Mzozo kati ya Urusi na Ukraine: Hatua 5 zinazoweza kuzuia vita

Chanzo cha picha, Reuters
Matokeo ya vita nchini Ukraine yanatisha zaidi, ikiwa Urusi itaivamia nchi hiyo, maelfu ya watu wanaweza kuuawa na wengine wengi kukimbia.
Gharama za kiuchumi na kibinadamu zitakuwa kubwa.
Urusi inaendelea kujenga vikosi vyake karibu na Ukraine, na nchi za Magharibi zinaendelea kutishia matokeo mabaya ikiwa Urusi itavuka mpaka.
Kwa hivyo kuna njia ya kidiplomasia, njia ya kuepusha makabiliano haya ambayo ni ya amani na ya kudumu?
Wanadiplomasia wanazungumza njia ambapo pande zote zinaweza kuzuia vita. Lakini kupata njia kama hiyo sio rahisi.
Maelewano yoyote yanaweza kuwa yenye gharama. Hapa hata hivyo, hizi ni baadhi ya mbinu zinazowezekana ambazo hazihusishi makabiliano ya kijeshi na kwa hivyo kuzuia umwagikaji damu.
Nchi za Magharibi zinaweza kumshawishi Rais Putin arudi nyuma.
Katika hali hii, mataifa ya Magharibi yanaweza kuzuia uvamizi wowote kwa kumshawishi Rais wa Urusi Vladimir Putin kwamba gharama zitazidi faida.
Anaweza kuamini kwamba hasara za kibinadamu, vikwazo vya kiuchumi na kuzorota kwa diplomasia vitakuwa vikubwa sana hivi kwamba hali inaweza kuwa mbaya zaidi hata kama atapata mafanikio ya kijeshi kwenye vita.

Chanzo cha picha, Getty Images
Anapaswa kuogopa kwamba nchi za Magharibi zitaunga mkono uasi wa kijeshi nchini Ukraine, na hivyo kuziweka katika hali ya vita vya gharama kubwa kwa miaka mingi.
Bwana Putin anapaswa kuamini kuwa gharama hizi zinaweza kudhoofisha uungwaji mkono wake nchini Urusi na hivyo kutishia uongozi wake.
Katika hali hii, nchi za Magharibi pia zitalazimika kumruhusu Bw. Putin kudai ushindi wa kidiplomasia, akijionyesha kama mhusika mkuu wa amani ambaye hakutaka kujibu kijeshi uchokozi wa NATO.
Bw Putin anaweza kusema kwamba hatimaye amevutia hisia za nchi za Magharibi na kwamba viongozi wake wanajibu kile wanachokiita "maswala yake halali ya usalama". Urusi inaweza kuwa imeukumbusha ulimwengu kuwa ini nguvu kubwa na imeimarisha uwepo wake huko Belarus.
Ugumu wa simulizi hii ni kwamba itakuwa rahisi kusema kwamba Bw. Putin ameshindwa. Vitendo vyake vitaonekana kuziunganisha nchi za Magharibi, na kusababisha NATO kupeleka vikosi vyake karibu na mipaka ya Urusi, na kuzihimiza Sweden na Finland kufikiria kujiunga na NATO.
Tatizo ni kwamba ikiwa Bwana Putin anataka kudhibiti Ukraine na kudhoofisha NATO, kuna sababu ndogo ya yeye kurudi nyuma sasa.
NATO na Urusi zinaweza kuafikia makubaliano mapya ya usalama
Mataifa ya Magharibi yameweka wazi kuwa hayataafikiana na kanuni za kama vile uhuru wa Ukraine, haki yake ya kuomba uanachama wa NATO, ambayo lazima iwe na "mlango wazi" kwa nchi yoyote inayotaka kujiunga.
Lakini Marekani na NATO hata hivyo zilikubali kwamba makubaliano ya pamoja yanaweza kupatikana katika masuala mapana ya usalama wa Ulaya.
Hii inaweza kuhusisha kufufua makubaliano ya udhibiti wa silaha ambayo yamepitwa na wakati ili kupunguza idadi ya makombora kwa pande zote mbili, kuimarisha hatua za kujenga imani kati ya vikosi vya Urusi na vile vya NATO, kuongeza uwazi wa mazoezi ya kijeshi na eneo la makombora, na kushirikiana katika majaribio ya silaha za kuharibu satelaiti.
Urusi tayari imeweka wazi kuwa masuala haya hayatatosha kushughulikia suala lake kuu, ambalo ni kwamba uanachama wa NATO kwa Ukraine utakuja kwa gharama ya usalama wake.

