Real Madrid v Chelsea: Nguvu na mahitaji - kwa nini Los Blancos ni wababe wa Ligi ya Mabingwa

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wachezaji wa Real Madrid

Zimesalia mechi tano pekee - mechi tatu – nzio zilizopo kati ya Real Madrid na taji lao la sita la Ligi ya Mabingwa katika kipindi cha miaka 10 iliyopita.

Iwapo watafanikiwa kuwaondoa Chelsea ambao hawachezi vyema, watakaofuata watakuwa Bayern Munich au Manchester City katika nusu fainali.

Kwa ndani, vijana hao wa Carlo Ancelotti wako pointi 13 nyuma ya vinara wa La Liga Barcelona, lakini ushindi wa hivi majuzi wa mabao 4-0 dhidi ya wapinzani wao hao kumewasaidia kutinga fainali ya Copa del Rey dhidi ya Osasuna na kutoa onyo kwa Ulaya nzima.

Ni Aprili. Ni wakati wa Real Madrid.

Tumekuwa hapa kabla. Hatutiwi wasiwasi na mchezo wetu mbaya katika ligi, lakini kwa namna fulani mechi kubwa za mtoano zinapoanza, Los Blancos wanakuwa katika hali nyengine.

Wakishikilia rekodi ya kushinda mataji 14 ya Uropa, ni vipi wameendelea kuonesha umahiri wao wa kuebuka washindi Ulaya?

PICHA: Real Madrid wakiadhimisha Ligi ya Mabingwa msimu uliopita

Real Madrid iliishinda Liverpool katika fainali ya Ligi ya Mabingwa mwezi Mei na kuandikisha rekodi ya mafanikio ya 14 katika mashindano hayo

Nguvu, mafanikio na Real Madrid daima wamekuwa marafiki wazuri

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kwa miaka mingi, hasa wakati wa utawala wa Franco, Real Madrid ilikuwa mwakilishi wa nchi hiyo kwenye jukwaa la soka duniani na ilibidi ionekane kuwa bora zaidi ambayo Uhispania inaweza kutoa. Ilikuwa ni wimbo wa taifa badala ya ule wa klabu ambao ulikuwa ukichezwa popote walipokwenda na kwa mtazamo huu unawapatia jukumu kubwa.

Unapotazama kwenye sanduku la rais hadi sasa siku ya mechi huko Santiago Bernabeu utangundua yote haya. Ukiwa umejaa wanasiasa wakubwa, vinara wa fedha, watu mashuhuri kutoka nyanja zote kama vile televisheni, filamu, michezo na vyombo vya habari, bila shaka utagundua kuwa hapa ndipo pa kuonekana.

Lakini wachezaji wote bora katika uwanja wao wanataka kuhusishwa na mafanikio. Umaarufu, nguvu na mafanikio vimeunganishwa kwa njia isiyoweza kutenganishwa na ikiwa unataka kukaa kuzungukwa na kampuni hiyo iliyoinuliwa, kushinda inakuwa wajibu.

Na nguvu hiyo ambayo imeenea kila kona ya Bernabeu ni chachu kwa wale wote wanaokumbatiwa nayo kwani ni uzito wa kutisha shingoni mwa wapinzani wao. Wachezaji na wasimamizi wengi wamezungumza kuhusu "hofu ya ajabu" ya uwanja wa Real Madrid, sentensi iliyotumiwa sana na mchezaji na meneja wao wa zamani, Jorge Valdano.

Pia kuna maoni kwamba "woga wa hali ya juu" husaidia kuwashawishi maafisa wakati ambao kuna mechi muhimu sana, katika matukio makubwa ambapo shinikizo ni kubwa.

Kila mtu kutoka juu hadi chini anaweka mahitaji ya juu sana na kushinda inakuwa falsafa pekee inayowezekana.

'Chochote isipokuwa ushinda ni janga'

Real Madrid wanapoenda kufanya manunuzi hawachukui chochote ila kilicho bora zaidi.

Matokeo yake ni ubora. Wachezaji wakubwa, wengi wao wakiwa na uzoefu mwingi, ambao wanaweza kukushindia mechi kubwa zaidi huwa ndio msingi wa kikosi chao.

