Jinsi nilivyofichua uongo wa afisa mnyanyasaji wa shirika la ujasusi la Uingereza

...
Muda wa kusoma: Dakika 13

Wapelelezi husema uongo, lakini hawapaswi kukamatwa.

Jioni moja iliyonyesha mvua, siku ya Ijumaa mnamo Desemba, mawakili watatu wa MI5 walikuwa wakikaa katika chumba kwenye makao makuu ya BBC mjini London. Katika upande mwingine wa meza walikuwa mawakili wa BBC na mimi.

Hakukuwa na maafisa wa MI5 aliyesalia, baada ya kukataa ombi la kufanya mkutano huo kwa siri.

Baada ya kubadilishana tabasamu za wasiwasi, tulianza kujadiliana – na kuwaonyesha kwamba idara ya Usalama ilikuwa ikitoa ushahidi wa uwongo kwa mahakama.

Mkutano ulifanyika baada ya kuwaambia MI5 mwezi Novemba kwamba tulikuwa tukipanga kuripoti kwamba walikuwa wameambia uongo na kuwapa fursa ya kutoa maoni yao.

Katika majibu, idara hiyo ya Usalama ilisisitiza – kwa hasira – kwamba ilikuwa ikisema kweli kabisa.

Ambacho hawakujua hadi kufikia mkutano wa Desemba, ni kwamba nilikuwa na ushahidi thabiti kuthibitisha kwamba msimamo wao ulikuwa wa uwongo.

Kufichua ushahidi wa uwongo ni muhimu kwa sababu unaibua wasiwasi mkubwa kuhusu uaminifu wa ushahidi wa MI5 katika mahakama, ambapo tathmini kutoka kwa idara ya Usalama hupewa heshima kubwa.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Pia inazua mashaka mapya kuhusu ikiwa MI5 inaweza kuendelea na sera yake kuu ya siri – baada ya kufichua kwamba ilikuwa ikitumia siri hiyo kufanya uteuzi.

Uongo wa kwanza wa shirika ulitokea wakati serikali ilipoipeleka BBC Mahakama Kuu mwaka 2022 ili kuzuia taarifa kuhusu mwanasiasa wa mrengo wa kulia anayefanya kazi kama afisa wa MI5 – neno linalotumika kumaanisha mtumishi aliyepewa malipo na idhini kama mpelelezi.

Mwendesha mashtaka wa zamani, Suella Braverman, alishindwa kuzuia kuchapishwa kwa taarifa hiyo lakini alifaulu kupata amri ya kumzuia mtu huyo kujulikana, akidai kwamba atakuwa katika hatari. Matokeo yake, mtu huyo anajulikana hadharani kama X.

Tulijadiliana kwamba anapaswa kutambulika ili wanawake waweze kuonywa kuhusu mwanaume mkatili na mwenye vurugu kama huyo. X alitumia nafasi yake ya MI5 kumtawala kwa nguvu mpenzi wake wa zamani, ambaye alijulikana hadharani kwa jina la Beth.

Alikuwa akitumia vurugu za kimwili na kingono, na alirekodiwa akimtishia kumuua kisha kumshambulia kwa panga la kukatia miti.

Wakati wa utaratibu wa kisheria, MI5 ilisema kuwa haiwezi kuthibitisha wala kukanusha hadharani (NCND) kama X alikuwa ni afisa, kulingana na sera yake ya muda mrefu.

Hadharani, MI5 inasisitiza umuhimu wa sera ya NCND, ambayo inasema inafuata kwa watumishi wake. Mambo yoyote ya kipekee yanadai kuharibu siri inayolinda wanaume na wanawake kama hao na kuathiri usalama wa taifa.

Lakini kisha, wakati wa utaratibu, afisa mkuu wa MI5 – naibu mkurugenzi wa shirika na afisa mkuu wa kupambana na ugaidi, ambaye alijulikana kortini kama Shahidi A – alitaja baadhi ya simu zilizohusiana na mimi.

Katika taarifa ya mashahidi ya shirika, Shahidi A alisema kwamba mwakilishi wa MI5 alikuwa amezungumza na mimi katika tarehe ya awali. Hii ilifanyika baada ya idara ya Usalama kugundua kwamba BBC ilikusudia kumjumuisha X katika taarifa ya uchunguzi.

..

