Ukraine: Jinsi Urusi ilivyojiandaa kwa shambulio

Picture of Russian soldiers

Urusi imeweka wanajeshi wake wapatao 130,000 - wakiwa na zana na kila kitu kuanzia vifaru na makombora hadi vituo vya matibabu na msaada wa vifaa - karibu na mpaka wake na Ukraine.

Wanajeshi hao wanajumuisha kikosi cha askari 30,000 kinachoshiriki mazoezi ya kijeshi katika nchi jirani ya Beralus .

Maafisa wanasema Urusi ina vikosi ambavyo viko tayari kuivamia Ukraine''wakati wowote ".

Lakini Urusi inakanusha kuwa inapanga shambulio.

Multiple rocket launchers being fire during the Allied Resolve 2022 joint military drills by Belarusian and Russian troops

Chanzo cha picha, Russian Defence Ministry

Maelezo ya picha, Mitambo ya kurusha roketi ukifyatuliwa wakati wa mazoezi ya Pamoja ya kijeshi katika Belarus

Vikosi vinavyohama

Ni wazi usaidizi wowote muhimu unaotakikana kwa ajili ya uvamizi upo katika kila eneo. Vikosi vinawasili kutoka kote nchini Urusi vimekuwa vikiongezwa kwa karibu wanajeshi 35,000 ambao wamekita kambi ya kudumu karibu na mpaka wa Ukraine.

Satellite image showing troop housing and field hospital in Belarus

Ripoti zinasema kwamba vikosi vya usaidizi muhimu kwa ajili ya uvamizi vimekuwa vikizunguka katika maeneo Pamoja na vikozi vya mapigano katika siku za hivi karibuni.

Wanajeshi hao wanasemekana kuwa wanajumuisha kikosi cha ukarabati wa vifaru, vifaa vya vya kuondoa matope na hospitali za usambazaji wa damu katika baadhi ya maeneo.

Baadhi ya wachambuzi wanasema uwepo wa hospitali zinazoweza kuhamishwa kweney maeneo ya mpaka , ni kiashirio muhimu cha utayari wa shambulio.

A serviceman of motorized rifle unit of the Russian Southern Military District takes part in a cross country driving exercise

Chanzo cha picha, Getty Images

Haiko wazi iwapo usaidizi wote muhimu kwa ajili ya uvamizi upo katika kia eneo.

Vikosi vinavyowasili kutoka maeneo yote ya Urusi vimekuwa vikiongezwa hadi kufikia wanajeshi takriban 35,000 ambao wamekita kambi kwenye mpaka na Ukraine.

Baadhi ya vikosi vipya vilivyowasili vimesafiri kutoka umbali wa takriban maili 4,000 mashariki zaidi mwa Urusi .

Nyingi kati ya siraha nzito zimekuwa zikiletwa kwa njia ya leri, baadhi zikipita kupitia mji wa Kursk, uliopo maili takriban 80 (130km) kutoka kwenye mpaka wa Ukraine.

Magari mengine yamewasili kwa barabara, kupitia jimbo la Bryansk.

Wengi wamekadiria kuwa idadi ya wanajeshi wa Urusi waliowekwa karibu na Ukraine kuwa 100,000 au zaidi.

Alhamisi, maafisa wa magharibi walisema idadi hiyo imefikia 130,000, juu ya ile iliyokadiriwa awali ya wanajeshi 100,000.

Waziri wa ulinzi wa Uingereza Ben Wallace alisema kuwa Urusi imepeleka "nusu ya wanajeshi wake wapiganaji " karibu na Ukraine au katika Belarus.

Ukraine ilitaja idadi sawa na hiyo, huku ikikadiria kuwa kikosi cha wanajeshi wa ardhini kina wanajeshi 112,000 kujumlisha na 18,000 wa kikosi cha majini n awa anga wakiwa katika maeneo ya mpaka.

Zaidi ya vikosi vya kawaida vya Urusi , inakadiriwa kuwa kuna wanajeshi wa Urusi 15,000 kutoka majimbo yaliyojitenga na Ukraine ya Luhansk na Donetsk.Ukraine inaamini kuwa idadi ya wanajeshi wanaojiandaa kwa ajili ya shambulio ni ya juu zaidi.

Mwezi wa Disemba, tathmini ya ujasusi wa Marekani ilisema jumla ya wanajeshi hao inaweza kuongezeka haraka na kufikia hadi wanajeshi 175,000.

Map showing where Russian troops are positioned. Updated 14 Feb

Wataalamu wengi wanaamini kwamba uvamizi kamili, utakaofuatiwa na kuchukuliwa kwa eneo kubwa au Ukraine nzima, utahitaji vikosi vingine zaidi kuliko vile ambavyo Ukraine imeviweka katika eneo la mpaka wake na Ukraine.

Unaweza pia kusoma:

Picha kutoka juu

Uwepo wa wanajeshi wakati mwingine unaweza kugunduliwa katika picha za setilaiti kwa rangi ya mahema.

