Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Wafahamu viongozi wakuu wa Iran waliouawa katika shambulio la Marekani ikishirikiana na Israel
Mashambulizi yaliyotekelezwa na Israel na Marekani dhidi ya Iran, yameleta ugomvi mpya Mashariki ya Kati, ugomvi ambao rais wa Marekani Donald Trump anasema "ni wa kumaliza tishio la usalama dhidi ya Washington na kuwapa raia wa Iran nafasi ya kufanya mapinduzi"
Katika orodha ya waliolengwa katika shambulio la kwanza walikuwa viongozi wa serikali ya Iran.
Miongoni mwa waliouawa ni kiongozi wa kidini Ali Khamenei.
Mashambulizi hayo pia yalisababisha vifo vya watu maaurufu ikiwemo viongozi wa kisiasa na kijeshi.
Jeshi la Israel lilisema liliwauwa viongozi wakuu 40 wa jeshi la Iran.
Wafuatao ni viongozi wakuu wa Iran waliotangazwa kuuawa na oparesheni ya kijeshi iliyotekelezwa nchini humo.
Aziz Nasirzadeh – Waziri wa ulinzi wa Iran
Aziz Nasirzadeh alizaliwa katika mji wa Sarab, mashariki mwa mji wa Azerbaijan, kaskazini magharibi mwa Iran mwaka 1964.
Baada ya kufuzu kama rubani, alifanya masomo mengine nje ya Iran kama kuendesha ndege za kivita nchini Pakistan.
Alikuwa miongoni mwa marubani waliokuwa wakitumia ndege za F-14, katika vita vya Iraq na Iran, kati ya mwaka 1980 hadi 1988.
Baada ya kumalizika kwa vita Nasserzadeh, alishikilia nafasi za uongozi nje na ndani ya Iran. Alihudumu katika ubalozi wa Rome nchini Italia, kabla ya kurejea nchini Iran na kuhudumu katika kitengo cha vita katika jeshi la Iran.
Alichaguliwa kuwa naibu kamanda ya jeshi la anga kabla kuwa mkuu wa wafanyikazi wa jeshi kati ya mwaka 2009 hadi 2017.
Baada ya ushindi wa rais Masoud Pezeshkian's mwaka wa 2024, Nasirzadeh, alichaguliwa kuwa waziri wa ulinzi wa Iran.
Ali Shamkhani – Katibu wa baraza kuu la Ulinzi
Shirika la habari kitaifa la Iran, limedhibitisha kifo cha Ali Shamkhani, mshauri wa kiongozi wa kidini Ali Khamenei, katika mashambulizi yaliyotekelezwa na Marekani.
Shamkhani alizaliwa mwaka 1955, eneo la Ahvaz, ni muarabu wa Iran kutoka Khuzestan. Alihusika na mageuzi ya kisiasa dhidi ya utawala wa Shah na baadaye kukamatwa.
In 1975, alianzisha kundi la "Mansouroun" na Mohsen Rezaei ambayo baadaye ilikuja kuwa kitovu cha Revolutionary Guard.
Miezi minane iliyopita, kulikuwa na uvumi kuwa ameuawa katika mapigano ya awali ya Iran na Israel, ila siku kadhaa baadaye iliripotiwa kuwa amejeruhiwa na alinusurika mashambulio hayo.
Hakuonekana kwa umma kwa muda, hadi alipoonekana katika mazishi ya makamanda wa Revolutionary Guard.
Baada ya vita hivyo alichaguliwa kuwa katibu na mwakilishi wa kiongozi wa kidini Ali Khamenei katika baraza kuu la ulinzi.
Mohammad Pakpour – Kamanda wa Revolutionary Guard
Shirika la habari la Iran lilidhibitisha kifo cha Meja Jenerali Mohammad Pakpour, kamanda wa Revolutionary Guard.
Katika siku ya kwanza ya duru iliyotangulia ya kuongezeka kwa mapigano, iliyojulikana kama "Vita vya Siku Kumi na Mbili," na baada ya kuuawa kwa Hossein Salami, uamuzi ulifanywa kumpandisha cheo Mohammad Pakpour kutoka brigedia jenerali hadi meja jenerali, na kumteua kuwa kamanda mkuu wa Revolutionary Guard.
Katika miezi minane aliyokuwa akiongoza Revolutionary Guard,alisisitiza mara kwa mara juu ya utayari wa vita, uwezo wao wa makombora, na kutoa vitisho vya moja kwa moja dhidi ya Marekani na Israel.
Pakpour alisisitiza kwamba Iran ilikuwa imefikia kilele cha uwezo wake wa kijeshi na shambulio lolote jipya lingekabiliwa na jibu kali na lenye nguvu zaidi. Alionya kwamba ikiwa vitisho vingeendelea, Iran ingeanzisha tena vita "kutoka vilipoishia" na isingeruhusu washambuliaji kuepuka bila kuadhibiwa.
Katika hotuba zake na barua rasmi, alisisitiza maendeleo ya teknolojia ya kijeshi, ikiwa ni pamoja na uwezo wa makombora na matumizi ya teknolojia za kisasa katika vita.
Mohammad Pakpour, aliyezaliwa mwaka 1961 katika mji wa Arak, alikuwa kamanda mkongwe katika Revolutionary Guard. Kabla ya kuteuliwa kuwa kamanda mkuu wa Revolutionary Guard, aliongoza vikosi vya ardhini kwa muda wa miaka 16.
Abdul Rahim Mousavi- Mkuu wa wanajeshi wa jeshi la Iran
Meja Jenerali Abdul Rahim Mousavi, mkuu wa wanajeshi wa Jeshi la Iran, aliuawa katika mashambulizi ya Marekani na Israel ambayo yanaaminika kuwalenga viongozi wa juu wa Iran na makamanda wa kijeshi.
Mousavi alizaliwa mwaka 1959 katika mji wa Qom na anachukuliwa kuwa mmoja wa viongozi mashuhuri zaidi wa jeshi la Iran. Kuteuliwa kwake kuwa Mkuu wa Majeshi wa Vikosi vya Ulinzi kulikuwa hatua ya mabadiliko katika muundo wa uongozi wa kijeshi, baada nafasi hiyo kushikiliwa kwa muda mrefu na kamanda wa Revolutionary Guard.
Mousavi alijiunga na jeshi mwaka wa 1979, ambapo alisoma katika Chuo cha maafisa wa vikosi vya ardhini. Ana shahada ya uzamivu katika usimamizi wa ulinzi kutoka Chuo Kikuu cha Supreme National Defense University.
Wakati wa Vita vya Iran na Iraq, alihudumu katika kikosi cha mizinga akiwa mstari wa mbele wa vita eneo la Kurdistan na Khuzestan, alishiriki katika operesheni muhimu na kujeruhiwa wakati wa mapigano.
Baada ya vita kumalizika alipandishwa cheo.
Alihudumu kama mwenyekiti wa wakuu wa majeshi kati ya mwaka 2005 na 2008, kisha akawa naibu kamanda Mkuu wa Jeshi hadi mwaka 2015. Mwaka 2016, alichukua wadhfa wa naibu mkuu wa majeshi ya Ulinzi.
Baadaye alipandishwa cheo hadi kuwa Meja Jenerali na kuteuliwa kuwa Kamanda mkuu wa Jeshi mwaka 2017, nafasi aliyoishikilia hadi mwezi Juni 2025.
Imetafsiriwa na Beldeen Waliaula