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, MI5 - iliyoko Thames House - imekubali ushahidi mahakamani haukuwa sahihi

Shahidi A alisema kwamba, wakati wa majadiliano, nilisema nilikuwa nikimshuku X kuwa ni afisa wa serikali, lakini kwamba MI5 "haikuthibitisha wala kukanusha" kama hili lilikuwa kweli.

Hakueleza ni nani aliyeanzisha majadiliano - ilikuwa MI5. Pia hakusema jinsi idara ya Usalama ilivyogundua taarifa inayopangwa ya BBC - X alikuwa amewaambia.

Katika taarifa yangu ya mashahidi, nilisema kwamba maelezo haya hayakufanana na kumbukumbu yangu kwa namna mbalimbali. Sikuenda kwa undani zaidi, kwa sababu - bila kukiuka sheria ya siri - nilishauriwa na mawakili kwamba haitaathiri masuala muhimu katika mzozo, ambayo yalijikita kwenye madai ya hatari kwa X ikiwa atatambulika na BBC.

Timu ya BBC pia ilipata sehemu ya taarifa kuhusu kesi hiyo - huku baadhi ya ushahidi na vikao vilifanyika kwa siri.

Wakati mmoja ambapo utaratibu wa siri ulitumika,mimi na timu ya BBC hatukuwepo, mawakili walioidhinishwa na usalama kwa niaba yetu walielezwa pia na maafisa wa MI5 kwamba ilikuwa imefuata sera yake ambayo "haikuthibitisha wala kukanusha" nilipozungumza nao kwa simu.

Lakini nilijua kwamba kile Shahidi A alisema kuhusu mimi katika taarifa yake kilikuwa si kweli. Nilijua kwamba MI5 haikuwa imetekeleza NCND. Kuwa mkweli, nilichukizwa na uongo wake.

Pia Sasa tunaweza kuripoti kwamba Mkurugenzi Mkuu wa MI5, Sir Ken McCallum, alimpigia simu Mkurugenzi Mkuu wa BBC, Tim Davie, mnamo Desemba 2021, ili kutia shaka kuhusu taarifa inayofanywa na BBC kuhusu X.

Maelezo ya Sir Ken kwa njia ya simu, ambayo yalitumwa kama sehemu ya ushahidi wa serikali katika kesi ya Mahakama Kuu ya 2022, yanaonyesha akidai kwamba taarifa inayoandaliwa "haikuwa sahihi na pia ya hatari."

Hata hivyo, taarifa ilikuwa sahihi. Jaji aliafiki kwamba nilichukua hatua sahihi kutathmini kama vipengele mbalimbali vya taarifa vilikuwa vya kweli na kwamba ilionyeshwa "kwa urahisi" kuwa na msingi wa ushahidi wa kuaminika.

Licha ya kutokuruhusiwa kumtambulisha X, Mahakama Kuu iliamua kwamba tunaweza kuripoti matokeo ya uchunguzi wetu. Ilionyesha kwamba X alikuwa akimnfanyia vurugu Beth na mpenzi mwingine wa zamani, na kwamba alikuwa msumbufu.

Wakati huo, Beth alifungua malalamiko kuhusu namna alivyotendewa na MI5 kwa (IPT) mahakama huru yenye uwezo wa kuchunguza madai ya haki za binadamu dhidi ya idara hiyo ya Usalama.

Ni katika mahakama hii ambapo MI5 ingeweza kusema uongo tena.

IPT mara nyingi hukutana kwa siri bila upande wa wadai, wawakilishi wao wa kisheria, wanahabari au umma kuwepo, ili kuzingatia ushahidi unaohusishwa na usalama wa taifa. Katika kesi ya X, hii ilimaanisha taarifa zote zilizothibitisha kwamba alikuwa ni afisa wa MI5.

..

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, X alimnyanyasa Beth kimwili na kingono, na kumshambulia kwa panga

Mawakili wa IPT wanapaswa kuwakilisha maslahi ya wadai katika vikao vya siri. Lakini Kate Ellis kutoka Kituo cha Haki za Wanawake, ambaye anamuwakilisha Beth, anasema mfumo huu una matatizo ya kimsingi.

"Huna haki ya kujua kinachosemwa kuhusu wewe. Kuna vitu ambavyo vinaweza kusemwa ambavyo unaweza kupinga. Unaweza kuitwa mwongo na huna haki ya kujua lolote kuhusu hili," anasema.