Chanzo cha picha, RUSSIAN DEFENSE MINISTRY
Lakini ikiwa, kwa mfano, uwekaji wa makombora ya NATO utapunguzwa sana, hiyo inaweza angalau kushughulikia wasiwasi fulani wa Urusi.
Kwa namna fulani, Putin tayari amefanya maendeleo katika eneo hili: Ulaya inajihusisha katika mazungumzo ya usalama juu ya masharti ya Urusi.
Ukraine na Urusi zinaweza kufufua mikataba ya Minsk
Yalikuwa ni makubaliano yaliyojadiliwa mnamo 2014 na 2015 katika mji mkuu wa Belarusi, Minsk, ambayo yalilenga kumaliza vita kati ya vikosi vya serikali na waasi wanaoungwa mkono na Urusi mashariki mwa Ukraine. .
Ni wazi kuwa alishindwa - mapigano yanaendelea.
Wanasiasa wa nchi za Magharibi wamependekeza kuwa kufufua mikataba ya Minsk sasa inaweza kuwa suluhisho la mgogoro huu.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anaamini kwamba Minsk ndio "njia pekee ya kujenga amani".
Tatizo ni kwamba masharti ya makubaliano yanavurugwa na kupingwa.
Urusi inaitaka Ukraine kufanya uchaguzi wa serikali za mitaa ili kuwapa uwezo wanasiasa wanaoiunga mkono Urusi. Ukraine inataka Urusi ianze kwa kuwapokonya silaha na kuwaondoa wapiganaji wa Urusi.
Mzozo kuu unahusu kiwango cha uhuru ambacho Minsk ingetoa kwa maeneo ya kujitenga ya Donbas. Ukriane inatetea uhuru wa kawaida. Urusi haikubaliani na inaamini kwamba Donetsk na Luhansk zinapaswa kuwa na sauti katika sera ya kigeni ya Ukraine na kwa hivyo kura ya turufu dhidi ya uanachama wa NATO.
Ukraine inaweza kutoegemea upande wowote kama Finland
Je, Ukraine inaweza kushawishiwa kupitisha aina fulani ya kutoegemea upande wowote?
Kulingana na baadhi ya habari - ambazo baadaye aziikanushwa - maafisa wa Ufaransa walipendekeza kwamba Ukraine kuchukua Finland kama mfano.
Finland ilikubali kutoegemea upande wowote wakati wa Vita Baridi. Ilikuwa nchi huru, huru na ya kidemokrasia. Ilibaki - na inabaki - nje ya NATO.
Hii inaweza kuivutia Ukraine? Hii itaepuka matokeo ya kijeshi. Kinadharia, inaweza kukidhi matakwa ya Bw. Putin ya kutotaka kuiona Ukraine ikijiunga na NATO.
Lakini Ukraine itakubali? Pengine sivyo, kwa sababu kutoegemea upande wowote kutaicha Ukraine wazi kwa ushawishi wa Urusi.
Kutoegemea upande wowote kunaweza pia kufanya uanachama wa EU kuwa mbali zaidi.
Mgogoro unaweza kuendelea kama hali ilivyo sasa

Yaweza kuwa kwamba mapambano ya sasa yanaendelea, lakini ukubwa wake unapungua kwa muda?
Urusi inaweza polepole kuwarudisha wanajeshi wake kwenye kambi zao, na kutangaza kwamba mazoezi yamekamilika. Lakini wakati huo huo, vifaa vingi vya kijeshi vinaweza kuachwa.
Urusi inaweza kuendelea kuunga mkono vikosi vya waasi huko Donbas. Na wakati wote huo, siasa na uchumi wa Ukraine utaendelea kuyumbishwa na tishio la mara kwa mara kutoka Urusi.
Kwa upande wake, nchi za Magharibi zinaweza kudumisha uwepo wa NATO ulioimarishwa katika Ulaya Mashariki. Wanasiasa wake na wanadiplomasia wataendelea kuwasiliana mara kwa mara na wenzao wa Urusi, ambapo mazungumzo yataendelea - lakini maendeleo kidogo yatafanywa.
Ukraine itaendelea kupigana, lakini angalau hakutakuwa na vita kamili.
Na polepole, makabiliano hayo yatatoweka kutoka kwa vichwa vya habari na kujiunga na orodha ndefu ya migogoro iliyohifadhiwa ambayo inafifia kutoka kwa macho ya umma.
Hakuna kati ya chaguzi hizi ni rahisi au zitawezekana. Zote zinahusisha maelewano.













