Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Je, sindano ya kuongeza testosterone inaweza kusaidia kurejesha hamu ya ngono?
Miaka ya 1990, Alan Reeves alikuwa msanii, aliwatumbuiza maelfu ya watu akiwa katika kundi la wavulana la kuimba la The Dreamboys.
Alikuwa maarufu sana kiasi kwamba yeye na kundi lake la wacheza dansi wa kiume walionekana pia katika filamu ya Spice Girls, Spice World.
Wakati huo, alikuwa na umri wa miaka 24 na, kwa maneno yake mwenyewe, "nilikuwa na muonekano vizuri."
Lakini alipofika umri wa miaka ya 30, alijipata katika hali tofauti sana , nguvu zake za kisaikolojia zilipungua na hata hamu yake ya ngono ilipotea.
"Sikuwa na hisi vizuri," anasema.
Reeves, ambaye sasa ana miaka 52, anasema kupungua kwa hamu yake ya ngono kulianza kuwa na athari kubwa kwenye mahusiano yake.
"Ilipita miezi mitatu au minne kabla sijashiriki tendo la ndoa. Sikuwa na hamu kabisa," anasema. "Kitu kama hiki kinaweza kuwa sababu ya watu wawili kuachana."
Reeves, ambaye sasa ni kocha wa afya na mtindo wa maisha mini London, alianza matibabu ya kurejesha homoni ya testosterone, ambayo anasema imemrudishia hamu yake ya ngono, na kumfanya kutohisi kama "mzee mwenye hasira" hadi kuhisi kama kijana wa miaka ishirini. "Nahisi vizuri sana," anasema.
Wanawake pia wameanza kutumia homoni hii ya testosterone.
Rachel Mason, mwanablogu wa umri wa miaka 37 anayefuatilia masuala ya kukoma kwa hedhi au menopause, anasema homoni hiyo imekuwa msaada "wa ajabu" kwa kumpa nguvu,kumfanya kuwa makini, na kuimarisha mahusiano yake ya kimapenzi.
Utoaji wa dawa za kuongeza testosterone kumeongezeka.
Takwimu za hivi karibuni kutoka shirika la National Health Service Business Authority, zilizokusanywa na Care Quality Commission, zinaonyesha kuwa maagizo yanayotolewa yameongezeka kwa 135 % kati ya mwaka 2021 na 2024.
Kuongezeka kwa matumizi haya kunatokea wakati hamu ya ngono inapungua kote Uingereza. Idadi ya watu wanaofanya tendo la ndoa imekuwa ikipungua kwa hatua ndogo ndogo, kulingana na utafiti uliochapishwa na National Survey of Sexual Attitudes and Lifestyles (Natsal), ambayo huwauliza watu zaidi ya 10,000 kuhusu maisha yao ya kushiriki mapenzi.
Katika mwaka wa 1990, watu wenye umri wa miaka 16 hadi 44 waliripoti kufanya tendo la ndoa wastani ya mara tano kwa mwezi.
Kufikia mwaka 2000, idadi hiyo ilipungua hadi mara nne, na kufikia mwaka 2010, ilishuka hadi mara tatu. Watafiti wanatarajia kupungua zaidi kwa mara ambayo watu wanashiriki mapenzi. Lakini hawajatoa sababu moja maalumu ya kupunguka huo.
Je, kuongezeka kwa testosterone kweli kunaweza kuongeza hamu ya ngono, au sehemu kubwa ya umakini?
Kupungua kwa hamu ya tendo la ndoa
ngono ni mfano mmoja tu wa kuashiria kupungua kwa hamu hiyo miongoni mwa watu wengi.
"Kwa miaka mingi, tumeona kupungua kwa hamu ya ngono katika kila kundi la idadi ya watu," anasema Sosig Clifton, mkurugenzi wa utafiti wa Natsal.
"Idadi ya wanandoa wanaoishi pamoja sasa ni ndogo kuliko ilivyokuwa miaka ya 1990. Hii inaweza kusaidia kuelezea kupungua kwa hamu ya ngono. Lakini hata tulipokuwa tunazingatia kundi hilo kwa namna maalumu, pia kulikuwa na kupungua huko."
Kupungua kwa haraka zaidi kwa idadi ya watu wanaofanya tendo la ndoa kumeonekana zaidi kati ya wanandoa wazee, , au watu wanaoishi pamoja.
Clifton anasema ni vigumu kusema hasa kwa nini hamu ya ngono inapungua.
"Kulingana na takwimu tulizo nazo kwa sasa, hatuwezi kusema kwa uhakika ni sababu gani hasa inayosababisha idadi kubwa ya watu kufanya tendo la ndoa mara chache kuliko miaka iliyopita," anasema.
Licha ya ugumu huu, vituo vya treni, mabasi, na mitandao ya kijamii sasa vimejaa matangazo: "Hamu ya ngono imepungua? Kumbukumbu haziko wazi? Umelala sana? Ni wakati wa kufanya kipimo cha testosterone! Mumeo amepoteza hamu yake? Inaweza kuwa kutokana na homoni zake!"
Basi, je, matibabu ya kurejesha testosterone kweli yanaweza kutoa suluhisho kamili kwa tatizo la kupungua kwa hamu ya mapenzi?