Beth aliweza kujua tu hatima yake kama alishinda au alishindwa, na kamwe hakuelewa ukweli ni kwanini, anasema Bi. Ellis.

Beth aliiomba mahakama hiyo kwamba MI5 iondoe sera yake ya hakuna"kuthibitisha wala kukanusha." Vinginevyo, mawakili wake walisema, sehemu kubwa ya kesi ingetakiwa kusikilizwa kwa siri. Walisema X alikuwa tayari amejitambulisha kwa Beth aliitumia kumnyamazisha.

Lakini mawakili wa MI5 walijitetea kuwa hii ingemaanisha idara ya Usalama kulazimika kwa "mara ya kwanza kabisa" kuthibitisha kwa upande wa tatu katika utaratibu wa kisheria ikiwa mtu huyo alikuwa ni afisa.

Majira ya kiangazi mwaka uliopita, IPT ilimkataa Beth. Ingawa ilikubali kwamba kutumia sera ya NCND kulikuwa na athari kwa haki yake ya kusikilizwa - kwa sababu hawezi kupinga ushahidi unaotolewa kwa siri - ilisema sera hiyo "inategemea kikamilifu uthabiti wa matumizi yake."

Iliongeza kwamba MI5 ilikuwa "imeshughulikia kwa ufanisi mkubwa katika mchakato huu na katika vikao vya BBC ili kuimarisha sera ya NCND."

MI5 iliendelea kutoa ushahidi wake wa uwongo kwa mahakama ya tatu wakati Beth alipoomba uchunguzi wa kisheria kuhusu uamuzi wa IPT.

Kuanzia hapo, nilijiamulia kwamba ukweli kuhusu tabia ya MI5 lazima uwekwe wazi. Nilimkuta Beth kwa mara ya kwanza alipokuwa mgonjwa sana baada ya unyanyasaji na kutishiwa na X. Nilielewa imefikia hatua mbaya kiasi gani na nilitamani kumtendea haki.

Nilianza kufanya kazi na timu ndogo ya mawakili wa BBC ili kuandaa mkakati.

Tatizo la MI5

Ukweli ni kwamba, katika simu kadhaa tulizozungumza, afisa mkuu wa MI5 alikiuka sera ya NCND kwa kunijulisha kwamba X alikuwa ni afisa na kuniita nifanye mawasiliano naye. Afisa huyo alisema alikuwa ameidhinishwa kisheria kuniambia taarifa hii.

Simu hizo zilikuwa sehemu ya jaribio la MI5 kunishawishi nisimtambulishe X kama mtu mwenye msimamo mkali kama sehemu ya taarifa yetu ya uchunguzi ilivyopangwa. Zilikuja baada ya mimi kumtumia X barua, ikielezea ushiriki wake katika vitendo vya vurugu na kumpa fursa ya kujibu.

Mnamo Novemba mwaka jana, baada ya kufanya kazi na timu ya kisheria ya BBC kwa miezi kadhaa, nilimwandikia MI5 kusema kwamba tulikuwa tukipanga kuripoti kwamba idara ya Usalama ilikuwa imeambia uongo mahakama, na kwamba ilikuwa imekiuka sera ya NCND katika mazungumzo nami kwa njia ya simu. Sikusema nitathibitishaje madai haya.

Wakati huo, mawakili wa BBC waliandikia ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu mpya, Lord Hermer, kuwaambia kwamba tulikuwa tukipanga kuomba mahakama ifungue sehemu ya taarifa ya shahidi wa MI5 ambapo ushahidi wa uwongo ulitolewa.

Mnamo 25 Novemba, mwanasheria wa serikali alijibu kwa niaba ya MI5 akiniambia kwamba MI5 "inasimamia maelezo yote yaliyotolewa kwa Mahakama Kuu katika taarifa ya Shahidi A".

Ilisema kwamba msimamo wa idara ya Usalama bado ni kwamba "hakukuwa na kigezo chochote" kutoka kwa sera ya NCND na ilipendekeza kwamba ushahidi wa MI5 ulikuwa "umezingatiwa kwa makini."

Nilishtushwa na majibu haya. MI5 ilikuwa ikibahatisha kwamba nisingeweza kuthibitisha kile nilichosema.

Ilikuwa ni kamari ambayo idara ya Usalama ilikuwa karibu kupoteza.

