Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
China-Taiwan: Jinsi Beijing inavyobadilisha majibu yake kuhusu kinachofanyika Taiwan
China imekuwa ikifanya mazoezi ya kijeshi tena kuzunguka Taiwan - lakini baadhi ya wataalamu wanasema Beijing imezifuta kwani kisiwa hicho kitafanya uchaguzi wa rais katika kipindi cha miezi tisa, na ni kwa manufaa ya China kuona ushindi wa chama cha upinzani cha Kuomintang (KMT).
Hakuna kombora lililorushwa karibu na kisiwa hicho, mazoezi hayo yalichukua siku tatu pekee na mwanasiasa huyo wa Marekani ambaye alikutana na Rais Tsai Ing-wen Spika wa Bunge Kevin McCarthy - hajaidhinishwa.
Jibu la Beijing wakati msemaji wa zamani Nancy Pelosi alipotembelea Taipei Agosti mwaka jana lilikuwa kali zaidi.
Mazoezi hayo yamekuwa sehemu ya "utaratibu wa kawaida wa uendeshaji" wa China baada ya safari ya Bi Pelosi, anasema Profesa Chen-shen Yen wa Chuo Kikuu cha Kitaifa cha Chengchi cha Taiwan. "Wanahitaji kueleza msimamo wao, lakini majibu yao hayawezi kuwa ya kupita kiasi."
Muda ni muhimu.
Chama cha Kikomunisti cha China kilishinda KMT katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyomalizika mwaka wa 1949, na kulazimisha chama cha pili kukimbilia Taiwan. Lakini katika miongo ya hivi karibuni, wapinzani wa zamani wamepata msingi sawa katika Makubaliano ya mwaka 1992, uelewa usioeleweka ambao unasema kuna "China Moja" pekee ambayo inajumuisha Taiwan.
Iwapo Beijing itaendelea na matamshi yake makali, itahatarisha kuwa mpiga kampeni bora zaidi wa chama cha Democratic Progressive Party (DPP) kinachoegemea uhuru katika uchaguzi huo, Prof Yen anasema.
KMT ilipata ushindi mkubwa katika chaguzi za mitaa za mwaka jana, lakini wachambuzi wanasema sababu ya China ina uzito zaidi katika uchaguzi wa rais.
China imepitisha mkakati wa kuweka karoti na fimbo, anasema Profesa Fang-yu Chen wa Chuo Kikuu cha Soochow cha Taiwan. Kwa upande mmoja China inaahidi mabadilishano - ikiwa ni pamoja na kiuchumi na kiutamaduni - ikiwa Taiwan itakubaliana juu ya kanuni ya "China Moja". Wakati huo huo, inaendelea kujenga kijeshi.
"Beijing inataka kuwaambia watu wa Taiwan kwamba kutakuwa na vita ikiwa watampigia kura DPP, lakini kutakuwa na amani ikiwa watapigia kura KMT," anaongeza.
Ni usawa usio rahisi kupiga. Hata hivyo, China pia inakabiliwa na shinikizo la ndani la kuchukua hatua kali kuelekea Taiwan, hasa kutokana na kwamba China imekuwa ikichochea utaifa miongoni mwa raia wake, anasema
Ikiwa mazoezi ya kijeshi ya China yanalenga kuwazuia wanasiasa wa Marekani na Taiwan kuwa karibu sana, imepata mafanikio fulani - Taiwan inaonekana imechukua hatua za kupunguza mvutano karibu na mkutano wa Tsai na McCarthy.
Julai mwaka jana, Bw McCarthy alisema angependa kuongoza wajumbe wa bunge ikiwa atakuwa spika wa bunge. Utawala wa Tsai ulifanikiwa kumshawishi wakutane Marekani badala yake kwa sababu ya wasiwasi wa usalama wa Taiwan, gazeti la Financial Times liliripoti, likinukuu vyanzo.
Marekani pia ilijaribu kuupuuza mkutano huo, ikisema kuwa hiyo ilikuwa ni safari ya saba ya Bi Tsai tangu achukue mamlaka. Marekani na Taiwan zimekielezea kama kituo cha usafiri, badala ya "ziara".
"Marekani na Taiwan wamejenga uelewa wa kimyakimya kwamba wanapaswa kuchukua hadhi ya chini," anasema Prof Chen.
Bado ni ushindi kwa Taiwan, anasema, kwani Bw McCarthy alikuwa afisa wa ngazi ya juu zaidi wa Marekani rais yeyote wa Taiwan ambaye amewahi kukutana katika ardhi ya Marekani tangu 1979, wakati Marekani ilipokata uhusiano wa kidiplomasia na Taiwan.
Suala la Taiwan ni kigezo kikubwa zaidi katika uhusiano wa Marekani na China. China inakiona kisiwa hicho kinachojitawala kidemokrasia kama sehemu ya ardhi yake na haijakataza matumizi ya nguvu kukidhibiti.
Huku Marekani ikionesha uungaji mkono mkubwa kwa Taiwan, China imeishutumu kwa kupuuza sera yake ya muda mrefu ya China Moja. kukiri kidiplomasia kwa msimamo wa China kwamba kuna serikali moja tu ya China.
Chini ya sera hiyo, Marekani inatambua na ina uhusiano rasmi na China badala ya kisiwa cha Taiwan, ambacho China inakiona kama jimbo lililojitenga na kuunganishwa na bara siku moja.
Lakini hii ni tofauti na kanuni ya China Moja, ambapo inasisitiza Taiwan ni sehemu isiyoweza kutenganishwa ya China.
Sera ya Marekani si uthibitisho wa msimamo wa Beijing na kwa hakika kama sehemu ya sera hiyo, Washington inadumisha uhusiano "usio rasmi" na Taiwan, ikiwa ni pamoja na kuendelea kuuza silaha kwa kisiwa hicho ili iweze kujilinda.
Mwaka jana Rais Joe Biden alisema mara kwa mara Marekani itaingilia kati kuisaidia Taiwan ikiwa China itaishambulia
Kama sehemu ya urekebishaji wake wa vikosi vyake huko Asia, Marekani itafanya mazoezi yake makubwa zaidi ya pamoja ya kijeshi na Ufilipino kuanzia Jumanne.
Marekani pia imepata ufikiaji wa besi nne za ziada za Ufilipino katika Bahari ya China Kusini, na tatu kati yao ziko karibu na Taiwan.
Nchini Taiwan kwenyewe, watu wamebaki watulivu wakati mazoezi ya kulenga shabaha na "kukifunga" kisiwa yamefanyika.
Lakini Profesa Yen ana wasiwasi kwamba Kisiwa hicho kikahadaiwa kuijiingiza katika hali ya usalana usiokuwepo.
Ongezeko la hivi majuzi limeshuhudia ndege za kivita za Beijing na meli zikipita mstari wa kati, njia isiyo rasmi ya kugawanya eneo la Taiwan na China ambayo iliheshimiwa na pande zote mbili kwa karibu miaka 70.
"China inaweza kuendelea na mazoezi katika siku zijazo na Taiwan haitajua jinsi ya kujibu ikiwa itashambulia siku moja," anasema