Wanyama wanaoweza kusafiri mbali zaidi duniani

Chanzo cha picha, Thikstock
Wanyama wengi hutembea maelfu ya maili kila mwaka kutafuta chakula, maji na kuzaana.
Lakini ni vigumu kubaini ni mnyama yupi anatembea mwendo mrefu zaidi, kutokana na sababu mbili.
Kwanza, baadhi yao husafiri kwa awamu, kumaanisha muda kamili wa kila "safari" unaweza kuhojiwa.
Pili, safari ya ardhini sio sawa na ya majini au angani. Kwa mfano, wanyama wanaopaa angani na wale wanaoogelea baharini wanasaidiwa na upepo mkali au mawimbi makali, wakati wale wanaotembea ardhini wanajifanyia kila kitu.
Tuanze na wanyama wa baharini
Nyangumi wanasafiri mwendo mrefu kutokana na uhamaji wao wa kila msimu.
Awali ilidhaniwa kwamba nyangumi wa rangi ya kijivu ndio wenye kasi zaidi, lakini mwaka 2007 nafasi hiyo ilichukuliwa na nyangumi aina ya humpbacks, wakati utafiti ulipobaini wanaogelea kwa kasi ya kilomita 8,299 kati ya Costa Rica and Antarctica. Uhamiaji ambao ni wa mbali zaidi wa wanyama hao.
Hata hivyo, papa wameshindwa na samaki: hususan, papa mweupe. Mfano wa kike aliyepewa jina la utani la "Nicole" aliogelea karibu kilomita 11,100 kutoka Afrika Kusini had Magharibi mwa Australia, na kurejea tena baada ya miezi tisa.

Chanzo cha picha, Thinkstock
Maisha ya wanyama wa baharini hufuata mkondo fulani wa uhamaji, lakini baadhi yao husafiri mbali kila siku.
Safari hizo hufanyika usiku, kama zile za samaki na plankton, ambao huogelea wima hadi karibu kina cha bahari kutafuta lishe.
Ardhini
Msimu wa kiangazi na wa mvua huchangia uhamiaji kwa mzunguko wa kilomita 3000 wa nyumbu wa bluu Afrika Mashariki.

Chanzo cha picha, Thinkstock
Wadudu
Hata hivyo, safari hizi hudhibitiwa kiasili na mipaka ya ardhini na majini. Angani hakuna mipaka.
Moja ya uhamaji wa kuvutia zaidi ni ule wa vipepeo wa aina ya monarch, ambao huruka kilomita 4,000 kwenda na kurudi kati Mexico na Canada.
Wengine wanaofanya hivyo ni vipepeo aina ya Vanese thistle ambao wana uwezo wa kuruka kutoka jangwa la Kaskazini mwa Africa hadi mzunguko wa Aktiki katika safari ya kilomita15,000 mduara.
Nzi aina ya dragon ambao wanafahamika Kama Pantala flavescens kwa jina la kisayansi wanachukuliwa kuwa wadudu ambao wanasafiri mwendo mrefu zaidi, huenda ni zaidi ya kilomita 18,000 kwa sababu wanasafiri kutoka India hadi Afrika Mashariki na kurudi.
Lakini sawa na vipepeo, wadudu hao hawaishi maisha marefu na hawawezi kusafiri hadi mwisho Uhamaji huo wa miaka hukamilishwa na vizazi vingine.
Ndege ndio mabingwa
Linapokuja suala la safari za mbali, ndege wanaongoza.
Hata spishi ndogo zaidi wanauwezo wa kuruka na kwenda mbali sana.

Chanzo cha picha, Thinkstock
Ndege aini ya albatrossi - wanasadikiwa kuwa ndege wakubwa wanaopaa duniani - ndege hao wanauwezo wa kuruka kwa zaidi ya kilomita 5,500. Ndege haha wanaweza kuzunguka dunia kwa siku 46 .
Hii inatokana na maumbile yao ya kipekee yanayowawezesha kuruka mbali. Kupitia mfumo unaojulikana kama kuinua kwa nguvu, albatrossi wanatumia nguvu kidogo kuliko mabawa ya ndege, hali inayowafanya kuruka mbali kuwa jambo rahisi.

Chanzo cha picha, Thinkstock
"Safari ya mwaka mmoja wanaweza kuruka hadi kilomita 30,000 , " anaelezea mwanajiolojia na mtafiti wa Marekani wa masuala ya biolojia Lee Tibbetts. "
Safari hiyo inaweza kukamilishwa na ndege ya kawaida kupitia safari ya siku tatu mfululuzo kwa karibu siku 20."
Tibbetts na watafiti wenzake waliochunguza uwezo wa kuruka wa ndege hao, wanahofia huenda wakaangamia.
"Sote tunajiuliza ikiwa usafari wa mwendo mrefu namna hiyo unaweza kufanywa bila kupumzika ili wapate nguvu zaidi ya kuruka na kuzaana. Ishara ya kwanza tuligundua kwamba ndege hawa hawabadili mwendo wao kuulingana na mazingira yalivyo, Tulipochunguza uwezekano wa kunusurika. Na kupungua kwa idadi yao, "anaonya Tibbetts.












