Kombe la Dunia 2026: Je, timu za Afrika zitafuzu vipi Marekani, Canada na Mexico?

Chanzo cha picha, Getty Images
Michuano ya Afrika ya kufuzu kwa Kombe la Dunia la Fifa 2026 itaanza tarehe 15 Novemba, huku bara hilo likitarajiwa kutuma idadi kubwa ya mataifa kwenye maonyesho mapya ya kimataifa ya soka yaliyopanuliwa.
Ni nchi tano pekee ndizo zilikuwepo kwenye fainali za 2022 nchini Qatar, ambapo Morocco iliweka historia kwa kuwa timu ya kwanza ya Afrika kutinga nusu fainali.
Hata hivyo, timu tisa za Afrika zimehakikishiwa nafasi ya kufuzu katika toleo lijalo nchini Canada, Mexico na Marekani, mchuano ambao utashirikisha timu 48, kutoka 32.
Kuna nafasi hata ya 10 kufuzu kupitia mchujo wa mabara.
Huku kukiwa na uwezekano maradufu wa idadi ya timu zitakazofuzu kwenda Amerika Kaskazini, Shirikisho la Soka Afrika (Caf) limebadilisha muundo wa kufuzu.
BBC Sport Africa inaeleza unachohitaji kujua kuhusu kampeni itakayodumu kwa miaka miwili.
Mechi zitachezwa lini?
Mechi mbili za kwanza katika kila kundi zitachezwa kati ya 15 na 21 Novemba, wakati raundi ya tatu na nne itafanyika Juni ijayo.
Huku mechi za kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika 2025 pia zikihitajika kuratibiwa mwaka wa 2024, siku sita za mechi zilizosalia za kufuzu kwa Kombe la Dunia zitasambazwa katika madirisha ya kimataifa mwezi Machi, Septemba na Oktoba 2025.
Vipi kuhusu mechi za mchujo?
Baadhi ya washindi wa pili katika makundi tisa ya kufuzu watapata fursa nyingine ya kufika Canada, Mexico na Marekani.
Timu nne zilizopo katika nafasi ya pili bora zitapangwa katika hatua ya mtoano, huku nusu fainali na fainali zikichezwa mnamo Novemba 2025 kuamua ni timu gani ya Afrika itafuzu kwa dimba la mchujo baina ya mabara.
Kujiondoa kwa Eritrea kutakuwa na athari kwenye viwango hivyo, huku Caf bado ikiwa haijatoa tangazo la jinsi suala hilo litakavyotatuliwa.
Raundi ya mwisho ya kufuzu kwa kombe la dunia itahusisha timu sita zitakazochuana kuwania nafasi mbili za mwisho kwenye fainali za 2026, na inatarajiwa kufanyika Machi 2026.
Je ni timu gani ndogo zinazopigiwa upatu kuwika?

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Ni nchi 13 pekee za Kiafrika ambazo zimewahi kucheza Kombe la Dunia, lakini kuongezeka kwa timu tisa zilizohakikishwa kufuzu kunamaanisha kuna nafasi kwa wachezaji wa kwanza katika muda wa miaka mitatu.
Kila kundi la kufuzu kwa 2026 lina angalau upande mmoja ambao hapo awali ulifuzu mashindano hayo.
Hata hivyo, Mali - ambao walilazwa na Tunisia katika mechi ya mtoano ya Afrika huko Qatar 2022 - ndio wanaongoza katika Kundi I mbele ya Ghana.
Burkina Faso, ambayo ilimaliza katika nafasi ya nne kwenye Kombe la Mataifa ya 2021 nchini Cameroon, inaweza kuijaribu Misri katika Kundi A huku Equatorial Guinea ikipata ushindi wa nyumbani dhidi ya wapinzani wao wa Kundi H Tunisia katika mechi za kufuzu kwa Kombe la Dunia la 2022 na Kombe la Mataifa ya 2023.
Licha ya kuwa na idadi ya watu zaidi ya nusu milioni, Cape Verde imejigeuza kuwa timu inayofuzu Kombe la Mataifa ya Afrika, na kufika katika michuano minne kati ya sita iliyopita, na watafurahia nafasi yao ya kuwavuruga wazani wa Kundi D, Cameroon.
Wakati huohuo, je Serhou Guirassy - ambaye alifunga mabao 15 katika mechi zake tisa za ligi akiwa na Stuttgart msimu huu - anaweza kusaidia Guinea kushinda Algeria katika Kundi G?
Ikizingatiwa kuwa mechi za kufuzu zimetawanyika kwa miaka miwili, huku mechi nne zikifanyika Septemba na Oktoba 2025, kunaweza kuwa na matukio ya kushangaza kulingana na umbo na usawa wa wachezaji.












