Uvimbe wa kudumu: Hali ya inayoweza kuathiri vibaya afya yako

w

Chanzo cha picha, Getty Image

Maelezo ya picha, Uvimbe (Inflammation) wa kudumu mwilini unaweza kusababisha magonjwa katika mfumo wa usambazaji wa wa damu kwenye ubongo

Kwa kawaida wakati maambukizi, jeraha au sumu huonekana, kwa ujumla kitu hatari ambacho kinaweza kudhuru mwili wako, uchochezi hutokea kama mchakato katika mwili wako wa kupigana na magonjwa haya, kama njia ya mwili kujiponya yenyewe.

Katika mchakato huu, mwili hutoa kemikali kama vile kingamwili au protini na kuongezeka kwa mtiririko wa damu kwenye eneo lililoharibiwa, jambo ambalo huchochea mwitikio wa utendaji wa mfumo wako wa kinga ya mwili.

"Ni pale ambapo mwitikio mzima wa kinga unapofanya kazi vyema, ambapo kiumbe huweza kuelewa wazi kuwa kuna uvimbe," anasema Mario López Hoyos, rais wa Chama cha Kinga cha Kihispania.

Hivi ndivyo inavyotokea tunapojikata, kwa mfano. Eneo lililoathiriwa mara moja huwashwa, hugeika rangi nyeundu na tunahisi uchungu, na kisha hatua kwa hatua huchukuliwa na mwili wetu mpaka unapojiponya wenyewe.

Na mwitikio huu wa mwili wa haraka na wa muda mfupi katika kujiponya, ni mfano wa uvimbe (Inflammation) usio na madhara makubwa mwilini

Kusudi ni kuulinda mwili, kuondoa vijidudu vinavyovamia ambavyo vinaweza kuwa na madhara, anaeleza Dk. Diana Alecsandru, mkurugenzi wa Kinga na Kushindwa kwa Uzazi katika IVI (Taasisi ya Infertility, Hispania).

Kwa hiyo, kwa ushirikiano kati ya vipengele mbalimbali vya seli, mfumo wetu unatahadharishwa, kwa mfano na homa ya mafua, na sababu inayofanya uharibifu huondolewa.

Lakini, kama ilivyo kwa inzi, ziada ya majibu haya kutoka kwa mfumo wetu wa kinga inaweza kuwa mbaya.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kuvimba, hivyo manufaa kwa mwili, yanaweza kuwa na athari hasi

Wakati mwili wako uko katika tahadhari ya mara kwa mara

Lakini inaweza kutokea kwamba mfumo wetu wa kinga ukaendelea kutoa tahadhari na, kwa hiyo, majibu kwa kile unachokiona kuwa ya ajabu. Ni kana kwamba unaendelea kugundua uwepo wa mvamizi ambaye hayupo tena.

"Unaendelea kuangazia mfumo wa kinga na unaendelea kufanya kazi dhidi ya mwili. Inaweza kutokea kwetu, kwa mfano, katika moyo , "anasema Alecsandru.

Ikiwa tuna uvimbe mwilini (inflammation) kwa muda mrefu , inaweza kuwa hatari, kwa sababu uvimbe huu unahusishwa na kupoteza kazi ya michakato mingi ya kisaikolojia na kiakili.

Uvimbe wa muda mrefu usiodhibitiwa utakuza aina zote za magonjwa, maambukizo sugu kama saratani, mizio na magonjwa mengine kama vile pumu na ukosefu wa kinga ya mwili," anasema López Hoyos.

Pia, wataalam wote wawili wanatoa maoni, magonjwa kama vile kuharibika kwa mimba, kuathiriwa kwa mfuko wa uzazi au kuharibika kwa kiinitete.

Mnamo mwaka wa 2018, jarida la Nature lilichapisha utafiti ambao ulionyesha kuwa zaidi ya 50% ya vifo vyote ulimwenguni vinatokana na magonjwa yanayohusiana na uchochezi: kuanzia ugonjwa wa moyo wa ischemic, ambo hutokea wakati mishipa inayosambaza damu kwenye misuli ya moyo inakuwa imeziba, saratani, kisukari, na magonjwa mengine ya ukosefu wa kinga mwilini.

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Kwa nini kuvimba mwilini (Inflammation) hutokea kwa muda mrefu?

Kuvimba kunaweza kuendelea kwa sababu maambukizi au jeraha halijapona vizuri, kwa mfano.

Jambo jingine ambalo linaweza kusababisha uvimbe ni wakati una ugonjwa wa autoimmune, ambapo mfumo wa kinga hushambulia vibaya tishu zenye afya au mfumo wam wili kwa ujumla.

Huweza pia kusababishwa na hewa chafu au kemikali za viwandani.

Na kwa mabadiliko ya maisha ya ubinadamu katika miaka 50 iliyopita.

‘’ Tunakula vyakula vilivyosindikwa zaidi, vitu vingi ambavyo ni vibaya kwa afya yetu. Na hivyo uwiano kati ya bakteria wazuri na bakteria nyemelezi hukosekana", anasema Dkt . Alecsandru.