Hawajawahi kuhangaishwa sana na mtindo wowote wa soka - tofauti na wapinzani Barcelona - lakini badala yake wanattumia fursa ya kipaji hicho bora zaidi.

"Huko Madrid, mbinu ya mchezo haijawahi kumuweka mtu macho. Mtindo ni kushinda... kushinda tangu mwanzo lilikuwa hitaji la kitaasisi," anasema mshindi wa Kombe la Dunia la Argentina Valdano.

"Jambo muhimu ni kwamba mchezaji anapofika Madrid anajifunza mara moja kwamba chochote chini ya ushindi ni janga.

"Klabu inajiwekea kikomo kwa kuwataka waishi kulingana na historia. Mashabiki pia, na bila huruma. Anayepata shinikizo yuko tayari kukabiliana na jukumu."

Wale ambao watashindwa kuonesha umahiri wao - na wamekuwa wengi - hawatadumu kwa muda mrefu katika klabu.

Kinachongojea wachezaji wapya ni ukumbi wa uwanja, maghala ya picha zinazowakilisha nani kati ya wababe wa soka - wa zamani na wa sasa - na wingi wa vikombe vinavyoonyeshwa. Itajaribu azimio lao la kiakili na utu kutoka siku yao ya kwanza.

Wale wanaofanikiwa wana ngozi ngumu. Kutoka kwa wahusika wa aina hii huja ushindi, ikiwa ni pamoja na matokeo ya kipekee na mechi za kutoka nyuma hadi kupata ushindi ndio alama yao ya biashara katika Ligi ya Mabingwa.

'Klabu inayowawezesha wachezaji'

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti

Carlo Ancelotti ameshinda kombe la vilabu bingwa mara mbili akisimamia klabu hiyo. Ni wachezaji wanaopanga ushindi au kushindwa katika klabu ya Real Madrid. Mchezaji wa zamani Victor Sanchez del Amo alisema kwamba Madrid ni bora kwaababu inawawezesha wachezaji.

Shabiki wa Real Madrid na mwandishi wa ‘Forging Glory’: Historia fupi ya Real Madrid’’, Jesus Bengoeche aliandika: Mbali na Jose Mourinho na fabio Capello, kumekuwa na nyakati chache ambapo kocha amekuwa muhimu kushinbda wachezaji.

"Nyota mkubwa wa Liverpool ni Klopp. Nyota mkubwa wa Madrid ni yeyote isipokuwa Ancelotti. Mambo yanapoharibika, mchezaji wa Liverpool anaangalia benchi akimtafuta Mjerumani huyo, kama mchezaji wa City akimtafuta Guardiola.

"Mchezaji wa Madrid haangalii benchi yake mambo yanapoharibika. Anajiangalia ndani na kukumbuka ni kwa nini Madrid walimsajili - kwa sababu ni mzuri ajabu, kwa sababu yeye ndiye mchezaji kwa wakati huo na mahali hapo."

Mchezaji huyo anaangalia beji kwenye shati lake na hahitaji kukumbushwa kuwa ilivaliwa na mastaa kama Di Stefano, Gento, Raul, Zidane, Cristiano, Ramos, Benzema, Modric anasema Bengoechea.

Wakati mwingine katika muktadha huu kidogo ni zaidi, kwenda kwa njia fulani kueleza kwa nini makocha wa Real Madrid kama vile Vincente del Bosque, Zinedine Zidane na Ancelotti wamepata mafanikio zaidi ya Ligi ya Mabingwa kuliko mifano migumu zaidi kama Capello na Mourinho.

"Hakuna kocha wa Madrid ambaye ameshinda Ligi ya Mabingwa bila, kwa kiwango fulani, kujua jinsi ya kutoweka kidogo," Bengoechea anahitimisha.

‘Real Madrid inaweza kuamka wakati wowote’

Akizungumza na wakufunzi wa FC Barcelona kabla ya mkondo wa pili wa Copa del Rey, na kutaja kuwa klabu hiyo ya Catalan iliwafunga wapinzani wao mara tatu mfululizo, kulikuwa na heshima, si kwa kile kilichotokea lakini kwa kile kinachoweza kutokea baadaye.