Tulijibu kwa kusema kwamba MI5 ilialikwa kwenye mkutano ambapo ingeweza kukagua ushahidi ambao tungeutumia katika maombi yetu mahakamani.

Tulichukua hatua hii isiyo ya kawaida ili kuruhusu MI5 kutafakari kama ingekubaliana na kubadilisha masharti ya zuio lililowekwa mwishoni mwa kesi dhidi yetu mwaka 2022.

Na hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa mkutano huo wa 13 Desemba, wakati mawakili watatu waliokuwa wakiwakilisha MI5 walifika ofisi za BBC- London kukutana na mimi na timu ya kisheria ya BBC.

Walipitia na kusikiliza taarifa muhimu, ambayo ilijumuisha maandishi ya simu ya kwanza kutoka MI5, barua pepe niliyomtumia afisa wa MI5 kufuatia simu hiyo, na rekodi ya sauti ya simu ya siku iliyofuata.

Niliipitisha timu ya MI5 katika ushahidi kwa mpangilio. Hisia yangu ilikuwa kwamba walionekana kuwa na nguvu kidogo walipoonyeshwa maandishi, walifadhaishwa na barua pepe, na walishindwa walipokutana na rekodi ya sauti ya dakika 40 - kwani kila hatua ilionyesha kwamba ushahidi wetu ulikuwa imara zaidi.

Ufichuzi wa hiari

Ushahidi wangu wa maandishi ulionyesha madhumuni ya simu ya MI5 - kunijulisha kwamba X alikuwa ni afisa.

Afisa wa MI5 ambaye aliniita alisema alikuwa "ameruhusiwa" kuniambia, kitu ambacho alisema vinginevyo kingekuwa "haramu".

Taarifa hii ilitolewa kwangu na MI5, si kama jibu la swali langu ikiwa X alikuwa afisa - jambo ambalo sikuuliza kwa X wala kwa MI5.

Sikuwa nimewahi kuzungumza na afisa wa MI5 hapo awali. Hakuwa chanzo za taarifa wala rafiki yangu. Kwa kweli, kama ningegundua baadaye, alikuwa akijaribu kumlinda X na kutoa picha ya uongo kuhusu hatari aliyosababishia wanawake.

Afisa huyo, ambaye alifanya kazi kwa karibu na Mkurugenzi Mkuu wa MI5 Sir Ken McCallum, alimtaja X kama mtu ambaye alikuwa anatoa taarifa kuhusu wanyanyasaji katika idara ya Usalama, lakini si yeye mwenyewe.

Ombi la simu lilikuwa kwamba tusiendelee na taarifa yetu iliyopangwa kwa sababu MI5 ilisema ilikuwa si ya kweli.

Hisia yangu ilikuwa kwamba MI5 ilipiga simu hiyo wakidhani ningeweza kukubali ombi hili bila tashwishwi yoyote. Badala yake, katika mazungumzo hayo, nilipinga namna MI5 ilivyomuelezea X, ambaye nilimwona - na bado namwona - kama mnyanyasaji.

..
Maelezo ya picha, Beth amekuwa akitafuta majibu kuhusu jinsi MI5 ilivyoshughulikia afisa wake baada ya kumfanyia unyanyasaji

Pia nilijadili na MI5 kuhusu vurugu, unyanyasaji na vitendo vya kikatili ambao X alikuwa akijihusisha nao katika maisha yake ya kibinafsi. Sikusema jinsi nilivyojua kuhusu mambo haya, wala kusema majina ya watu walioguswa nayo. Mambo haya hayakuwa katika barua yangu kwa X na nadhani afisa wa MI5 alistaajabia nilipo yaibua.

Nilieleza waziwazi jinsi nilivyokuwa na wasiwasi kuhusu mambo haya. Nilikuwa na wasiwasi kuwa MI5 ilikuwa ikijaribu kumlinda mtu niliyemwona kama tishio kwa wanawake, watoto na umma kwa ujumla.

Simu ilikatika na nikasema nitazingatia ombi lake, ikiwa ni pamoja na kujadili kwa kina katika vikao vya uhariri.

Afisa wa MI5 aliniambia alikuwa akifanya uhakiki kulingana na wasiwasi nilioonyesha kuhusu X. Aliniomba nitume barua pepe kumueleza kwa muhtasari kuhusu tabia ya kibinafsi ya mwanaume huyo ambaye nilikuwa nimetaja katika simu.

