Wadudu,wanyama nao huwapa wenzi wao zawadi, unajua kwanini?

Ndege madume hutoa zawadi kwa majike

Chanzo cha picha, Alamy

Muda wa kusoma: Dakika 4

Tunafikiria kutoa zawadi kama hulka ya kibinadamu tu, lakini kuna spishi nyingi ambazo hutoa zawadi kwa wenzi wao.

Utashangaa kujua ni zawadi gani ambayo wadudu wa kiume huwapa scorpionfly wa kike. Mdudu dume hutoa mate kama zawadi kwa jike.

Nge jike hufurahishwa na zawadi hiyo ya kupendeza. Inampa mwenzi fursa ya kuoana naye. Hii humpa nge jike virutubisho vingi. Pia, ikiwa ataolewa na wanaume wengi, pia anapata faida za maumbile kupitia zawadi hii ya mate.

Aina kama vile konokono, minyoo, na ngisi wamekutwa wakitoa zawadi kwa wapenzi wao. Aina hizi hutoa kipande cha lishe cha chakula kabla ya kumkaribia mwenzi wao.

Ndege pia wanajulikana kufurahia kutoa zawadi. Shrikes Mkuu wa Kijivu wa dume, hujaribu kuwavutia wenzi wao kwa kuonesha uhodari wao kwa kuwanasa wadudu wadogo kwenye miiba na matawi.

Unaweza kusoma
Buibui huwapa wenzao chakula kwa hariri (utando mwembamba unaofanana na nyuzi za protini).

Chanzo cha picha, Getty Images

Mbinu ya buibui

Kutoa zawadi ni jambo la kawaida kati ya wadudu na wanyama. Kwa mfano, nondo wa kiume mwenye madoa sita humpa mwenzi wake zawadi ya sianidi katika mbegu zake za kiume.

Taarifa za kemikali ambazo wadudu hutoa ili kuwasilisha ujumbe wa kujamiiana kwa wenzi wao pia ni muhimu.

Buibui huwapa wenzi wao chakula kilichofunikwa kwa hariri (uzi mwembamba wa nyuzi za protini ambazo buibui husuka kwenye utando wao). Wanaongeza kemikali ili kufanya chakula kivutie zaidi. Ikiwa buibui wa kike wanakataa, hufunga zawadi kwa hariri zaidi na kutoa tena.

Wakati mwingine madume hawa hujaribu kuwahadaa buibui jike kwa kufungia chakula cha ubora wa chini au chakula kilichoharibika, kilicholiwa nusu (vipande) kwenye hariri. Huku jike akiwa na shughuli ya kufunua zawadi hiyo, wanaume huchumbia nao kukimbia kabla ya jike kutambua kwamba wao ni bandia.

Utafiti uligundua kuwa asilimia 70 ya zawadi zinazotolewa na buibui zilikuwa bandia.

Ndege

Chanzo cha picha, Getty Images

"Wadudu wa dume hujaribu kudanganya. Wanafunga chakula katika hariri ambayo ni ya zamani au iliyokauka," anasema Daryl Guan, mwanaikolojia wa tabia katika Chuo Kikuu cha Toronto nchini Canada.

Wadudu wengine pia wamejulikana kujaribu kudanganya katika suala la malipo.

"Tukio zuri lilitokea karibu na nyumba yetu wakati wa chemchemi. Nzi wa kiume alienda mtoni na akarudi na kuumwa na wadudu ndani ya maji. Majike walimiminika kwenye chakula alicholeta.

Kwa sababu majike hawawezi kupata chakula peke yao. Wanahitaji lishe hii ili kutaga mayai. Katika kisa kimoja, wadudu wa kiume walileta kidonge cha manyoya ambacho, ambao ulichukuliwa kutoka kwa mbegu za mti umeao karibu na maji, (Willow).

Kutoa zawadi zisizo na thamani kunaweza tu kutoa faida za muda kwa wadudu wa kiume.

Chanzo cha picha, Getty Images

Kutoa zawadi zisizo na thamani kunaweza tu kutoa faida za muda kwa wadudu wa kiume.

Hii ni kwa sababu jike, anapofungua zawadi na kutambua kwamba amedanganywa, huwakataa wadudu wa kiume.

Hii ina maana kwamba wadudu dume wanaweza tu kujamiiana na jike kwa muda mfupi. Wadudu jike kwa kawaida hukutana na madume wengi.

Kwa hiyo, wadudu wa kiume wasio waaminifu hawana wa kurutubisha mayai na mbegu zao.

Wadudu wengine, hata hivyo, huhatarisha maisha yao kama zawadi kwa wanawake wanaotaka kuwavutia.

Wakati wa kujamiiana, mdudu dume wa sagebrush humruhusu jike kunyonya mbawa zake na kunyonya hemolymph, umajimaji unaofanana na damu.

Utafiti unasema kwamba kadiri nguvu inavyopungua baada ya hili kutokea, uwezekano wa mdudu dume kuoana tena na kupata mpenzi hupungua.

Buibui mwekundu dume huruhusu jike kuuma mwisho wa tumbo lake wakati wa jike kupandwa.

Wakati mwingine wanyama pia hutoa zawadi ili kumfurahisha mpokeaji.

Chanzo cha picha, Alamy

"Ni nadra sana kwa buibui wekundu kupata jike wa kujamiiana naye. Kwa upande wa utimamu wa Darwin, kwa kulalia chali na kumsumbua jike kwa chakula, huongeza muda wa kujamiiana. Matokeo yake, wanapata mbegu nyingi zaidi. matokeo yake, huzaa watoto zaidi," Daryl alielezea.

Pomboo

Chanzo cha picha, Getty Images

Kwa mfano, pomboo wamejulikana kuwaletea watu tuna, mikunga, na pweza ili kuwafurahisha. Pia kuna hadithi za kunguru kutoa zawadi kwa watu na kuwasaidia katika siku za nyuma.

"Nimepokea jozi, mizeituni, vifuniko vya chupa, vikombe vya divai kama zawadi kutoka kwa kunguru," Nicola Clayton, profesa wa utambuzi linganishi katika Chuo Kikuu cha Cambridge nchini Uingereza alisema.

Sokwe watu

Chanzo cha picha, Getty Images

Sokwe mtu, jamii ya nyani ambayo inashiriki karibu asilimia 99 ya vinasaba vya binadamu, pia hutoa zawadi ili kuwafurahisha wengine.

Utafiti wa 2013 uligundua kuwa, kama wanadamu, sokwe watu pia hutoa zawadi kwa wageni.

Sokwe watu hutoa zawadi ya vitu kama tufaha na ndizi na wanyama walio nje ya kundi lao, na wako tayari hata kuacha chakula chao kwa ajili ya kuwasiliana na wanyama wasiowafahamu.

Yote hii inaleta swali la kwa nini wanyama hutoa na kupokea zawadi. Aina tofauti zimeibuka mara nyingi kufanya hivyo. Kufanya hivyo kumeongeza uwezekano wa kuimarisha mfumo wa uzazi kwa madume na majike. Hii hakika hutokea katika aina kama wadudu na buibui.

"Madume hutoa chakula kwa majike. Majike husaidia wanaume kuzaliana," Daryl alisema.

Imetafsiriwa na Lizzy Masinga