Testosterone "imenirudishia maisha yangu"
Melissa Green amekuwa akitumia testosterone kwa takriban mwaka mmoja. Anasema haijamrudishia tu "msisimko wa maisha," bali pia imeokoa ndoa yake.
Mwanamke huyu wa miaka 43 anasema kwamba ukosefu wa hamu ya ngono ulikuwa ukileta athari kubwa kwenye mahusiano wao.
Daktari wake tayari alikuwa amempa estrogen na progesterone kupitia matibabu ya kurejesha homoni, kwa kuwa alikuwa katika hatua ya 'premenopause'. Lakini Green anasema daktari hakukagua viwango vyake vya testosterone, akisema homoni za ziada hazikuwa muhimu.
Miili ya wanawake hutoa kiasi kidogo cha testosterone, na miongozo ya National Health Service inasema kwamba testosterone inaweza kupewa wanawake wenye ambao hawana hamu ya mapenzi. Hii inaweza kuathiri wanawake wa umri wowote, lakini kwa kawaida huongezeka zaidi wakati wa kukoma kwa hedhi.
Mwishowe Green alikwenda katika kliniki binafsi na akaambiwa viwango vyake vilikuwa vya chini baada ya vipimo vya damu. Baada ya kurudisha matokeo hayo kwa daktari wake, sasa anapewa homoni ya testosterone.
"Imenirudishia maisha yangu. Wakati mwingine nahisi nikiwa na miaka ishirini," anasema. "Nina nguvu zaidi, naweza kufikiri kwa uwazi na nimepata tena hamu mapenzi."
Wakati baadhi ya watu wanashangilia homoni ya testosterone kuwaongezea hamu ya mapenzi, wengine wanasema pia imeleta athari zisizotarajiwa.
Cheryl O'Malley alitumia testosterone kwa mwaka mmoja. Anasema imeweza kumemsaidia kurejesha baadhi ya nguvu aliyoipoteza wakati wa kukoma kwa hedhi, lakini pia ilifanya hamu yake ya mapenzi kuongezeka sana na kumfanya kuwa mkali sana.
"Nilikuwa nah amu kubwa ya tendo la ndoa. Nilitaka kufanya mapenzi na mume wangu, na kwa wakati huo huo nilihisi namchukia."
"Ndipo nilipojua kwamba hii si nzuri, Sikuweza kujidhibiti."
Rachel Mason anasema kwamba alipokuwa akiandika kuhusu matibabu ya kurejesha testosterone kwenye mitandao ya kijamii, aligundua kuwa "Wanawake wengi wanaogopa kuanza kutumia testosterone. Wanaogopa wataonekana kama wanaume, watakua na nywele za uso na watapoteza utambulisho wao."
Pamoja na ongezeko la ukuaji wa nywele mwilini, matibabu ya kurejesha testosterone pia yanaweza kusababisha athari zingine. Kwa wanawake, athari zinazojitokeza mara kwa mara ni ukuaji wa nywele nyingi mwilini, chunusi, na kuongezeka kwa uzito, ambazo kwa kawaida zinaweza kurekebishwa kwa kupunguza au kuacha dozi hiyo. Kupoteza nywele (alopecia) na kuwa na sauti nzito ni nadra katika matibabu ya testosterone.
Kwa wanaume, athari zinaweza kujumuisha kuongezeka kwa uzito, hamu Zaidi ya mapenzi, kupoteza wa nywele kichwani na mabadiliko ya hisia.
Pia inaweza kupunguza uzalishaji wa manii na kuathiri uzazi. Kuna matibabu yanayoweza kusaidia hali hizi, lakini ni muhimu kutafuta ushauri wa daktari.
Ni njia rahisi ya kupata pesa.
Baadhi ya madaktari wa NHS na wanashauri wameiambia BBC kwamba kliniki binafsi zinapata faida kutokana na uuzaji wa dawa ya kurejesha testosterone kama suluhisho la haraka.
Dkt. Paula Briggs, mshauri wa National Health Service katika kitengo cha afya ya uzazi , anasema kuwa imekuwa njia ya kupata pesa kwa urahisi, ambapo watu lazima walipe pesa nyingi kwa kitu ambacho hawahitaji.
Kwa wanaume, viwango vya testosterone huanza kupungua kwa 1% kati ya umri wa miaka 30 na 40. Kulingana na National Health Service, hii ni sehemu ya kawaida ya mchakato wa kuzeeka na siyo jambo linaloweza kuathiri hamu ya ngono kwa kiwango kikubwa.
Kwa wanawake, viwango vya testosterone huanza kupungua kati ya umri wa miaka 20 na 40, na vinatulia karibu na kipindi cha kukoma hedhi. Kupungua kwa viwango hivi ni jambo la kawaida, ila swali ni, upungufu wa kiwango gani kunaweza kuaathiri hamu ya mapenzi na ustawi wa mtu kwa jumla.
Wakati matibabu ya kurejesha testosterone yanasaidia baadhi ya watu, ni wachache sana wanaosema wanahitaji testosterone ambao kweli wanapata faida kutokana nayo.
Kulingana na ushahidi wa kisayansi uliopo hadi sasa, matibabu ya kurejesha testosterone yanawanufaisha zaidi wanawake baada ya kukoma kwa hedhi na wanawake wenye hamu ya chini ya mapenzi.