Barua pepe niliyomtumia muda mfupi baadaye ilisema: "Kama tulivyozungumza, mwanaume anayehusika alikuwa na anahusishwa na tuhuma za vurugu na udanganyifu dhidi ya mwanamke Mwingereza. Vurugu zinazojumuisha jaribio la mauaji."

"Anadaiwa kujihusisha na unyanyasaji wa kijinsia na unyanyasaji wa kingono, kuonyesha mwelekeo wa ukatili kwa watoto, na kusababisha athari za kisaikolojia familia yake."

"Jaribio la mauaji" lilihusu tukio la panga. Wakati huo, nilikuwa nimesimuliwa na Beth kuhusu tukio hilo lakini sikuwa nimeona video ya tukio hilo. Baadaye ningepata video hiyo na kuchukua hatua za uchunguzi ili kuthibitisha kile nilichokuwa nimesikizwa, jambo ambalo MI5 lingefanya kama lingengependa.

Kuvuka mipaka

Kesho yake kulikuwa na simu nyingine kutoka kwa afisa huyo wa MI5.

Nilirekodi mazungumzo hayo kwa madhumuni ya kutunza kumbukumbu, kwa mujibu wa Miongozo ya Uhariri ya BBC, kwa sababu nilitaka kuwa na rekodi kamili ya kile kilichosemwa. Pia, sikuwa na imani na MI5.

Katika simu iliyorekodiwa, afisa mkuu wa MI5 alidai idara hiyo "imetathimini kwa hakika kwamba afisa huyo hakujihusisha na vurugu za hivi karibuni.

Utafiti wangu ungeendelea kuthibitisha kwamba tathmini hii ilikuwa ya uwongo kabisa na shambulio la panga lilikuwa ni la mwaka mmoja uliopita.

Afisa huyo alisema: "Tunatilia shaka sana tuhuma za hivi karibuni za vitendo vya vurugu, hasa dhidi ya mtu huyo."

Alisisitiza kwamba tathmini ya MI5 ilikuwa kwamba "tunaamini kwamba kwa kweli hakujihusisha na vitendo vya vurugu vya hivi karibuni," ingawa aliongeza kuwa hawangeweza "kusema kwa dhahiri kuwa hilo lilikuwa kweli."

Katika simu hiyo, alikubali pia kwamba X hakuwa na thabiti na alikuwa akijihusisha na "shughuli nyingi za... magenge ya madawa ya kulevya" awali, "alipitia mambo mengi," na alikuwa "kutoka kwenye historia ya mbaya sana," akimaanisha alikuwa na vurugu.

Licha ya yote haya, MI5 ilimtaja uhusiano wa X na Beth kama "kidogo kuwa na matatizo,"akitaja kwamba alikuwa na changamoto ya "afya ya akili."

Nilipomwandikia X, nilitaja chapisho la mtandaoni la kutisha na kushtua aliyoiweka, kuhusu unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake - kwa kutumia lugha chafu sana.

Afisa wa MI5 alidai kwamba wakati X alipoweka chapisho hili alikuwa amepunguziwa mamlaka kwa muda - yaani hakuwa akifanya kazi kwa MI5 wakati huo.

Nilielezea kwamba, kulingana na nilivyomjua X, posti hiyo ndiyo ilikuwa tabia yake halisi, ilionyesha mwelekeo wake wa kutumia vurugu dhidi ya wanawake, na hiyo ndiyo ilikuwa sababu ya wasiwasi wangu kuhusu yeye.

Afisa huyo alikubali kwamba chapisho hilo lilivuka mpaka," lakini alionekana kutokuelewa mantiki wazi kwamba, kama ilipostiwa wakati X alikuwa amekatwa mamlaka, hiyo ilikuwa ikionyesha asili halisi ya X zaidi. Alikuwa mnyanyasaji wa wanawake hatari kwa kweli - haikuwa ni uigizaji aliofanya kwa ajili ya MI5.

Afisa wa MI5 alionekana kuwa na shauku kubwa kuhusu jinsi tulivyogundua utambulisho wa kweli wa X. Nilishangaa kuhusu hili, kwa kuwa nilikuwa nikizungumza na MI5, na nilielezea kuwa ilikuwa ni kanuni ya msingi ya uandishi wa habari. Wakati wa simu hiyo, nilimwambia pia afisa huyo kuwa X alikuwa kwenye mtandao kwa kutumia jina la utani alilotumia kwenye kazi yake ya MI5.