Mahema yanayokaliwa hutambuliwa kwa kuwa huwa yamewekewa mitambo ya joto kutokana na baridi, barafu iliyoyeyuka na huw ana muonekanao wa rangi nyeusi kutoka juu .

Baadhi ya mazoezi kwa kutumia vifaru vya kijeshi yanaonekana wazi.

Satellite image showing tanks on firing range in Voronezh

Magari ya silaha yanaweza kutambuliwa kwa maumbo yake, na mataili ya malori au matope yanayoonyesha gari linalotembea.

Setilaiti zimeonyesha ongezeko la haraka la shuguli za kijeshi katika Crimea ambako, kulingana na moja ya tathmini , askari 10,000 viliwasili Januari na mapema Februali.

Satellite image showing troop shelters and vehicles in Crimea.

Kuongezeka kwa wanajeshi katika Belarus

Mazoezi ya Pamoja katika Belarus yamepangwa kufanyika hadi Februali 20.

Kiongozi wan chi hiyo, Alexander Lukashenko, anamuunga mkono Rais wa Urusi Vladimir Putin.

Satellite image showing helicopters and troop tents at Zyabrovka

Mji mkuu wa Ukraine capital, Kyiv, upo chini ya maili 100 (150km) kutoka kwenye mpaka wa Belarus.

Katibu mkuu wa muungano wa kijeshi wa Nato, Jens Stoltenberg, alisema kwamba vikosi vya mapigano 30,000 vya Urusi vilikuwa vimewasili katika Belarus, kikiwa ni kikosi kikubwa zaidi cha Urusi kuwahi kupelekwa na Moscow tangu kumalizika kwa Vita Baridi.

Picha za setilaiti zinaionyesha mitambo ya ufyatuaji wa makombora ya Urusi ya masafa mafupi- Iskander karibu na mji wa Yelsk wa Belarus, umbali wa chini ya maili 45 (72km) kutoka mpaka wa Ukraine.

Satellite image showing equipment near Yelsk. Updated 10 Feb

Miongoni mwa vifaa vya Urusi vilivyopelekwa Beralus ni Pamoja na mitambo ya ulinzi wa mashambulio ya anga, risasi na usaidizi wa kimatibabu.

Bw Stoltenberg alisema kwamba operesheni za kikosi maalumu cha Urusi kinachofahamika kama Speznaz pia ziko Beralus.

S-400 air defence system, sent by Russia, are seen at the Brestsky training ground in Belarus

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mifumo ya ulinzi wa makombora ya anga ya Urusi inayofahamika kama S-400 pia imewasili Beralus.

Ndege za kisasa za mashambulio ya nchi kavu zinazofahamika kama Advanced Su-25 pia zimepigwa picha ya setilaiti katika uwanja wa ndege wa Luninets.

Satellite image showing Su-25 aircraft at Luninets airfield. Updated 10 Feb.

Kuongezeka kwa wanajeshi katika bahari

Urusi inaendesha mafunzo na mazoezi makubwa ya jeshi la majini kuanzia bahari ya Atlantic hadi Pacific, ambayo yanafanyika katika mwezi mzima wa februari, yakigusisha takriban:

•Meli za kijeshi 140 na vyombo vingine vya usadizi vya majini

•Ndege 60

•Wanajeshi 10,000

The Admiral Essen frigate leaves Sevastopol to take part in exercises on 25 January

Chanzo cha picha, Russian Defence Ministry

Maelezo ya picha, Mkuu wa majeshi Admiral Essen akiondoka katika eneo la Sevastopol tarehe 25 Januari

Vyombo sita vya majini vya jesi la wanamaji la Urusi ambavyo vilipitia katika eneo la English Channel mwezi wa Januari sasa viko katika bahari nyeusi.

Vina uwezo wa kusafirisha mizinga mapigano, wanajeshi na magari ya silaha.

Jumamosi, Urusi ilisema kuwa zaidi ya manowari 30 zimeanza mazoezi karibu na Crimea.

The Pyotr Morgunov sails through the Bosphorus Strait en route to the Black Sea on 9 February

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mamonari ya urusi Pyotr Morgunov ilisafiri kupitia Bosphorus Strait ikielekea katika Bahari nyeusi.

Jumatatu, afisa wa kijeshi wa Urusi alisema kwamba Urusi iko tayari kufyatua moto kwa meli za kigeni na manowari ambazo zinaingia kinyume cha sheria katika maeneo yake ya maji, kulingana shirika la habari la Interfax.

Moscow imetoa tahadhari ikielezea mazoezi ya ufyathuaji wa makombora na risasi za bunduki kwenye maeneo yake ya mwambao katika bahari nyeusi.

Baadhi ya wachambuzi wanasema kuwasili kwa vikosi vya Urusi katika maeneo ya bahari kunaweza kuwa vigumu na vikosi vya majini vinaweza kuwa ni " kupoteza lengo" kwa lengo la kuyafanya majeshi ya Ukraine yasonge mbali kutoka kwenye maeneo ya ardhi yanayoweza kutumiwa katika shambulio la nchi kavu.