Jinsi China inavyokabiliana na Taiwan katika eneo la mpakani

Wakati Taiwan ilipopiga kamsa mwezi uliopita kuhusu idadi ya ndege za kivita za China zinazovuka mpaka usio rasmi kati yao, Beijing ilisema kwamba njia hiyo haipo.

Ndege 103 za kivita ambazo China ilirusha karibu na Taiwan - 40 kati ya hizo ziliingia katika eneo la Utambulisho la Ulinzi wa Anga (ADIZ) katika kisiwa hicho - zilikuwa ni uchokozi wa China katika mikakati yake ya kivita.

Beijing, ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikidai kuimiliki Taiwan, katika mwaka uliopita imefanya mazoezi mara kwa mara kuzunguka kisiwa hicho kinachojitawala kwa ndege za kivita na meli za jeshi la wanamaji. Mazoezi ya kijeshi yamechukua zamu ya kutisha hasa kwa kuzingatia viapo vya China vya "kuungana tena" na Taiwan.

Lakini Taiwan sasa ni kisanduku katika kile ambacho kimekuwa uhusiano tete kati ya Marekani na China - na wachambuzi wanasema mbinu za eneo la kijivu ni sehemu ya mkakati wa Beijing kudhibiti Taipei bila kufyatua risasi hata moja.

China inajaribu kuafikia nini?

Mbinu za vita za ukanda wa kijivu zinalenga kudhoofisha adui kwa muda mrefu - na hivyo ndivyo China inajaribu kufanya dhidi ya Taiwan, waangalizi wanasema.

Kwa kuvuka mara kwa mara ADIZ ya Taiwan, Beijing inajaribu ni umbali gani Taipei itaenda kuiimarisha, anasema Alessio Patalano, profesa wa vita na mikakati katika Asia Mashariki katika Chuo cha King's London.

ADIZ inahesabiwa kitaalamu kama anga ya kimataifa, lakini serikali zinaitumia kufuatilia ndege za kigeni.

Taiwan imekuwa ikiwaanda rubani wake katika ndege za kijeshi mara kwa mara ili kuonya ndege za China katika eneo lake la ADIZ - jibu ambalo linaweza kuzorotesha rasilimali za Taiwan kwa muda mrefu, Prof Patalano alisema.

Lakini hiyo sio lengo pekee - au faida. Mazoezi hayo yanaruhusu Uchina kujaribu uwezo wake kama vile uratibu wa nguvu na ufuatiliaji, kulingana na wachambuzi. Na pili zinalingana na mtindo wa China wa kuhalalisha viwango vya kuongezeka kwa shinikizo la kijeshi kwa Taiwan ili kuujaribu ulinzi wa Taiwan na msaada wa kimataifa kwa kisiwa hicho.

"Hatua kama hii siku moja inaweza kusasabisha shambulio la kwanza la kweli , na kuifanya iwe ngumu kwa Taiwan na [mshirika wake mkuu] Marekani kujiandaa ipasavyo," David Gitter, mshirika ambaye sio mkazi katika makao yake makuu ya Marekani.

Hatua za Beijing pia ziliweka upya msingi wa kukanusha madai ya Taiwan kwamba ina mpaka na Uchina katika Mlango-Bahari wa Taiwan, eneo la maji ambalo liko kati ya kisiwa hicho na China bara

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Mao Ning alisema "hakuna kinachojulikana kama mstari wa kati" katika mlangobahari huo alipoulizwa kuhusu mwitikio wa Taiwan kwa mazoezi ya Septemba.

"Pia inatumika kuzima umma wa Taiwan kwa tishio linaloletwa na jeshi kama hilo, ambalo linaweza kudhoofisha uungwaji mkono wa kisiasa kwa kujitolea zaidi kwa maandalizi ya kijeshi ya Taiwan kwa uwezekano wa vita," Bw Gitter alisema.

Wachambuzi wengi wanakubali kwamba jeshi la Taiwan - jeshi lenya idadi ndogo ya , jeshi la wanamaji na silaha za zamani – haliwezi kufananishwa na China yenye nguvu zaidi.

WaTaiwan wengi wanaonekana kukubaliana pia, kwa kuzingatia uchunguzi wa mwaka jana wa Wakfu wa Maoni ya Umma wa Taiwan ambao uligundua kuwa zaidi ya nusu yao wanafikiri China itashinda ikiwa itaingia vitani - ni thuluthi moja tu inayoamini Taiwan itashinda.

Na bado hamu ya bajeti kubwa ya ulinzi inaonekana kuwa dhaifu. Takriban nusu ya watu wa Taiwan wanadhani matumizi ya sasa yanatosha huku theluthi moja wakidhani kuwa tayari ni mengi, kulingana na uchunguzi wa hivi majuzi wa Chuo Kikuu cha Nottingham.

Je, ni wakati gani China hupeleka mbinu zake za kijeshi katika eneo la Grey zone

China mara nyingi hufanya mazoezi ya kijeshi kujibu mabadiliko ya kisiasa ya ngazi ya juu kati ya Taiwan na Marekani, ambayo inayachukulia kama uchochezi.

