki wa kushoto wa Lokomotiv Moscow. Baada ya mafanikio yake katika klabu ya AEK Athens, na misimu miwili yenye mafanikio sana akiwa na Lokomotiv Moscow ilifuata.

Juventus wanaripotiwa kumtaka, na anatarajiwa kuanza mchezo wa ufunguzi wa Albania dhidi ya Italia huko Dortmund.

Vladyslav Vanat - Ukraine

Umri wake ni miaka 22. Ni mshambuliaji Dynamo Kiev. Akiwa amebarikiwa na kasi na udhibiti, Vanat alicheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa dhidi ya Ujerumani Juni mwaka jana.

Alitia saini mkataba mpya wa miaka mitatu wa kusalia Kiev.

Jeremie Frimpong – Uholanzi

k

Chanzo cha picha, getty images

Maelezo ya picha, Frimpong alijiunga na Manchester City akiwa na umri wa miaka tisa na kukaa na klabu hiyo kwa miaka tisa kabla ya kujiunga na Celtic mwaka wa 2019. Alihamia Leverkusen mwaka wa 2021

Umri wake ni miaka 23. Mshambuliaji wa kulia au beki wa kulia wa Bayer Leverkusen. Amefunga mabao 14 na kutajwa katika timu bora ya Bundesliga kwa mwaka wa pili mfululizo.

Alitumiwa kama winga ya kulia na Ronald Koeman na kupata matokeo mazuri katika mechi ya kirafiki ya Uholanzi dhidi ya Canada, ambapo alifunga bao na kusaidia.

Alikuwa sehemu ya kikosi kwenye Kombe la Dunia la 2022, lakini hakushiriki.

Matej Jurasek - Jamhuri ya Czech

Umri wake ni miaka 20. Ni winga wa Slavia Prague. Kwa muda wa angalau miaka amekuwa akitajwa kuwa mchezaji bora zaidi kutoka Jamhuri ya Czech na bado anaweza kujumuishwa kwenye orodha hii.

Ni mchezaji mzuri kila upande, anaweza kutatizika kupata nafasi ya kuanzia kwenye Euro kwa sababu ya mfumo finyu wa Czech.

Morten Hjulmand - Denmark

Umri wake ni miaka 24. Ni kiungo wa Sporting. Amekuwa sehemu ya timu ya Ruben Amorim iliyoshinda taji la ligi ya Ureno msimu huu.

Ana umri wa miaka 25 baadaye mwezi huu lakini huu haukuwa msimu wake wa kwanza akiwa Sporting na alicheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa mwezi Septemba, hivyo bado ni mpya kabisa.

Kenan Yildiz - Uturuki

k

Chanzo cha picha, getty images

Maelezo ya picha, Yildiz aliisaidia Juventus kuishinda Atalanta katika fainali ya Coppa Italia msimu uliopita

Umri wake ni miaka 19. Ni m shambuliaji wa klabu Juventus. Mzaliwa wa Ujerumani alifunga katika Olympiastadion mjini Berlin katika mchezo wake wa kwanza wa kimataifa Novemba wakati Uturuki ilipoishinda Ujerumani katika mji wao mkuu.

Aliondoka Bayern Munich majira ya joto wakati mkataba wake ulipoisha na akakataa ofa kutoka Barcelona, akipendelea kujiunga na Juventus.

Lazar Samardzic – Serbia

Umri wake ni miaka 22. Ni kiungo wa klabu ya Udinese. Ni zao la timu za vijana za Hertha Berlin na RB Leipzig, alihamia Udinese miaka mitatu iliyopita na nusura ajiunge na Inter Milan msimu wa joto uliopita.

Uhamisho wa dirisha hili unaonekana kuwa wa uhakika kwenda Juventus - wanaongoza orodha ambayo inasemekana inajumuisha Borussia Dortmund na Brighton.

Adam Obert - Slovakia

Umri wake ni 21. Ni beki wa kati wa Cagliari. Amewahi kuwa nahodha wa kikosi cha Slovakia chini ya umri wa miaka 21 na yuko tayari kuichezea timu ya wakubwa, baada ya kucheza mechi zote mbili za kirafiki za Machi dhidi ya Austria na Norway.

Uamuzi wa Cagliari kumsainisha mkataba mpya msimu uliopita wa kiangazi unaonekana kuwa wa busara.

Zan Vipotnik - Slovenia

k

Chanzo cha picha, getty images

Maelezo ya picha, Vipotnik

Umri wake ni miaka 22. Ni mshambuliaji wa klabu ya Bordeaux. Vipotnik alifunga katika mechi yake ya kwanza ya kimataifa dhidi ya Kazakhstan mwaka mmoja uliopita na kuhama kutoka Maribor hadi Bordeaux muda mfupi baadaye.

Mabao kumi ya Ligue 2 yalimfanya kuwa miongoni mwa wachezaji wachache waliojitahidi wakati wa mafanikio mabaya ya Bordeaux.

Imetafsiriwa na Rashid Abdallah na kuhaririwa na Ambia Hirsi