Barabara juu ya Bahari:Ifahamu barabara kuu ya Marekani 'inayoelea'

Chanzo cha picha, Alamy
Ikiwa na urefu wa maili 113 kwenye bahari ya wazi, uhandisi huu wa kiajabu uliunganisha eneo la Florida Keys na eneo la bara na ilibadilisha Florida milele.
Shakwe walilia juu juu nilipokuwa nikiteleza kwenye maili ya maji yenye kumeta-meta mahali fulani kati ya Bahari ya Atlantiki na Ghuba ya Mexico. Anga iliyeyuka na kuwa bahari ya rangi ya samawati , ilipozama ndani ya mifereji kati ya visiwa vya matumbawe na chokaa. Ilikuwa kama meza ya bluu, ikienda mbali zaidi ya nilivyoweza kuona .
Nilipokuwa nikirekebisha miwani yangu ya jua, niliona kitu kikisonga majini kutoka kwenye kona ya jicho langu. Pomboo wa chupa! Alikuwa na marafiki, na punde walifanya dansi ya majini, wakirukaruka katika safu za kupendeza kabla ya kutumbukia tena kwenye mawimbi. Boti za uvuvi zilinizunguka na nilikuwa na hamu ya kutupa chambo cha kuvua samaki baharini lakini ingekuwa vigumu kufanya hivyo wakati nikindesha gari kwa 50mph kando ya barabara kuu.
Kusafiri kutoka Miami hadi kisiwa cha Key West, Florida, kumekuwa safari ya kutojali kila wakati. Katika sehemu kabla ya Karne ya 20, njia pekee ya kufanya safari hadi sehemu ya kusini kabisa katika bara la Marekani ilikuwa ni safari ya siku nzima ya mashua, na hiyo ilitegemea hali ya hewa na mawimbi.
Lakini kutokana na uhandisi wa ajabu unaojulikana kama Barabara Kuu Juu ya bahari ambayo ina urefu wa maili 113 kutoka ncha ya kusini ya bara kuvuka visiwa 44 vya tropiki kwenye madaraja 42, nilionekana nikielea kwenye mkufu wa misitu ya mikoko na mashimo nilipokuwa nikisafiri hadi mahali ambapo Amerika Kaskazini na Caribbean zinakutana.

Chanzo cha picha, Robert Zehetmayer/Alamy
Barabara Kuu ya Ng'ambo kwa hakika ilianza kama Reli ya Juu ya Bahari , na ilikuwa ni wazo la msyawishaji maarufu Henry Morrison Flagler (anayejulikana kama "Baba wa Florida ya Kisasa"). Mnamo 1870, Flagler alianzisha Kampuni ya Mafuta ya Standard Oil pamoja na mfanyabiashara mkubwa John D Rockefeller, na ikawa moja ya mashirika makubwa na yenye nguvu zaidi ulimwenguni mwanzoni mwa Karne ya 20. Baada ya kutembelea Florida na kutambua uwezekano wa utalii wa jimbo hilo lililopewa jina la "The Sunshine State", Flagler akamwaga utajiri wake mwingi katika eneo hilo, akijenga hoteli za kifahari ambazo zilibadilisha mojawapo ya majimbo maskini zaidi ya Marekani kuwa paradiso ya majira ya baridi kwa wasafiri na watalii kutoka Kaskazini-Mashariki mwa Marekani. Hata hivyo, hapakuwa na njia kwa wageni kufika kwenye hoteli za kifahari za Flagler zilizokuwa mbali .
Kwa hivyo mnamo 1885, Flagler aliunganisha safu ya reli zilizotengana kando ya Pwani ya Atlantiki ya Florida kutoka Jacksonville, mwisho wa kaskazini wa Florida, hadi Miami, karibu na ncha ya kusini ya jimbo hilo.
Miami ilipaswa kuwa mwisho wa njia hiyo, lakini wakati Marekani ilipoanza ujenzi kwenye Mfereji wa Panama mwaka wa 1904, Flagler aliona uwezekano mkubwa wa Key West - sehemu ya karibu zaidi ya ardhi ya Marekani na Mfereji huo na bandari ya kina kabisa Kusini-mashariki mwa Marekani. Kitovu chenye shughuli nyingi kilikuwa tayari kinashamiri kutokana na viwanda vya sigara, na uvuvi (Key West lilikuwa jiji kubwa la Florida hadi 1900), lakini eneo la mbali la kisiwa lilifanya iwe vigumu na ghali kusafirisha bidhaa kaskazini.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Kwa hiyo, Flagler aliamua kupanua njia yake maili 156 kusini hadi Key West, hasa juu ya bahari ya wazi. Kinachojulikana kama Upanuzi wa Key West ulionekana kuwa hauwezekani na watu wengi wa wakati wake, na maono yake yaliitwa "Flagler's Folly" au 'Kasoro ya Flagler' na wakosoaji wake. Kati ya 1905 na 1912, vimbunga vitatu vilipiga eneo la ujenzi, na kuua wafanyakazi zaidi ya 100. Bila kukata tamaa, Flagler akasonga mbele. Ilichukua miaka saba; $50m ($1.56bn leo); na wahamiaji 4,000 Waamerika, Bahama na Wazungu kujenga reli - ambao wote walilazimika kushindana na mamba, nge na nyoka walipokuwa wakifanya kazi katika mazingira magumu .
Wakati reli hiyo ilipokamilika mnamo 1912, iliitwa " Kioja cha nane cha ulimwengu ". Katika uzinduzi wa treni hiyo, treni iliyokuwa ikitumia kuni ilifika Key West kutoka Miami ikiwa imembeba Flagler mwenye umri wa miaka 82, ambaye alitoka kwenye behewa lake la kibinafsi la kifahari (ambalo linapatikana kwenye Jumba la Makumbusho la Flagler huko Palm Beach ) na inadaiwa alimnong'oneza rafiki yake, "Sasa naweza kufa kwa furaha. Ndoto yangu imetimia."

