Wafahamu ndege wa Tanzania wanaokabiliwa na tisho la kuangamia
Toka enzi za kale baadhi ya ndege wamekuwa wakitumika kama njia ya asili ya kutoa ishara kwa wakulima na wananchi wa jamii za kiafrika hasa Tanzania kuashiria kipindi cha masika au kiangazi.
Miongoni mwa ndege hao ni Lesser Flamingo ambao wanapatikana nchini Tanzania ambapo wataalamu wanasema kuwa ndege hawa wapo katika hatari ya kutoweka katika uso wa dunia kutokana na mabadiliko ya tabia nchi na uharibifu mkubwa wa mazingira unaofanywa na binadamu.
Mwandishi wa BBC @frankmavura ametembelea moja ya kijiji kilichopo wilaya ya Kibiti nje kidogo ya jiji la kibiashara la Dar es Salaam na kutuandalia taarifa ifuatayo.