Maisha ya Siri ya kujamiiana ya Mimea

mm

Njia zinazoshangaza na hatari kwa kiasi fulani ambazo aina fulani ya mimea utumia kuzaliana.

Maisha ya ngono ya mimea yanaweza kuwa ya ajabu. Na hapa tunamaanisha ajabu sana.

Kwa miaka mingi kuna baadhi yao wameunda mbinu za kushangaza za kueneza mbegu zao na kuhakikisha uhai wa aina ya mbegu zao zinapatikana. Hebu tuangalie njia 7 zisizo za kawaida ambazo mimea hufanya ngono.

Mimea ambayo mbegu zake huwa zinalipuka

Baadhi ya Matango huenda kwa umbali urefu ili kusambaza mbegu zao. Mmea wake huwa unasambaza mbegu kama mlipo fulani ambao huwa ni sababu nzuri.

Mmea wa jamii hii huwa unategemea matakwa ya

wanadamu na wanyama katika kueneza mbegu zao, kielelezo hiki cha kusisimua kina njia ndogo sana ya kujieneza yenyewe. Hulipuka, na kurusha mbegu zake kwa umbali wa mita sita (futi 20) na kutawanyisha mbegu.

Ili kufanikisha katika hili, tunda linaloning'inia huwekwa chini ya mkazo mkubwa sana wa ndani linapoiva.

Hujaa hadi kupasuka kwa mbegu na utomvu na kufikia shinikizo la 27- takribani sawa na vile ungepitia karibu mita 280 (futi 915) chini ya maji. Shinikizo linapokuwa kubwa sana, tunda hudondoka na utomvu hutolewa nje kwenye safu, na kusambaza mbegu zake.

mm

Maua yanayojulikana kama Orchid

Maua haya ni mojawapo ya familia kubwa na tofauti zaidi ya mimea mingine ya maua: kuna aina 25,000 kati yao, zinazopatikana katika makazi yote ya mabara sita. Sababu ambayo wamefanikiwa kujieneza maeneo mbalimbali ni rahisi. Ni mazuri sana katika kuzaliana kwa njia za ajabu za uerevu.

Spishi moja kama hiyo, hupatikana katika milima ya mbali ya Mediterania. Kama jina lake linavyodokeza, huwashawishi nyuki wa kiume kujifanya wakike jinsi wanavyotazamwa kwa nyuma. Pia huwa yanatoa harufu sawa.

Nyuki aliyedanganywa na kitendo hiki cha udanganyifu wa kijinsia, anatua juu yake kufanya tendo kwa msisimko. Lakini katika kuchanganyikiwa na kufadhaika kwake, hupata hasira na kupeleka mbegu za ua hilo kwa ua lingine ambalo pia linamdanganya. Ni wazi kuwa unaweza kumdanganya nyuki zaidi ya mara moja.

mm

Mti unaobadilisha Jinsia

Tawi la mti wa parachichi ni tofauti kabisa na mmea mwingine wowote. Katika mazingira yake ya asili huko Kusini mwa Mexico, miti ya parachichi inaweza kubadilisha jinsia katika muda wa saa chache. Maua yao yana viungo vya ngono vya kiume na vya kike, zisivyoweza kufanya kazi kwa wakati mmoja. Badala yake, ina ‘hatua’ za kike na kiume, jambo ambalo hupunguza uwezekano wa kupata mbegu zake.

Hivyo, ikiwa ua ni la kike linapofunguka, linaweza kuchafuliwa na wadudu. Lakini itakapofunguliwa tena siku inayofuata, mabadiliko ya ajabu yatakuwa yamefanyika: kitendo hicho hakifanyiki tena, badala yake zinachukuliwa na viungo vyake vya kiume. Sasa hutumia njia hii kueneza mbegu zake yenyewe, kabla ya ua kufungwa tena.

.

Msambazaji mbegu anayelala

Matunda maarufu ya mti wa hazel uzaa kwa njia ya kipekee. Kama ilivyo kwa parachichi, miti hii hubeba sehemu za kiume na za kike.

Sehemu zake za kiume ni maua marefu, yaliyoinama ambayo yanapasuka kwa njia ya kupendeza katika kina cha majira ya baridi.

Huwa, kama unavyoweza kukisia, ni wachavushaji wake, nao hueneza mbegu zao siku zenye upepo.

Miti ya karibu huchukua maua yao madogo, mekundu ya ‘kike’. Mti wa hazel hauwezi kujichavusha, lakini kwa kuwa mbegu zake zinaweza kusafiri hadi futi 50, hivyo sio shida kamwe.

Kwa kawaida, hakuna kinachotokea mara tu zinapofika kwenye ua. Badala yake, chavua hulala hadi mwishoni mwa majira ya kuchipua, na hatimaye inarutubisha mti. Na baada ya majuma sita mengine, mbegu hukua kabisa.

mm

Mnyanyasaji wa kingono

Iwapo nyuki waliokuwa wakining'inia karibu na ua wakifikiri kwamba walikuwa na hali mbaya, walipaswa kukutana na Jack-in-the-pulpit. Au tuseme, hawapaswi kuwa hapo kabisa. Misitu hii hatari ya kudumu, inayopatikana katika sehemu za mashariki za Amerika Kaskazini, ina njia ya kuvutia ya uzazi.

Sehemu ya juu ya ua lake lenye milia meupe na kahawia ni nyeusi zaidi ndani.

Nyuki huruka ndani - mahali ambapo giza huwasumbua na huchukua chavua wanapozunguka zunguka. Mara baada ya kuondoka nayo, wanaona kile kinachoonekana kuwa njia ya kutoroka.

Lakini inageuka kuwa wamedanganywa!

Huu ndio msingi wa kike wa maua na hakuna njia ya kutoka.

Nyuki baada ya kuchafua maua ya mmea bila kukusudia, anaachwa afe, akiwa ametimiza kusudi lake

mm

Mchanganyiko wa Mimea

Nchini Ufaransa, Amerika Kusini, utakuta ua linalofanya kazi kama mdudu sawa majira ya usiku. Maua yanayofanana na yungiyungi, yakiwa yamejazwa na bua ili ‘kuunganisha’, hutoa joto, manukato, chakula cha kutosha, na mahali penye giza, tulivu pa kulala.

Hapa ndipo mahali pazuri pa kukutana na panafaa kwa uzalishaji pia. Wadudu huchukua chavua yake wakati wa matukio yao ya usiku na kisha kuisambaza kwa maua mengine, hivyo basi kukuza mafanikio ya ngono .

mm

Maua yanayotoa harufu mbaya

Sio maua yote ni mazuri, au kuwa na harufu nzuri. Mfano kama huo ni tabia nyingine ya udanganyifu, kwa maua yanayojulikana kama 'ua la maiti' kwa sababu ya kuwa na harufu mbaya ambayo hutoa ili kuvutia wenzie wanaopenda nzi.

Wanaponusa kile wanachoamini kuwa ni chakula kitamu cha nyama iliyooza, wadudu hao huchunguza maua, wakihamisha chavua bila kukusudia kutoka sampuli moja inayonuka hadi nyingine.

Haya ni ya kupendeza sana ina maua mekundu na kahawia na mara nyingi maua makubwa ya kutisha. Yanaweza kukua hadi zaidi ya mita tatu (futi 10) kwa urefu.

Inaonekana hisia za ngono za mimea ni tofauti zaidi kuliko kitu chochote tunachoweza kufikiria hata katika ndoto zetu. Waenezaji hawa ni wa kipekee huleta maana mpya kabisa .