Haya yamekua makubwa na ya mara kwa mara tangu wakati wa ziara ya Spika wa Marekani Nancy Pelosi nchini Taiwan mnamo Agosti 2022. Beijing ilijibu kwa mazoezi ya wiki moja ambayo yalijumuisha mazoezi ya siku nne ya kuzima moto, na kufuatiwa na mazoezi ya kupambana na mashambulizi ya nyambizi pamoja na mazoezi ya uvamizi wa baharini.

Kisha mwezi wa Aprili, baada ya Rais wa Taiwan Tsai Ing-wen kukutana na Spika wa wakati huo wa Marekani Kevin McCarthy huko California, China ilifanya mazoezi ya "kuifunga" Taiwan katika kile kinachojulikana kama upanga wa pamoja na huku meli yake ya kubeba ndege za kivita kwa jina shandong pia ikishiriki .

China ilirusha ndege zake hadi pwani ya Taiwan ya Pasifiki upande wa mashariki, ikidokeza kuwa ilikuwa ikifanya mazoezi ya mashambulizi kutoka upande huo, badala ya magharibi, inayoelekea China Bara.

China inaonekana kufanya mazoezi ya kuzuia Taiwan. Lakini maafisa wa Pentagon wanasema hakuna uwezekano wa kufaulu kwasababu hali hiyo itawapatia fursa washirika wa Taipei kujihamasisha .

Mazoezi ya Septemba pia yalifuatia ziara ya makamu wa rais wa Taiwan William Lai nchini Marekani. Taipei ilionya kuhusu mazoezi baada ya China kumwita Bw Lai, aliye kifua mbele katika uchaguzi wa urais wa Januari, kama "msumbufu" kwa sababu ya kwenda Marekani.

Baadhi ya wachambuzi pia wanaamini kuwa China ilikuwa ikijaribu kuongeza nguvu kufuatia uvumi kuhusu kutokuwepo kwa waziri wake wa ulinzi Li Shangfu.

Mbinu pia si za kipekee kwa msuguano na Taiwan. Uchina hutumia hatua kama hizo kudai karibu Bahari nzima ya Uchina Kusini, ambayo inaweza kuwa ufunguo wa kuchukua udhibiti wa Taiwan.

Maji huandaa njia ya meli ya mabilioni ya dola na inaaminika kuwa na akiba kubwa ya mafuta na gesi. Beijing imejenga majengo makubwa juu ya miamba katika maji yanayozozaniwa ambapo Ufilipino, Taiwan, Malaysia, Vietnam na Brunei zina madai yanayokinzana.

Pia imetuma meli za walinzi wa pwani na wanamgambo kuzuia meli za usalama na uvuvi za Ufilipino katika maji haya licha ya mahakama ya kimataifa kutoa uamuzi kwamba madai ya Beijing hayana msingi wa kisheria.

Je, mbinu hizi za eneo la Grey zone zinaweza kuongezeka?

Mazoezi hayo yamepelekea eneo lenye jeshi kuongezeka - iwe katika maji karibu na Taiwan, au juu angani.

Marekani na washirika wake pia wameongeza mazoezi yao ya kijeshi katika Bahari ya Kusini ya China. Wiki hii tu, Marekani na Ufilipino zilianza awamu nyingine.

Hata ikiwa hakuna upande wowote wenye nia ya kuchochea, wachunguzi wanahofia kwamba kujengwa kwa meli za kivita na ndege za kivita kumeongeza uwezekano wa makosa ya gharama kubwa.

Wanajeshi wa nchi hizo mbili pia hawawasiliani tena moja kwa moja - ingawa Marekani inasema inajaribu kufufua simu hiyo ya dharura, ambayo itasaidia kutuliza ongezeko la tukio lolote ambalo halijapangwa.

Licha ya kuanza tena mazungumzo ya hali ya juu na Marekani, China haijaonyesha dalili za kuunga mkono Taiwan.

Uvamizi wa mara kwa mara mwezi Septemba unaonyesha kwamba ujanja kama huo utaendelea kama sehemu ya sera za Rais wa China Xi Jinping, hata bila "vichochezi vya kigeni", Bw Gitter alisema. Bw Xi hivi majuzi alisema "hatawahi kuahidi kuacha matumizi ya nguvu" na kwamba Taiwan "lazima itaungana" na China.

Lakini wachunguzi wa mambo wanasema China italazimika kutembea kwa kamba katika miezi ijayo kwa sababu kunyoosha misuli kupita kiasi kunaweza pia kufungua njia kwa Bw Lai, ambaye inamwona kama mgombeaji wa uhuru wa Taiwan, kushinda katika uchaguzi muhimu wa Januari.

Mwaka ujao pia ni wakati ambapo Beijing itazindua huduma ya meli yake mpya ya kubeba ndege za kivita Fujian, ambayo ni ya juu zaidi, ambayo Taipei inasema itaimarisha uwezo wa China wa kufunga Mlango wa bahari wa Taiwan.

Mazoezi ya kijeshi ya China yataendelea kuwa makubwa na ya mara kwa mara, Bw Gitter alisema.

"Tunaweza kutarajia nambari hizi kuongezeka zaidi hadi zifikie viwango ambavyo mtu anaweza kuona katika shambulio la kweli," alisema.