Afisa wa MI5 alionekana kuwa na wasiwasi na habari hii.

Hata hivyo, alinihimiza niende kukutana na X na kufahamu kuhusu kazi yake kama afisa. Alitoa pendekezo hili mara mbili wakati wa simu hiyo. Nilipuuzilia mbali mapendekezo yote mawili.

Hisia yangu ilikuwa kwamba hii ilikuwa ni jitihada ya kijinga ya kunipa kitu cha kusisimua - kukutana na afisa wa MI5 - ambacho kingenifanya nisahau wasiwasi wangu. Niliona kuwa ilikuwa si sahihi kabisa, ikizingatiwa dhihaka ya X kwa wanawake, tabia za udhalilishaji wa watoto, vurugu na unyanyasaji.

Kutokuwa sahihi

Siku tano baada ya mkutano wa Desemba ambapo tulisikizisha mazungumzo ya simu kwa mawakili wa MI5, serikali iliandika kwa BBC ikisema kwamba MI5 sasa ilichukua msimamo kwamba ushahidi wake "huenda ukawa si sahihi kwa kiasi kikubwa, na kwamba ni muhimu msimamo huo usahihishwe haraka iwezekanavyo."

BBC iliamua kwamba njia bora ya kuhakikisha mahakama na serikali wana ushahidi husika ilikuwa kuwasilisha ombi letu la kuchapisha ushahidi wa uwongo. Ombi hilo lilijumuisha tamko jipya la shahidi kutoka kwangu.

Tulifungua mnamo Krismasi.

MI5 ilibadili msimamo wake kabisa.

Katika tamko jipya la shahidi lililowasilishwa kwa mahakama, naibu mkurugenzi wa MI5, Shahidi A, alisema alijuta "kwa dhati" kutoa ushahidi usio sahihi.

Alisema kwamba taarifa hiyo potofu "ilionyesha imani yangu ya dhati wakati huo, na ambayo ilionyesha kwa usahihi taarifa nilizozipata."

Alisema pia kwamba "sasa ni wazi kwangu kwamba MI5, kwa kweli, ilijitenga na NCND wakati wa mazungumzo."

Wakati huu, hajatoa maelezo kuhusu jinsi alivyotoa ushahidi potofu, licha ya serikali kusema miezi miwili iliyopita kwamba ilikuwa ikifanya kazi "kwa haraka" kutoa maelezo.

Shahidi A hajamtaja mtu aliyeutoa taarifa aliyotegemea.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, BBC iliiomba Mahakama Kuu kuchapisha ushahidi huo wa uongo

Hakuna maelezo kuhusu nani alihusika na kutoa ruhusa ya kufichua nafasi ya X kwangu. Ushahidi wetu unaonyesha kuwa maafisa mbalimbali wa MI5 walikuwa wanafahamu kuhusu mazungumzo yaliyonihusisha , ikiwa ni pamoja na maafisa wa kesi hiyo na wakuu wa kupambana na ugaidi.

Zaidi ya hayo, sera ya serikali inayohusiana na mipango ya kujitenga na NCND inasema kuwa mashirika yanapaswa kuwajulisha wenzao wa Whitehall, ikiwa ni pamoja na Ofisi ya Baraza la Mawaziri, kwa "njia ya wakati." Hii inamaanisha kwamba Ofisi ya Baraza la Mawaziri na Ofisi ya Ndani – kama idara ya Whitehall inayohusika na MI5 – walipaswa kujua mapema kuhusu afisa X kuondoka NCND.

Katika taarifa ya Jumatano, serikali ilisema mawaziri na watumishi wa serikali hawakushirikishwa "kawaida" kuhusu utambulisho binafsi na kwamba hawakushirikishwa katika tukio hili.

Idara ya Usalama inafanya uchunguzi wa kina na serikali imeanzisha mapitio ikipendekeza mabadiliko ya kuhakikisha kuwa mahakama zinapewa taarifa sahihi katika siku zijazo.