Chanzo cha picha, Florida Memory/Alamy
"Ukweli kwamba Flagler alifadhili [zaidi ya $ 30m ya mradi huu ] kutoka kwa mfuko wake siku hiyo ilikuwa ya kushangaza," mwanahistoria wa Florida Brad Bertelli alisema. "Jeff Bezos au Bill Gates wanaweza kufanya hivyo leo. Elon Musk na SpaceX yake inaweza kuwa ulinganisho bora zaidi wa kisasa."
Reli hiyo ilifanya kazi hadi 1935, wakati tufani mbaya zaidi katika karne ilisomba maili ya reli. Badala ya kujengwa upya, kazi bora ya Flagler ilizaliwa upya ili kushughulikia upendo mpya wa Wamarekani wa magari. Mnamo mwaka wa 1938, serikali ya Marekani iliazimia kujenga mojawapo ya barabara ndefu zaidi za maji duniani kwa kutegemea madaraja ya Flagler yanayoonekana kutoweza kuharibika, ambayo yangeweza kustahimili upepo wa 200mph. Wafanyakazi waliweka lami juu ya reli ili kubeba magari, na Barabara Kuu mpya ya Ng'ambo iliyofunguliwa hivi karibuni ilibadilisha kisiwa cha Keys cha Florida kuwa kivutio kizuri cha watalii walipo leo.
Zaidi ya karne moja baada ya reli kukamilika, madaraja 20 ya awali bado yanabeba wasafiri kutoka Miami hadi Key West. Unaweza kutumia gari kwa chini ya saa nne, lakini kupotoka njiani ni sehemu ya kufurahisha. Msururu wa vituo vya kuvutia, vilivyo chini ya rada huwasaidia wasafiri kufahamu vyema jinsi maajabu haya ya kiuhandisi yalivyotokea, na athari yake ya kudumu kwa Florida Keys.
Maili sitini na tisa kusini mwa Miami, Key Largo ndio sehemu ya kaskazini kabisa ya Florida Keys na kituo kikuu cha kwanza. Mamba,Nyoka na wanyama wengine wengine wa majini wanaweza kuwa na hofu kwa wafanyakazi wa ujenzi wa Flagler, lakini siku hizi, wasafiri wanakuja Key Largo ili kustaajabia maisha yake mengi ya baharini. Hifadhi ya Kitaifa ya Baharini ya Florida Keys inayopakana na Mbuga ya Jimbo la John Pennekamp Coral Reef inawavutia wapiga-mbizi na wapiga mbizi wanaotamani kujitumbukiza kwenye miamba ya matumbawe pekee hai ya Amerika Kaskazini.

Chanzo cha picha, Jeffrey Isaac Greenberg 8+/Alamy












