Vita vya Ukraine: Washirika wa Magharibi wanaishiwa na silaha

WSDXA

Chanzo cha picha, REUTERS

Maelezo ya picha, Ukraine hurusha maelfu ya makombora kila siku katika vita vyake na Urusi

Mataifa yenye nguvu za kijeshi ya nchi za Magharibi yanaishiwa na silaha za kuipa Ukraine kujilinda dhidi ya uvamizi wa Urusi, Uingereza na Nato zimeonya.

Afisa mkuu wa Nato, Adm Rob Bauer aliliambia Baraza la Usalama la Warsaw kwamba silaha zimekuwa kidogo sasa.

Alisema serikali na watengenezaji wa silaha sasa walilazimika "kuongeza uzalishaji katika kiwango cha juu zaidi."

Ukraine inarusha maelfu ya makombora kila siku na mengi yao yanatoka Nato.

Afisa huyo, ambaye ni mwenyekiti wa Kamati ya Kijeshi ya Nato, alisema miongo kadhaa ya uwekezaji duni katika ulinzi unamaanisha kuwa nchi za Nato huipa Ukraine silaha kutoka katika ghala ambazo ni nusu au hazina tena kitu.

"Uchumi huria tulioujenga pamoja katika miaka 30 ni mzuri kwa mambo mengi - lakini sio katika eneo la vikosi vya kijeshi wakati kuna vita vinavyoendelea."

Waziri wa Ulinzi wa Uingereza James Heappey alieleza katika kongamano hilo kuwa hifadhi za kijeshi za Magharibi "zinaonekana kupungua" na kuwataka washirika wa Nato kutumia 2% ya utajiri wao wa kitaifa katika ulinzi.

"Ikiwa sio wakati wa kutumia 2% kwa ulinzi wakati Ulaya kuna vita, ni lini tutatumia?" aliuliza.

"Hatuwezi kuacha kusaidia Ukraine kwa sababu tu hifadhi zetu zinaonekana kupungua," Heappey alisema. "Lazima tuiwezeshe Ukraine kwa vita usiku wa leo na kesho na keshokutwa na keshokutwa. Na ikiwa tutasitisha, haimaanishi kwamba Putin ataacha vita."

"Ukweli ni kwamba sio kila nchi katika muungano anatumia 2% ya Pato lao la Taifa katika ulinzi. Hilo lazima liwe msingi wa matumizi yetu ya ulinzi."

Aliongeza: "Linapokuja suala la muungano, Marekani inazidi kuangalia mashariki na magharibi, na nadhani wenzetu katika Bunge la Marekani wanahitaji kuona mataifa yenye nguvu ya Ulaya yanatumia 2% ya rasilimali kwa ajili ya Nato."

sdc

Chanzo cha picha, EPA-EFE/REX/SHUTTERSTOCK

Maelezo ya picha, Siku ya Jumatatu, Mawaziri wa wa Umoja wa Ulaya walifanya mkutano wa kuzitaka nchi wanachama kuendelea kuunga mkono Ukraine
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Waziri wa Ulinzi wa Sweden, Pol Jonson alisema ni muhimu kwa Ulaya kuboresha ulinzi ili kuisaidia Ukraine kwa muda mrefu.

Wizara ya ulinzi ya Uingereza inasema tangu kuanza kwa uvamizi huo Februari 2022, Uingereza imetoa zaidi ya silaha 300,000 za mizinga na imejitolea kutoa "makumi ya maelfu zaidi" ifikapo mwisho wa mwaka. Wizara ya mambo ya nje ya Marekani inasema kuwa katika kipindi hicho hicho.

Huo ndio utegemezi wa Kyiv kwa silaha za Marekani na kuna wasiwasi miongoni mwa washirika wa Nato kuhusu uwezekano wa Donald Trump kuchaguliwa tena kuwa rais mwaka ujao.

Wanahofia uungaji mkono wa kijeshi wa Marekani kwa Ukraine huenda ukapungua ikiwa Trump atatafuta aina fulani ya suluhu la kisiasa na Moscow.

Ugumu ni kwamba licha ya majaribio ya kuongeza uzalishaji, Ukraine inatumia silaha kwa kasi zaidi kuliko mataifa ya Magharibi yanavyoweza kuzalisha.

Nchi za Nato na Umoja wa Ulaya zimekubaliana mipango mbalimbali ikiwemo mikataba ya pamoja na watengenezaji wa silaha, kutoa ruzuku kwa uzalishaji kadri wawezavyo.

Lakini inaonekana kwamba bado silaha ni kidogo kwa Ukraine.

Wachambuzi wanasema kinyume chake, Urusi inaonekana kuwa na uwezo zaidi wa kusimamia uchumi wake wakati wa vita ili kujaza akiba yake ya silaha.