‘’Kulala muda mfupi , kuwa na mafadhaiko, mkubwa pia hupunguza sana mwitikio wa kinga, kuvuta sigara, kunywa pombe, kula vibaya na mafuta yaliyojaa, na ukosefu wa vitamini D itokanayo na jua huathiri utendaji mzima wa mwili na kusababisha uvimbe mwilini (inflammation)’’, anasema.

Kwa hiyo, maambukizi yanaonekana kwenye kiwango cha pelvic, na mkojo

Na hii hatimaye ina athari kwa afya yetu kwa ujumla: "Inaathiri damu yetu, kwa kiwango cha neva ... Kila kitu," anasema Alecsandru.

Je ni dalili zipi?

López Hoyos anadokeza kuwa uvimbe wote, kulingana na vigezo vya kitabibu vya kawaida, hugunduliwa kwa njia nne: maumivu, uvimbe, kutokwa na maji, na kushindwa kufanya kazi.

Kwa Dk Alescsandru, dalili za kuvimba kwa muda mrefu kwa kiwango cha chini cha uvimbe ni jambo la kawaida sana kiasi kwamba mara nyingine hata hatujui , "tumezoea kuhisi: kuwa na hali ya uchovu wa muda mrefu, udhaifu, maambukizi ya mara kwa mara, baridi ya mara kwa mara ".

Njia nyingine ya kuona kwamba kuna kuvimba ni wakati tunapokuwa na matatizo ya ngozi ya mara kwa mara kama vile eczema au psoriasis hutokea. "Ngozi ni kiungo kikubwa zaidi, kuna seli nyingi za kinga chini ya ngozi na hii ni kiashiria cha kwanza cha kuwa tatizo mwilini," anasema.

Mfumo wetu wa utumbo kwa ujumla unaweza pia kutuambia kuhusu iwapo kuvimba. Iwapo kuna vidonda mdomoni, mmeng'enyo mzito wa chakula, matatizo ya kumeza chakula vizuri, kujaa gesi tumboni, kupata haja kubwa zaidi au kupata shida kuwa nayo, tumbo kulegea hata baada ya kula kitu kidogo , au maumivu ya tumbo inaweza kuwa dalili nyingine ya uvimbe (Inflammation) mwilini.

Dalili zingine zinaweza kuwa shida ya kulala au wasiwasi.

Lakini bila shaka, Alecsandru anasisitiza, maambukizo ya mara kwa mara ni kiashiria wazi kwamba kuna kuvimba kwa muda mrefu.

“Mfumo wa kinga unafanya kazi ya kurekebisha, lakini ikiwa haufanyi chochote isipokuwa kurekebisha na kurekebisha kila wakati, unachoka na haufanyi kazi vizuri .

K

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kupata haja kubwa mara nyingi au mara chache inaweza kuwa kiashiria cha kuwa na uvimbe mwilini (Inflammation)

Jinsi ya kuepuka

Ni rahisi. Ikiwa kinachoweza kusababisha uvimbe huu wa muda mrefu ni tabia mbaya ya maisha, njia ya kuzuia ni kuacha kabisa tabia hizi.

Hii ni pamoja na kupata usingizi mzuri wa usiku, kutokuwa na msongo wa mawazo, na kufanya mazoezi. Lakini, katika kisa cha mwisho, wataalam walishauriana kuzungumza juu ya kufanya mazoezi ya wastani na ya kuendelea, kwa sababu ikiwa yatakuwa makali sana pia yanaweza kusababisha uvimbe (inflammation)

Na Alecsandru anaonyesha kuwa ni bora ikiwa tunaweza kufanya shughuli fulani katika mazingira ya asili na sio katika jiji, ambapo kuna mazingira mazingira ambayo huweza kusababisha uvimbe.

Inahitajika pia kuzuia athari za mawakala wa mazingira wa nje ambazo huamsha utendaji wa kinga ya mwili kwa urahisi, kama vile uvutaji wa tumbaku.

Lakini ikiwa tayari una kuvimba kwa muda mrefu, kuna njia ya kuuzuia?

“Kama umeshaanza ni shida, maana tayari umeshawasha moto na ulichonacho," anasema López Hoyos, ambaye anabainisha kuwa jambo la kwanza, karibu kila mara, ni kupunguza uzito na kuboresha mtindo wa maisha.

Ikiwa tunaona kwamba kila wakati "tunakula chakula kibaya zaidi, itakuwa vizuri kushauriana na mtaalamu wa lishe na kwa mabadiliko rahisi, kama vile kula baadhi ya vyakula na sio vingine, kuchukua antioxidants, kinga au probiotics, tunaweza kuboresha afya zetu," anasema. Alecsandru.

Na zaidi ya yote, ni lazima tusikilize na kuona miili yetu, kwa sababu kama Dk. Alecsandru asemavyo, "ni kitabu kilicho wazi, kinatupa ishara kila mahali. Mwili wetu unapotuambia jambo mara nyingi, lazima tuzingatie. hilo".