Uhusiano wa kimapenzi ulioanza kwa ujumbe wa facebook

.

Chanzo cha picha, Mohamed Kadawe

Maelezo ya picha, wapenzi

Mohamed Muhyadin Ahmed ni kijana aliyezaliwa na kukulia mjini Mogadishu. Miaka kumi iliyopita, alikuwa mwanachama wa Jeshi la Somalia na alijeruhiwa katika vita kati ya vikosi vya serikali na Al-Shabaab.

Mohamed, ambaye aliiambia BBC jinsi alivyohisi alipojeruhiwa, alisema: "Siku nilipojeruhiwa, nilipoteza kutembea, nilipoteza uelekeo, nilipoteza fahamu, nilipoteza kila kitu."

Mohamed na mkewe Hawa walifunga ndoa wiki iliyopita mjini Mogadishu.

Kabla ya kuoana, wenzi hao waliishi Somalia na Saudi Arabia kukiwa na umbali mrefu kati yao.

Jinsi walivyofahamiana

Mtandao wa kijamii wa Facebook umekuwa na jukumu muhimu katika uhusiano wao

Mapenzi ambayo yalianza kwa ujumbe wa Facebook yalileta mafanikio kwa ndoa yao. Mohamed, ambaye aliiambia BBC jinsi alivyokutana na mkewe Hawa na hofu yake walipokutana na wazazi wao, alisema:

“Mimi na mke wangu tulifahamiana kwenye mitandao ya kijamii hasa Facebook kwa kuwa nilikuwa mtu ambaye mara nyingi huwa sitembei wala kutoka nje ili kukwepa unyanyapaa ambao nimekuwa nikikutana nao kwenye jamii, tulizungumza kwa muda, tukakubaliana na baadaye tuliungana."

Hofu iliyowakabili Mohamed na Hawa, baada ya makubaliano ya ndoa yao

Walikabili shinikizo kutoka kwa wazazi walipofikiria jinsi ya kuwashirikisha katika jambo hilo.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Mohamed alisema kuwa yeye na mkewe waliogopa jinsi ya kuwakabili wazazi wa Hawa walipokubali kuoana.

“Kwa kuwa mimi ni mtu wa kutumia viti vya magurudumu, niliogopa nilipokwenda kwa familia ya Hawa kwamba wangekataa ndoa yetu, tulifikiria hata kutoroka pamoja, lakini kwa bahati nzuri wazazi wetu hawakukataa,” alisema.

Lakini Hawa Luul alisema kwamba mwanzoni alimshirikisha babake kuhusu makubaliano ya ndoa hiyo peke yake .

“Mimi na Mohamed tulipokubaliana kuhusu ndoa nilimshirikisha baba tu, akaniambia hakuna shida nakubali, muda wa mahari ulipofika akanilipia. " alisema Hawo, ambaye alimuombea baba yake.

Kando na tangazo la baba yake, Hawa alisema kuwa familia nzima haikushiriki suala la ndoa ya Mohamed kwani aliogopa kukatishwa tamaa.

Kwa upande mwingine, Haawo Luul, ambaye pia alitoa maelezo kuhusu kwa nini aliamua kwenda Mogadishu kwa sababu ya Mohamed, ambaye hajawahi kukutana naye, alisema:

"Baada ya kuelewana, niliamua kuelekea Mogadishu na kuacha kazi, kwa sababu Mohamed hakuweza kuja kwangu."

Harusi ya wanandoa hao ilisaidiwa sana na vijana wanaoishi mtaa mmoja na Mohamed. Alituambia kuwa alipoamua kuoa, hakuwa na pesa lakini marafiki zake wachanga walijitokeza kumsaidia na kumfanyia sherehe nzuri ya harusi.

Vikwazo anavyokumbana navyo katika jamii

Mohamed alisema kuwa baadhi ya watu wanamdhania kuwa ni ombaomba wanapoona gari lake likisukumwa.

“Watu wakiniona kwenye gari langu wanafikiri mimi ni ombaomba na kunipa pesa jambo ambalo linanifanya nisitoke mara kwa mara.” Kuna wakati hata niliiweka baiskeli yangu pembeni na niliona haina maana kuiendesha ni baada ya kuwa na matukio mengi ya ubaguzi katika jamii,” alisema.

Kwanini Mohamed alijiunga na jeshi?

.

Chanzo cha picha, Mohamed kadawe

Maelezo ya picha, Wapenzi

Katika mahojiano na BBC, Mohamed alisema kuwa alijiunga na jeshi la Somalia kusaidia familia yake maskini.

“Nilikuwa mvulana mdogo ambaye wazazi wangu wawili walitengana, na mama yangu alikuwa akifanya kazi, akilea mtoto mdogo. Kwa hivyo najiuliza ikiwa leo nina nguvu kidogo ninawezaje kusaidia familia yangu? Nilipoteza kazi yangu kama mfamasia na bawabu. Kwa hivyo niliamua kujiunga na Jeshi la Kitaifa la Somalia ili kupata mshahara mdogo na kuifanya nchi yangu kuwa salama ili watoto wetu waishi kwa amani katika siku zijazo," alisema.

Mohamed alisema kuwa hakupokea msaada wowote au usaidizi wa kimatibabu kutoka kwa serikali ya Somalia wakati alijeruhiwa. Lakini, watu pekee ambao hawajakata tamaa na kusimama kando yake walikuwa ni familia yake na masahaba.