Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 17.11.2023

tt

Chanzo cha picha, Getty Images

Brentford wana imani kuwa mshambuliaji wa Uingereza Ivan Toney, 27, ambaye amekuwa akihusishwa na Arsenal na Chelsea, atasaini mkataba mpya na klabu hiyo. (Talksport)

Lakini Toney, ambaye mkataba wake unakamilika katika msimu wa joto wa 2025, anataka kuondoka na huenda akadai kifungu cha kutolewa katika mkataba wowote mpya na klabu hiyo. (90min)

Manchester City itamenyana na Liverpool kumsajili tena mshambuliaji wa Bayern Munich na Ujerumani Leroy Sane, 27. (Bild, via Sun)

tt

Chanzo cha picha, Getty Images

Sir Jim Ratcliffe, ambaye anakaribia kununua 25% ya Manchester United, anatarajiwa kuchukua mwongozo kutoka kwa Sir Alex Ferguson wakati akifanyia marekebisho klabu hiyo. (Telegraph - usajili unahitajika)

Crystal Palace na Fulham wanavutiwa na mkataba wa mkopo wa mshambuliaji wa RB Leipzig na Ujerumani Timo Werner, 27, ambaye amekosa kuvutia katika klabu hiyo ya Bundesliga. (90 min)

Wakala wa kiungo wa Barcelona Ilkay Gundogan amepuuzilia mbali tetesi zinazomhusisha mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 33 na kuhamia klabu ya Uturuki ya Galatasaray. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania)

.

Chanzo cha picha, Reuters

Arsenal wako tayari kumruhusu mlinzi wa Poland Jakub Kiwior kuondoka katika klabu hiyo kwa mkopo kwani mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 anataka muda zaidi wa kucheza katika kikosi cha kwanza. (90 min)

Chelsea huenda wakamrejesha kiungo wa Brazil Andrey Santos,19, kutoka klabu ya Nottingham Forest ambako anacheza kwa mkopo kwa sababu ya kukosa muda wa kucheza. (Standard)

Mshambuliaji wa Tottenham Son Heung-min, 31, amepuuza madai kwamba alipata jeraha alipokuwa akiichezea Korea Kusini katika mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Singapore. (Standard)

Son Heung-min

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mshambuliaji wa Tottenham Son Heung-min

Manchester City wamekubali mkataba wa pauni milioni 1.2 kumsajili kiungo mshambuliaji wa Leeds United mwenye umri wa miaka 15 Finley Gorman. (Football Insider)