Lakini kuna wasiwasi halisi kuhusu jinsi uchunguzi huo utakavyokuwa wazi, kama mapitio sasa yanahitaji kupendekeza jinsi ya kuhakikisha MI5 inatoa ushahidi sahihi kwa mahakama, baadhi ya watu watajiuliza nini kimekuwa kikifanyika hadi sasa.

Vizuizi

Swali hili linatiwa wasiwasi hasa kwa sababu mahakama zinahitaji kutoa udhibiti maalum kwa MI5 kuhusu masuala ya usalama wa taifa.

Mahakama na wapelelezi wanaoshughulikia masuala kama haya mara nyingi hufanyika kwa siri, lakini hushughulikia masuala uhuru, maisha na kifo – mashambulizi ya mauaji ambayo hayakuzuiwa na MI5, watu ambao uraia wao wa Uingereza umepokonywa, watu waliokubaliwa kuishi chini ya mamlaka kali za kupambana na ugaidi.

MI5 imetoa "pole isiyozuilika" kwa BBC na mahakama zote tatu ambazo zilitumiwa na ushahidi potofu. "MI5 inachukua jukumu kamili," taarifa zake za kisheria zinasema.

Imesema inatambua umuhimu wa kuhakikisha kwamba ushahidi wowote inaotoa ni wa kweli, sahihi na kamili.

Na iliongeza: "Inatambua kikamilifu majukumu maalum ambayo MI5 inayo katika suala hili, na kwamba mahakama lazima iweze kutegemea kabisa ushahidi wowote inaotoa."

Ufichuzi huu unakuja wakati ambapo kuna uchunguzi mkubwa zaidi kuhusu sera ya NCND, kufuatia uchunguzi kuhusu afisa wa serikali ya Uingereza anayeitwa "Stakeknife", muuaji na mtesaji ambaye alitoa taarifa kuhusu IRA wakati wa matatizo huko Ireland ya Kaskazini.

Vikosi vya usalama na serikali wamekataa kuthibitisha au kukanusha kama Stakeknife alikuwa Freddie Scappaticci, ambaye alifariki mwaka jana, ingawa ukweli huu unajulikana sana.

Jon Boutcher, mkuu wa zamani wa upelelezi aliyeandika ripoti yake ya awali, alisema ndani ya serikali na vikosi vya usalama kuna "dhamira isiyotetereka yenye kufananishwa na ukuta wa mawe."

Alisema sera hiyo "inadhania utendaji wa kisheria kutoka kwa vikosi vya usalama," jambo ambalo "kwa ujumla ni dhana salama," lakini ambalo linahitaji "upimaji na uthibitishaji."

Ripoti yake ilipendekeza kwamba serikali iangalie, iandike na kufafanua mipaka halali ya sera ya NCND katika uhusiano wa kutambua maafisa katika muktadha wa kesi za kihistoria huko Ireland ya Kaskazini.

Serikali bado haijajibu pendekezo hilo.

..

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Jon Boutcher alisema kwamba sera ya NCND ilikuwa na dhamira thabiti

Kesi ya Beth tayari ilikuwa na athari kubwa kwa MI5 kuhusiana na jinsi inavyothamini na kudhibiti maafisa, hasa wale wanaoweza kuwa hatari kwa wanawake na wasichana.

Sasa imepata athari kubwa zaidi – kuhusu kiasi gani ushahidi wa MI5 unaweza kuaminika na kutegemewa, na kama sera ya NCND inahitaji kubadilishwa.

Ushahidi mpya unaonyesha kwamba MI5 haikufuata NCND katika kesi ya X na, kweli, ilitelekeza kabisa sera hiyo huku ikipuuzilia mbali tabia ya unyanyasaji na itikadi kali ya afisa huyo.

Inaonyesha kwamba MI5 ilijua aina ya mtu alivyokuwa, na inadhihirisha mtazamo wake wa kupuuzilia mbali wasiwasi kuhusu unyanyasaji na vurugu alizokuwa akizifanya.

Na hii inatarajiwa kumaliza kesi ya mapitio ya kisheria ya Beth, ambayo ilikuwa inachunguza kama MI5 ilipaswa kuruhusiwa kuimarisha NCND.

MI5 yenyewe imependekeza kwamba uamuzi huo sasa upitiwe upya na mahakama ya awali, IPT.

Beth atarudi mahakamani, akitafuta ukweli kati ya siri za serikali na uongo.

Imetafsiriwa na Martha Saranga na kuhaririwa na Ambia Hirsi