Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 14.07.2023

.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Riyard Mahrez

Al Ahli wanatayarisha dau la pauni milioni 30 kumnunua winga wa Algeria Riyad Mahrez, 32, kutoka Manchester City. (Athletic -Subscription required)

Kocha wa City Pep Guardiola anatazamiwa kufanya mazungumzo na Mahrez kutokana na nia hiyo kutoka Saudi Arabia. {Mirror)

Klabu ya Saudi Arabia Al-Ittihad iko tayari kutoa ofa ya pauni milioni 40 kwa kiungo wa kati wa Liverpool Fabinho mwenye umri wa miaka 29 wa Brazil. (Athletic -Subscription Required)

Kiungo wa kati wa Liverpool na Uingereza Jordan Henderson, 33, amekubali mkataba mnono kutoka kwa Steven Gerrard Al-Ettifaq. (Guardian)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Thiago Alacantara

Kiungo wa kati wa Liverpool na Uhispania Thiago Alcantara mwenye umri wa miaka 32 anaweza kurejea Barcelona msimu huu wa joto. (Sport – In Spanish)

The Reds huenda wakamnunua kiungo wa kati wa Southampton na Ubelgiji Romeo Lavia, 19. (Mirror)

Aston Villa wamewasilisha ombi lao la kwanza la kumnunua winga wa Bayer Leverkusen mwenye umri wa miaka 24 Moussa Diaby. (Sky Sports Germany)

Villa pia wanavutiwa na winga wa Nottingham Forest na Wales Brennan Johnson, 22. (Mail)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Andre Onana

Manchester United wanakaribia kufikia makubaliano yenye thamani ya £43m, pamoja na nyongeza ya £4.3m kwa mlinda lango wa Inter Milan raia wa Cameroon Andre Onana, 27. (Fabrizio Romano).

Tottenham itampa mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane, 29, mkataba mpya wenye thamani ya zaidi ya £400,000 kwa wiki na kazi yake baada ya kuacha kucheza ili kumbakisha katika klabu hiyo, huku kukiwa na nia ya Bayern Munich. (Telegraph – Subscription Required)

Ofa za mchezaji wa Manchester United pamoja na pesa kwa mshambuliaji wa Denmark Rasmus Hojlund, 20, zimekataliwa na Atalanta, ambao wanataka malipo kamili ya pesa. (Athletic - Subscription Required)

Fulham wana matumaini ya kuwashinda vilabu vya Barcelona, Atletico Madrid, Arsenal na Liverpool hadi kufikia makubaliano ya kumnunua kiungo wa kati wa Fluminense na Brazil Andre Trindade, 21. (90min).

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Harry Kane

Nottingham Forest wako kwenye mazungumzo ya juu zaidi ya kumsajili kiungo wa kati wa Ivory Coast Ibrahim Sangare, 25, kwa mkataba wa pauni milioni 30 kutoka PSV Eindhoven. (Football Insider)

Kipa wa Liverpool na Jamhuri ya Ireland Caoimhin Kelleher, 24, ameonekana kulengwa na Wolves huku mlinda mlango wao Mreno Jose Sa, 30, akivutiwa na Forest. (Mail)

Beki wa Leeds na Denmark Rasmus Kristensen, 26, anatazamiwa kujiunga na Roma kwa mkopo wa msimu mzima. (Sky Sports)

Chelsea wamewasiliana na Lyon kuzungumzia mkataba wa majira ya joto kwa winga wa Ufaransa Rayan Cherki, 19. (90min).