Tetesi za Soka Ulaya Jumatano: Klabu tatu za Saudia zinamfukuzia Son Tottenham

Son

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 2

Klabu za soka za Al-Ahli, Al-Nassr na Al-Qadsiah ncjini Saudi Arabia zimeonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa Tottenham Hotspur na Korea Kusini Son Heung-min, 32, na ziko tayari kulipa pauni milioni 34. (Sportsport)

Bayern Munich itaelekeza macho yake kwa winga wa Brighton na Japan Kaoru Mitoma, 28, na mshambuliaji wa Liverpool na Uholanzi Cody Gakpo, 26, ikiwa haitafanikiwa kumsajili winga wa Uhispania na Athletic Bilbao Nico Williams, 22. (Sky Germany).

Mlinda lango wa Uingereza Tom Heaton,39, atasalia Old Trafford baada ya kufikia mkataba wa mwaka mmoja na Manchester United . (Fabrizio Romano)

Beki wa Bournemouth na England Max Aarons, 25, ananyatiwa naklabu ya Rangers, huku Cherries wakipania kumsajili kwa mkataba wa kudumu badala ya mkopo. (Daily Record)

Beki wa Chelsea Muingereza Zak Sturge, 21, yuko mbioni kujiunga na Millwall kwa mkataba wa kudumu baada ya kuichezea klabu hiyo kwa mkopo msimu uliopita. (Daily Express)

AC Milan imekutana na wawakilishi wa kiungo wa Bayer Leverkusen na Uswizi Granit Xhaka, 32. (Football Italia)

.

Chanzo cha picha, Reuters

Napoli iko mbioni kumsajili winga wa Manchester United na England Jadon Sancho, 25, baada ya kipindi chake cha mkopo bila mafanikio akiwa Chelsea. (Gianluca di Marzio - kwa Kiitaliano)

Nottingham Forest inavutiwa na kiungo wa Colombia na klabu ya Palmeiras Richard Rios, 25, ambaye mkataba wake unajumuisha kipengele cha kuachiliwa cha takriban £85m. (Give me Sport)

Klabu za Leeds United na Aston Villa zinamuwania kiungo wa kati wa Strasbourg na Senegal Habib Diarra, 21. (Sports Mole)

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi