Je, mpango wa makombora wa Iran ni kwa ulinzi wa taifa au tishio la kimataifa?

v

Chanzo cha picha, Getty Images

    • Author, Majid Khayamdar
    • Nafasi, BBC

Asubuhi moja majira ya joto 2018, eneo kubwa la kusafisha mafuta ulimwenguni limeshambuliwa. Rada za Saudi zilikuwa zikitazama anga kuzuia makombora kutoka Iran au Yemen, makombora na droni yalipiga kituo cha mafuta cha Aramco.

Uzalishaji wa mafuta wa Saudia ulipungua kwa muda. Waasi wa Houthi wa Yemen walihusika na shambulio hilo, lakini Saudi Arabia na madola ya Magharibi yalinyooshea kidole cha lawama Iran. Lakini Iran ilikana kuhusika.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetangaza kuwa mpango wake wa makombora ni kinga dhidi ya mashambulizi ya kigeni. Lakini madola ya Magharibi na washirika wao wa kikanda wanaona mpango huu kama tishio dhidi yao.

Iran ndio nchi pekee isiyo na silaha za nyuklia ambayo imeunda makombora yenye uwezo wa kushambulia hadi kilomita 2,000.

Kufichuliwa kwa mitambo ya siri ya nyuklia mwaka 2002, ikiwa ni pamoja na kituo cha kurutubisha uranium huko Natanz na kinu cha maji mazito ya plutonium huko Arak, kulizidisha shaka kwamba nchi hiyo inatafuta kutengeneza silaha za nyuklia. Lakini Iran inasisitiza haina mpango wa kuunda silaha za nyuklia.

Hossein Mousaviyan, aliyekuwa mkuu wa kamati ya sera za kigeni ya Baraza Kuu la Usalama la Taifa katika miaka ya kwanza baada ya kufichuliwa kwa mpango wa nyuklia wa Iran, baadaye alikiri mipango ya makombora na nyuklia ya nchi hiyo ilianzishwa wakati wa vita na Iraq.

Maendeleo ya mpango wa nyuklia wa Iran katika miaka iliyofuata na utengenezaji wa makombora yenye uwezo wa kubeba vichwa vya nyuklia - yaliongeza wasiwasi kuhusu mpango wa makombora wa Iran.

Lakini makubaliano ya nyuklia (JCPOA) kwa kiasi fulani yalipunguza wasiwasi kuhusu mpango wa huo. Mataifa yenye nguvu duniani yaliuwekea vikwazo mpango huo kwa kupitisha azimio katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, lakini Iran haijawahi kutii vikwazo hivi na imeendelea na shughuli zake za makombora.

Baada ya Marekani kujitoa JCPOA, na hatua ya kupunguzwa ahadi za nyuklia za Iran, sambamba na kuendelea na mpango wake wa makombora kumezidisha wasiwasi kwamba siku moja Iran inaweza kuwa na makombora ya nyuklia.

Mbali na kuendeleza mpango wa makombora, Iran imejaribu kuongeza uwezo wake katika vita vya ardhini, majini, kutumia wana mgambo na uwezo wa kushambulia maeneo jirani.

Kwa upande mmoja, hatua hizo zimezidisha nguvu za Iran, na kwa upande mwingine zimeongeza wasiwasi wa kiusalama wa madola ya Magharibi na waitifaki wao katika eneo hili.

Makombora

v

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kambi ya Ain al-Assad baada ya kupigwa na makombora ya Iran
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Mpango wa makombora wa Iran uliundwa wakati wa vita na Iraq miaka ya 1960. Iraq ilikuwa ikipiga miji na vituo vya kimkakati vya Iran kwa makombora ya balestiki tangu mwanzo wa vita. Iran ambayo haikuwa na makombora kama hayo, haikuweza kujibu.

Lakini baadaye ilijibu kwa makombora ya Scud kutoka Libya na Korea Kaskazini. Baada ya vita, Iran iliendelea na mpango wa makombora kwa msaada wa kigeni (hasa kutoka Korea Kaskazini na kwa kiasi fulani kutoka Urusi na China).

Hivi sasa, Iran ina idadi isiyojulikana ya aina mbalimbali ya makombora - ya masafa mafupi na marefu ya hadi kilomita 2000. Idadi kamili haijatangazwa rasmi, lakini vyanzo mbalimbali vinakubali kwamba silaha za makombora za Iran ni kubwa zaidi katika Mashariki ya Kati.

Makombora ya Scud kutoka Korea Kaskazini wakati wa vita na Iraq yana asili ya Kirusi. Kombora la Shahab 1 ni nakala ya kombora la Scud B. Kombora hili hufika hadi kilomita 300 na linaweza kubeba kichwa chenye uzito wa kilo 1000.

Kombora la Shahab 2 toleo la Scud C. Kombora hili linaweza kubeba kichwa cha kilo 770 hadi kilomita 500. Kombora la Shahab-3 hutumia teknolojia ya makombora ya Nudong ya Korea Kaskazini.

Iran baadaye iliboresha kombora la Shahab 3 na kuzalisha makombora ya Qadr na Emad. Makombora haya yanaweza kufikia umbali wa kilomita 2000.

Kombora jipya zaidi la umbali wa kilomita 2,000 ni kombora la "Khorramshahr." Iran inasema kombora hili linaweza kubeba vichwa kadhaa, linaweza kuongozwa na lina usahihi wa hali ya juu.

Inaaminika kuwa kombora hili liliundwa kwa kutumia teknolojia ya kombora la Mossudan ya Korea Kaskazini. Iran inasema haina mpango wa kutengeneza makombora yenye masafa ya zaidi ya kilomita 2,000.

Wakati wa vita na Iraq, Iran ilianza kutengeneza roketi imara za "Eagle" kwa msaada wa kiufundi wa China. Mradi wa kutengeneza aina hii ya roketi ndogo ya umbali wa kilomita 40 na kichwa cha kilo 70, ilikuwa hatua ya kwanza kuelekea maendeleo ya mpango wa makombora wa Iran.

Roketi za "Fajr" ziliundwa kwa msaada wa China na Korea Kaskazini. Iran imetoa idadi isiyojulikana ya roketi hizo kwa Hezbollah ya Lebanon na Wapalestina huko Gaza. Wakati wa migogoro ya miaka iliyopita, baadhi yao zimetumiwa dhidi ya Israel.

1990 kombora la ardhini kwa jina "Somar" la umbali wa kilomita 700 lilizinduliwa miaka ya 90. Inasemekana kwamba kombora hili limetengenezwa kutoka kwa mtindo wa Kirusi ambao Iran ilinunua kutoka Ukraine miaka iliyopita.

Saudi Arabia imesema kuwa Iran ilitumia aina hii ya kombora katika shambulio la vituo vya mafuta vya Aramco, lakini Iran imekanusha kuhusika na shambulio hilo. Katika maadhimisho ya miaka 40 ya Mapinduzi ya Kiislamu, Iran ilizindua kombora la "Howeza" la kilomita 1,350.

Iran pia ina idadi ya makombora ya kuzuia meli, ikiwa ni pamoja na Raad, Nasr, Kausar, Zafar, na Noor makombora ya masafa mafupi. Makombora haya yanatolewa hasa kutoka kwa sampuli zilizotengenezwa China.

Ufanisi wa Makombora

v

Chanzo cha picha, Getty Images

Ufanisi wa makombora hayo ulidhihirika kwa kiasi fulani katika shambulio la eneo la jeshi la Marekani katika kambi ya Ain al-Assad nchini Iraq, operesheni ambayo ilifanywa kulipiza kisasi mauaji ya Qassem Soleimani, kamanda wa zamani wa jeshi hilo.

Kwa mujibu wa maafisa wa ulinzi wa Marekani, makombora 16 ya balestiki yalirushwa katika shambulizi hili. 11 kati yao walitua katika kambi ya Ain al-Asad na moja ikagonga karibu na kambi ya Erbil. Makombora manne hayakufanya kazi ipasavyo na hayakufikia shabaha.

Kamanda wa IRGC pia alisema makombora mawili hayakufika Iraq kabisa na yalitua Iran. Sehemu ya vifaa vya kambi ya Ain al-Asad, ikiwa ni pamoja eneo la kuhifadhia ndege, hospitali ya wanajeshi na hema za kijeshi, viliharibiwa, ingawa kulingana na maafisa wa Marekani, hakuna mtu aliyeuawa kwa sababu tayari walikuwa wamehamishiwa sehemu salama.

Inaweza kusemwa kwamba iwapo idadi kubwa ya makombora yatarushwa kutoka Iran kuelekea katika vituo hivyo, hasa ikiwa vituo hivyo havina ngao ya kujikinga na makombora, baadhi yao huenda yakagonga shabaha au angalau eneo lililolengwa. IRGC ilitangaza ilitumia makombora ya Fatih 313 na Qayam katika shambulio hili.

Mpango wa anga wa Iran

vc

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Makombora ya "Fatih" ndiyo makombora ya Iran yanayolenga shabaha kwa usahihi zaidi

Iran ina programu ya anga za juu. Kurushwa kwa satelaiti ya "Omid" mwaka 2007 ilikuwa tajriba ya kwanza ya mafanikio ya Iran katika uwanja huu. Miaka iliyofuata, satelaiti kadhaa ziliwekwa kwenye mzunguko wa dunia kwa kutumia roketi ya "Safir". Iran pia ilitumia roketi za Kaushgar kurusha viumbe hai angani na kuwarejesha duniani.

Katika miaka iliyopita, Iran imetumia roketi yenye nguvu zaidi ya Simorgh kuweka satelaiti nzito kwenye miinuko ya juu. Lakini baadhi ya majaribio yalishindwa. Kuna uwezekano wa hujuma za Marekani katika mpango wa makombora ya satelaiti ya Iran.

Kurushwa kwa satelaiti ya kwanza ya kijeshi ya Iran na IRGC mapema 2019 kulileta mjadala wa mpango wa anga wa Iran katika ngazi ya juu zaidi. Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu lilitangaza kuwa limeiweka satelaiti ya "Noor" katika mzunguko wa kilomita 425 kutoka ardhini."

Katika tathmini yake, Shirika la Ujasusi la Ulinzi la Marekani limeibua hoja kwamba licha ya miongo kadhaa ya vikwazo, Iran imeweza kutoa silaha kubwa zaidi ya makombora katika Mashariki ya Kati.

Shirika hili lilisema Jamhuri ya Kiislamu, inachukulia uundaji wa mpango wake wa makombora kama hitajio la kimkakati ili kuzuia maadui zake kushambulia nchi hii.

Hata hivyo Mtaalamu wa ngazi ya juu katika Taasisi ya Kimataifa ya Mafunzo ya Kistratejia, Michael Elman anasema Iran haifikii viwango vya Magharibi katika masuala ya teknolojia ya makombora, bali imeendelea zaidi kuliko nchi nyingine nyingi zikiwemo Korea Kaskazini na Pakistan.