Makocha wa Catalan waliendelea kurudia kuwa Real Madrid wanaweza kuamka wakati wowote na kwamba hatujaona ubora wao msimu huu lakini hawana haja ya kucheza vizuri ili kushinda mechi kubwa. Real Madrid iliogopesha hata ndani ya Barcelona.

Real Madrid walishinda Ligi ya Mabingwa msimu uliopita baada ya kuwalaza Liverpool 1-0 kwenye fainali. Jinsi walivyoweza kufika huko, na kisha kushinda, ni jambo lingine kabisa.

Ukweli ni kwamba - mbali na mkondo wa kwanza wa Chelsea katika robo fainali - Real Madrid hii ilikuwa chini ya kila timu ambayo ilicheza katika hatua ya mtoano hadi na kujumuisha fainali.

Lakini walipata njia ya kushinda, na kuibuka na ushindi mnono dhidi ya Manchester City na Paris St-Germain wakiwa njiani kunyanyua kombe hilo.

Sifa yao kama wafalme waliorejea ni mbali na mpya, tangu wakati Derby ilipokuja Madrid katika Kombe la Uropa la 1975-76 na kuongoza 4-1 na kupoteza mechi ya pili 5-1 katika mojawapo ya mabadiliko makubwa zaidi barani Ulaya.

Msimu wa 1984-85 Uefa Cup, ushindi wa 3-0 dhidi ya Inter Milan baada ya kufungwa 2-0 kwenye mechi ya kwanza ulifuatiwa msimu uliofuata na ushindi wa 5-1 dhidi ya Borussia Monchengladbach baada ya kuibuka na ushindi wa 4-0 ugenini katika mchezo wa kwanza. Walifika fainali msimu huo kwa ushindi wa mabao 2-0 katika mechi ya mkondo wa pili baada ya kufungwa na Inter kwa mabao 3-1 ugenini.

Imani ya Real Madrid kutoka kwa vyombo vya habari hadi kwa mashabiki ni kwamba wanaweza kumshinda mtu yeyote.

Kushindwa kwa Barcelona kunaumiza zaidi na maumivu yake hudumu zaidi. Huko Madrid, wanasahau tu halafu kwa msingi wa kutokuwa na mantiki yoyote mara kwa mara wanazungumza juu ya uwezo wa kuishinda timu yoyote ilio mbele yao. Aina hiyo ya mawazo yasiyoweza kushindwa huwafikia mashabiki na hayaharibiki inapotokea. Watafanya hivyo wakati ujao.

Tofauti kati ya vilabu hivyo viwili ilifupishwa na mhariri wa Diario AS, Alfredo Relano, aliposema: "Barca ni eneo la hisia na Madrid chombo cha ushindi".

Mahitaji ya hali ya juu Real Madrid

Ni klabu ambayo kushindwa si chaguo, hasa kulingana na shabiki wa klabu hiyo.

Hakuna mchezaji mkubwa kuliko klabu. Uliza mtu yeyote ambaye amecheza huko na wote watakuambia kuwa haijalishi wewe ni nani, unaweza kuwa na jina kubwa kiasi gani, usipochukua jukumu lako vizuri watakuwa mwepesi kukukumbusha majukumu yako kwao na klabu. . Nyota wote wakubwa wa klabu hiyo wamepigiwa filimbi na kuzomwa huko Bernabeu. Hakuna mtu ambaye amesamehewa.

Mbinu hiyo ni tofauti na ile ya Anglo-Saxon na mashabiki wa Real Madrid wamechanganyikiwa ni kwa nini mashabiki wangependa kupongeza timu yao baada ya kupata kipigo cha mabao 5-0.

Mwishowe wanalingana zaidi na wale ambao kwa maneno ya Valdano, "kamwe hawakati tamaa na ambao kwa njia hiyo wanaheshimu historia ya Real Madrid na hadithi zake zote ‘’.