Viumbe vipya vya ajabu vya bonde la Congo

Chanzo cha picha, Nik Borrow
Ripoti mpya iliyotolewa tarehe 3 Disemba na shirika la uhifadhi wa wanyamapori World Wide Fund for Nature (WWF) imebainisha kuwa zaidi ya aina 700 za wanyamapori na mimea zimegunduliwa na wanasayansi katika Bonde la Kongo katika kipindi cha miaka 10 iliyopita.
Miongoni mwa ugunduzi huo ni pamoja na aina mpya wa mbuni, bundi mwenye sauti za ajabu na mamba mwenye umbo dogo.
Likijulikana kama "lungs of Africa" au ‘‘mapafu ya Afrika’’ bonde la Congo ni msitu wa pili kwa ukubwa wa mvua duniani, ukipatikana katika u nchi sita. Pia ni eneo kubwa lenye kisima kikubwa zaidi cha kaboni duniani - mfumo wa ikolojia unaofyonza hewa ya kaboni kuliko ile inayotolewa.
Ripoti hiyo inaelezea kazi ya mamia ya wanasayansi duniani kote na WWF inasema "inaangazia bayoanuai ya ajabu na mahitaji ya haraka ya uhifadhi wa moja ya mifumo muhimu ya maisha ya viumbe hai , ekolojia duniani".
Mwezi uliopita, WWF ilichapisha matokeo ya hifadhi za ulimwengu wa asili ambazo zilionyesha kupungua kwa asilimia 73 kwa idadi ya wanyamapori duniani.
"Bonde la Congo halijulikani lenyewe, na watu wengi hawajui umuhimu wake," Jaap Van der Waarde, Mkuu wa Uhifadhi wa bonde la Congo, anaiambia BBC.
Van der Waarde anaeleza kuwa mbali na kuwa na viumbe hai wengi wa kipekee, bonde hilo ni la mwisho kati ya safu kubwa za misitu ya mvua duniani ambazo bado zinafyonza kaboni zaidi kuliko inavyotolewa - tofauti na msitu wa Amazon, ambao umekuwa ukipoteza uwezo huo.
"Spishi mpya zinaweza tu kulindwa tu iwapo uwepo wake utaendelezwa. Na tusisahau kwamba bonde la Congo linahitaji sana utulivu wa hali ya hewa," anaongeza.
Bundi anayetoa mlio wa sauti ya 'nyau'

Chanzo cha picha, WWF
Bundi wa Principe (Otus bikegila), aliyegunduliwa mnamo 2022, hupatikana tu katika taifa dogo la kisiwa cha Sao Tomé na Príncipe.
Ana masikio yenye muundo wa tawi na sauti yake haifanani na ya mlio wa paka. Kulingana na Birds of the World, hifadhidata ya ndege duniani, bundi huyo yuko hatarini sana, akiishi katika mazingira yenye idadi ya watu kati ya 1,100 hadi 1,600.
Pink Floyd mwenye mabawa

Chanzo cha picha, Jens Kipping
Kundi la mwamba wa Uingereza la Pink Floyd liliruka kwa kasi juu ya London katika miaka ya 1970. Lakini pia limehamasisha jina la aina mpya ya mdudu aliyegunduliwa katika bonde la Congo.
Umma gumma ulipewa jina la albamu ya Pink Floyd ya mwaka 1969 ya Ummagumma na timu ya wanasayansi ambao hawakuweza kupinga kuwa pun - umma ni neno linalotumika kuainisha aina fulani za wadudu.
Nyoka wa kutisha na mjanja

Chanzo cha picha, Jean-François Trape
Licha ya kugunduliwa tu mnamo 2020, Mongo ambaye ni nyoka mwenye sumu na nywele (Atheris mongoensis) tayari anajulikana kwa kuwa moja ya aina ya nyoka wenye sumu zaidi barani Afrika.
Ni hatari zaidi hasa kutokana na uwezo wake wa kubadilikabadilika rangi yake anapotafuta mawindo: mchanganyiko wa kijani, njano na nyeusi hali ambayo inamruhusu nyoka huyu kutogundulika kwa urahisi katika mazingira ya misitu.
Chura mdogo anyetoa ishara

Chanzo cha picha, Vaclav Gvozdik
Chura wa Congo (Congolius robustus) ni chura ambaye hadi sasa ameonekana tu katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, baada ya kupatikana katika maeneo kadhaa kusini mwa Mto Congo.
Ana urefu wa chini ya sm 4cm na kuishi kwake katika eneo dogo - hutumika kama kiashiria muhimu hali ya mazingira ya makazi yake.
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi












