Ajali ya ndege Ziwa Victoria: Ifahamu nguvu kazi iliyopotea
Na Yusuph Mazimu, BBC Swahili

Chanzo cha picha, MAELEZO
Tanzania inaomboleza vifo vya watu 19 waliofariki katika ajali ya ndege ya Precision Air iliyotokea Jumapili hii ya Novemba 06, 2022.
Ndege hiyo ATR 42-500 yenye namba PW 494 ilianguka kwenye ziwa Victoria mita chache kutoka uwanja wa ndege wa Bukoba, ikijiandaa kutua ikitokea.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amesema serikali itafanya uchunguzi kubaini chanzo hasa cha ajali hiyo, iliyoibua simanzi kwa watanzania. Na pengine itafahamika zaidi hasara na athari za ajili hiyo.
Pamoja na hayo, taifa hilo limepoteza wataalamu wengi na nguvu kazi muhimu, iliyokuwa ikitumika kutoa huduma na kuzalisha kwa manufaa ya taifa na watu wake.
Madaktari na watafiti katika sekta ya afya
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
Miezi 6 tu iliyopita (Aprili 16, 2022), Serikali ilitangaza ajira za watumishi wa sekta ya afya 1650, ili kupunguza uhaba wa watumishi katika sekta hiyo muhimu kwa maisha ya watu hasa eneo la tiba na utafiti.
Inaelezwa mahitaji halisi kutosheleza sekta ya afya hivi sasa ni watumishi 208,282 lakini waliopo hawafikii nusu ya hiyo hali ambayo inafanya kuwepo uhaba mkubwa wa watumishi hao hasa katika ngazi ya zahanati na vituo vya afya.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
Madaktari na watumishi wa sekta ya afya ni miongoni mwa waliofariki katika ajali hiyo. Menejimenti na Maendeleo ya Afya (MDH), yenye makao yake Mikocheni jijini Dar es Salaam inaweza kuwa imepata pigo zaidi kwa kupoteza watumishi wake watano kati ya nane waliokuwemo kwenye ndege hiyo.
Waliothibitika kufariki dunia ni Dokta Boniface Jullu , Dokta Neema Faraja na Dokta Alice Simwinga ambao ni watafiti, na Sauli Happymark pamoja na Mkuu wa kitengo cha mawasiliano MDH Zarcharia Mlacha. Watumishi wa MDH walionusurika ni Nickson Jackson, Dokta Josephine Mwakisambwe na Dokta Felix Otieno.
Atulinde Biteya alikuwa mtumishi wa NHIF Morogoro, kama alivyo ndugu yake yake Aneth Biteya naye ni miongoni mwa waliopoteza maisha katika ajali hiyo.
Mtumishi mwingine ajaye wa sekta hiyo angekuwa Hanifa Hamza ambaye ndiyo kwanza alikuwa amerejea nchini akitokea masomoni Uturuki, alikokuwa amehitimu masomo yake ya udaktari.
Mameneja na wakurugenzi
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 3
Imani Paul, alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Jambo for Development (JFD). Aliongoza shirika hilo na kutoa mchango mkubwa kwenye sekta mbalimbali ikiwemo elimu.
Alijiunga nalo mwaka 2014 na kwa muda sasa shirika hilo chini yake limeweza kufikia shule zaidi ya 800 magharibi mwa Tanzania na kusaidia wanafunzi zaidi ya 500 katika kuwaanda na elimu za maisha, ziwasaidia katika maisha yao ya baadae.
Ni pigo kwa familia ya shirika, lakini pigo kwa wanafunzi waliokuwa wanategemea mchango wake kwenye maisha yao.
Mbali na Imani, MDH pia imempoteza Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Zarcharia Mlacha huku Mamlaka ya dawa na vifaa tiba (TMD) imempoteza Mtani Njerenge ambaye alikuwa Meneja wa Pharmacovigilency ikielezwa ni miezi miwili iliyopita tu alipandishwa cheo hicho, akitokea kanda ya Ziwa (Mwanza)
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 4
Wataalam wengine

Chanzo cha picha, CHARLES MWEBEYA/TBC
Ukiacha wastaafu, Tanzania imepoteza pia wataalamu wengine muhimu katika ajali hiyo. Buruani Bubaga, alikuwa rubani akisaidiwa na Peter Odhiambo. Rubani huyu ni mmoja mwa warubani wazoefu waliodumu kwenye sekta ya usafrishaji wa anga kwa miaka karibu 20.
Aneth Biteya ambaye katika ajali hiyo alikuwa na nduguye Atulinde Biteya waliofariki wote, alikuwa mtaaalama wa masuala ya Tehama, akifanya kazi kitengo cha Tehama, (ICT) kwenye mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), mamlaka muhimu inayokusanya kodi kwa ajili ya maendeleo ya taifa hilo.
Wengine waliofariki katika ajali hiyo ni Lin Zhang, raia wa kigeni, Neema rafaja, Aneth Kaaya, Victor Laurean, Said Lyangama, Faraji Yusuph, Sauli Epimark, Eunice Ndirangu, Zacharia Mlacha na Zaituni Shillah.
Waziri mkuu Majaliwa leo ameongoza mamilioni ya watanzania kuaga miili ya marehemu hao katika uwanja wa Kaitaba Bukoba.