Urusi: Jinsi wasiojulikana walipo katika mkoa wa Kursk wanavyotafutwa kisiri

fgvb

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Baada ya kutekwa kwa Sudzha na jeshi la Ukraine, watu wapweke na wazee walibaki katika mji huo
    • Author, Elizaveta Fokht & Andrey Kozenko
    • Nafasi, BBC
  • Muda wa kusoma: Dakika 4

Zaidi ya watu laki moja wamehamishwa kutoka maeneo yanayokaliwa na Ukraine katika mkoa wa Kursk. Lakini wengine elfu mbili hawajuulikani walipo, jamaa zao na timu za utafutaji za Shirika la Msalaba Mwekundu la Urusi zinawanawatafuta.

Hapa tunazungumzia juu ya wazee ambao hawakuweza kuhama peke yao. Kuwapata ni vigumu sana. Mawasiliano ya simu katika maeneo yanayokaliwa na Wanajeshi wa Ukraine hayafanyi kazi.

Krill na Mama yake

Mara tu baada ya uvamizi wa jeshi la Ukraine, kwenye mpaka wa mkoa wa Kursk usiku wa Agosti 5-6, jumbe za kwanza zilionekana kwenye mitandao ya kijamii za watu wanaotafuta watu wao - raia na wanajeshi walio karibu na mpaka.

Kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa uvamizi wa Ukraine, Warusi wamejikuta katika hali sawa na raia wengi wa Ukraine katika kipindi cha wiki mbili zilizopita. Hakuna habari za kuaminika kuhusu waliokufa na raia waliojeruhiwa na wanajeshi wa pande zote mbili.

Katika siku chache zilizopita, BBC imewasiliana na watu huko Urusi ambao wanatafuta wapendwa wao katika eneo la Kursk. Wengi wao hawakujibu ujumbe au walikataa kuzungumza na waandishi wa habari kwa kuhofia hatima ya ndugu ambao wako kwenye eneo lililo chini ya udhibiti wa Ukraine.

Lakini mkazi mmoja wa eneo hilo, Kirill (BBC imelibadilisha jina lake), alikubali kueleza kilichotokea kwake.

Asubuhi ya Agosti 6, Kirill, mkazi wa Lgov, mji mdogo katika mkoa wa Kursk, aliingia kwenye gari na kuelekea Sudzha kumchukua mama yake mwenye umri wa miaka 78 (umbali wa kilomita 100). Tangu jioni ya siku moja kabla, umeme na maji vilikatika huko Sudzha, wakati mapigano yanakaribia. Kufikia asubuhi hakukuwa na mawasiliano tena. Mama yake Kirill na marafiki zake wengine walikaa usiku kucha kwenye handaki.

Lakini mama yake Kirill alikataa kabisa kuondoka Sudzha mara baada ya Kirill kuondoka - aliamini "jeshi letu litakuja kutusaidia."

Kirill "alikata tamaa" na kuanza kuchukua majirani. Kwa jumla, Agosti 6, Kirill alisafiri kutoka Lgov hadi Sudzha na kurudi mara tatu. Wakati wa moja ya safari hizi, mbele ya macho yake, kombora lilipiga nyumba.

Kufikia jioni, Wanajeshi wa Ukraine walikuwa wamefika Zaoleshenka, kijiji ambacho barabara kati ya Lgov na Sudzha inapita. Jeshi la Urusi lilifunga barabara, na kufika Sudzha kuliwezekana tu kupitia barabara za vijijini na shambani.

Kirill aliamua kurudi kumfuata mama yake. Anakumbuka katika masaa hayo vyombo vya habari vya Urusi vilianza kuandika juu ya kifo cha mwanamke mjamzito, mkazi wa eneo hilo.

gh

Chanzo cha picha, Reuters

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Akiwa njiani kuelekea Sudzha, Kirill aliona ndege isiyo na rubani ya Ukraine angani. Aligundua kuwa hawezi kwenda mbali zaidi.

Kufikia wakati huo, ikawa wazi kuwa jeshi la Ukraine lilikuwa tayari linachukua mji wa Sudzha. Baadaye, marafiki wa Kirill kutoka vyombo vya usalama walimshauri asijaribu kumuokoa mama yake, kwa kuzingatia ukweli kwamba yeye mwenyewe alishiriki katika uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Kirill alirudi Lgov bila mama yake. Agosti 9, viongozi walianza kuwahamisha wakazi, na Kirill mwenyewe pia aliishia kuhamishwa huko Vologda. "Nilipoteza kila kitu: nyumba, hati, pesa. Nilibaki na shati na kaptula,” anasema.

Tangu Agosti 6, hajajua chochote kuhusu hatima ya mama yake. Kirill anajua juu ya kile kinachotokea katika jiji hilo kupitia chaneli za telegramu. Anasema alisoma kwamba wapiganaji wa Ukraine wanatoa msaada wa kibinadamu kwa wakazi wa eneo hilo, na waliojeruhiwa wanapelekwa hospitalini huko Sumy.

“Hakuna aliyemuona mama yangu. Nina hofu, anaweza kufa njaa. Na mimi pekee ndiye ninayepaswa kulaumiwa kwa hili, "anasema Kirill. "Laiti ningejua hili lingetokea, ningemchukua kwa nguvu."

Kulingana na Kirill, wale ambao wamepoteza wapendwa wao wanashauriwa na mamlaka kusubiri tu. Yeye mwenyewe aliwasilisha ombi la kumtafuta mama yake kwa Shirika la Msalaba Mwekundu la Urusi (RKK).

Mbinu za kutafuta wapendwa

gfhb

Chanzo cha picha, Getty Images

Katika mazungumzo na BBC, katibu wa vyombo vya habari, Evgenia Erokhina, alisema wamezindua simu ya saa 24 "kurejesha uhusiano wa kifamilia" kwa wakazi wa mkoa wa Kursk. Wale wote ambao wamepoteza mawasiliano na jamaa zao wanampigia simu. Tangu Agosti 11, zaidi ya watu elfu 4 wametuma maombi kwake.

Baada ya kupokea ombi hilo, wataalamu huituma kwa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu - huko wanakusanya maombi kutoka kote kwenye hifadhidata moja ili kutafuta taarifa zinazofanana.

Lakini Kirill, bado anauliza maswali. “Hapa kuna Wizara ya Ulinzi. Kwa nini hawakuona mkusanyiko mkubwa wa Wanajeshi wa Ukraine karibu na mpaka? Kwa nini hawakuchukua hatua?

Kutafuta watu hakika haitakuwa kazi rahisi katika siku zijazo; kwani vikosi vya usalama vinawataka wakazi wa eneo hilo kupunguza matumizi yao ya mitandao ili kujilinda.

Imetafsiriwa na Rashid Abdallah na kuhariwa na Ambia Hirsi