Vita vya Ukraine: Mashambulizi yamepungua, lakini kuiondoa Urusi ni kazi ngumu

ggg

Chanzo cha picha, SOPA IMAGES

Wachache wanaijua vizuri gharama ya kukabiliana na ushawishi wa Urusi kuliko Viktor Yushchenko.

Rais huyo wa zamani wa Ukraine aliwekewa kemikali yenye sumu alipokuwa akifanya kampeni mwaka 2004 dhidi ya mgombea aliyependekezwa na Moscow.

Kisha aliongoza maandamano dhidi ya uchaguzi ulioibiwa kabla ya kuchukua madaraka mwaka uliofuata.

Akiwa ameketi katika nyumba yake iliyojengwa kwa mbao nje kidogo ya mji wa Kyiv, Bw Yushchenko anasifu "nguvu ya uzalendo kitaifa" kama ufunguo muhimu wa uhuru wa Ukraine.

"Leo naweza kusema kwa kujiamini kwamba Waukraine milioni 42 wanazungumza sauti moja. Na hiyo inaruhusu sisi kukabiliana na adui yeyote, ikiwa ni pamoja na Urusi."

Bado unaweza kuona kovu kwenye uso wa rais huyo wa zamani tangu alipowekewa sumu.

ggg

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Rais wa zamani wa Ukraine Viktor Yushchenko: "Kigezo cha uhuru ni nguvu ya umoja"

Siku ya uhuru wa Ukraine inaangukia miezi sita tangu Vladimir Putin alipoanzisha uvamizi kuanzia kaskazini, mashariki na kusini. Wakati huo, jeshi la Ukraine linasema karibu watu 9,000 wameuawa. Baadhi ya vifo vya raia 5,500 vimethibitishwa na Umoja wa Mataifa.

Ingawa ni wachache hapa waliotabiri vita, Bw Yushchenko analaumu kwa kiasi kikubwa kile anachokiona kama historia ya nchi za Magharibi kutokuwa na uwezo wa kupambana na ukatili wa Urusi, haswa mzozo wa 2008 huko Georgia na kuchukuliwa kwa Crimea miaka sita baadaye.

Hata hivyo, anadhani mtihani wa mwisho wa Ukraine umebadilisha msimamo wake duniani.

"Leo, wakati zaidi ya nchi 50 zinaonyesha mshikamano katika mapambano yetu. wanatoa kila aina ya msaada ikiwemo kijeshi, kifedha na kibinadamu."

Useremala sasa unachukua muda mwingi wa kiongozi huyo wa zamani. Tumezungukwa na sanamu nyingi na rais wa zamani ananiambia juu ya imani yake kamili kwamba Ukraine inaweza kupata ushindi katika vita hivi.

Maelfu ya raia wa Ukraine walijiunga na jeshi kupigana na Urusi mwanzoni mwa vita wakiwemo wanamuziki wa bendi ya rock ya Antytila.

Kadiri Urusi inavyojaribu kuivuta Ukraine kwenye mzunguko wake, ndivyo hisia za watu wake za Utaifa zinavyozidi kuwa na nguvu.

Katika kiwanda kidogo kwenye ukingo wa kushoto wa mto Dnieper uliopo Kyiv, biashara ya Nataliia ilikuwa ikitengeneza sare za hoteli, lakini sasa inazalisha bendera za Kiukraine.

ggg
Maelezo ya picha, Maombi ya kununua bendera za Ukraine yameongezeka tangu uvamizi wa Urusi miezi sita iliyopita

Alianza kupata maombi kutoka katika vituo vya ukaguzi vya kijeshi mwanzoni mwa uvamizi huo, sasa anapokea zaidi ya maombi 2,500 kwa mwezi - sio tu kutoka kwa jeshi, lakini kwa biashara pia.

"Hizi ni rangi tunazopenda sana," anasema.

"Kila raia wa Ukraine anahisia na rangi hizi na tunawaona katika kila kitu. Hii inatupa raha, furaha na hisia nzuri, kwa sababu kazi yetu ni muhimu."

Miezi sita ya vita, Ukraine inaonyeshwa baadhi ya uhalisia usiopendeza.

Baada ya wiki kadhaa ya kuzungumzia, mpango wa kukabiliana na mashambulizi ya Ukraine uliopangwa kusini, kwenye mji unaokaliwa wa Kherson, bado haujatimia.

Kumekuwa na mashambulizi ya makombora ya masafa marefu zaidi ndani ya eneo linaloshikiliwa na Urusi, lakini vita hivi sasa vinatawaliwa na mizinga kwenye mstari wa mbele.

ggg
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kufikia sasa silaha za Magharibi zinaisaidia Ukraine kushikilia usambazaji na kutibua usambazaji wa Urusi, lakini itakuwa kitu cha kutetemesha sana kubadilisha na Kyiv kuiondoa Urusi kabisa.

Kwa hivyo, hali hii ya kijeshi inaonekana kuendelea, kwa gharama inayokua isiyoweza kufikiriwa kwa makumi ya maelfu ya familia.

Pia - wakati anatazamwa sana kama shujaa wa vita wa nchi hiyo, Rais Volodymyr Zelensky sasa anakabiliwa na ukosoaji wa jinsi alivyojiandaa kwa shambulio la Urusi. Hasa juu ya uamuzi wake wa kutoshughulikia maonyo kutoka Marekani, akisema itasababisha hofu na kuharibu uchumi wa Ukraine.

Ishara nyingine ya ukaidi wa Ukraine iko kwenye chumba cha habari cha Kyiv Independent.

Tovuti hii ya habari ya lugha ya Kiingereza ilianzishwa wiki kadhaa kabla ya uvamizi. Ndani ya siku kadhaa wafuasi katika mtandao uliongezeka kutoka makumi ya maelfu hadi mamilioni.

"Ni Siku ya Uhuru ambayo hatukujua ingetokea," anasema mhariri mkuu Olga Rudenko.

ggg
Maelezo ya picha, Olga Rudenko, mhariri mkuu wa Kyiv Independent, tovuti ya habari iliyoanzishwa wiki chache kabla ya uvamizi wa Urusi.

Anaelezea jarida hilo kama sauti ya Ukraine na dirisha la dunia ndani yake.

"Hapo nyuma mwezi Februari, wakati mambo hayakuwa ya uhakika, hatukujua kama sehemu kubwa ya nchi ingevamiwa au ikiwa tungeuawa," anasema. "Kuwa bado kuweza kusherehekea, kuna maana sana."

Mkataba wa hivi majuzi, ambao umeiruhusu Ukraine kwa mara nyingine tena kusafirisha nafaka kupitia Bahari Nyeusi, unasalia kuwa mafanikio pekee ya kidiplomasia katika vita hivi.

Wengine wanaona kuwa kama msingi wa mkataba wa amani.

Hiyo ni mbali sana na Ukraine tayari imepoteza udhibiti wa sehemu ya tano ya eneo lake.

Ili kudumisha uhuru wake, nchi hii itategemea ulimwengu wa nje kwa usaidizi kwa muda.