Kwa nini Iran inazishambulia nchi tatu kwa wakati mmoja?

h

Chanzo cha picha, EPA

Na Jiar goal

Mwandishi wa BBC

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran, IRGC, limeimarisha nafasi yake miongoni mwa mataifa yenye nguvu katika miaka ya hivi karibuni.

IRGC linasema wazi kwamba kambi za kijeshi za Marekani katika Mashariki ya Kati, kambi za kijeshi za Israel mjini Tel Aviv na Hafia pia zinalengwa na makombora yao.

Siku ya Jumatatu usiku, walinzi wa mapinduzi wa Iran walirusha makombora 11 ya masafa marefu katika mji wa Irbil, mji mkuu wa jimbo la Kurdistan linalojitawala nchini Iraq.

Utawala wa Kurdistan unasema raia wasiopungua wanne wameuawa na wengine sita kujeruhiwa katika mashambulizi hayo.

Waziri Mkuu wa jimbo la Kurdistan Masrour Barzani ameyataja mashambulizi hayo kuwa ni uhalifu dhidi ya Wakurdi.

Shirika la habari la Fars lenye mafungamano na IRGC lilidai kuwa mashambulizi hayo yaliharibu maeneo matatu yanayohusishwa na idara ya ujasusi ya Israel -Mossad.

Serikali ya Iraq ya Kurdistan imekanusha kuwepo kwa mawakala wa kigeni katika ardhi yake. Hata hivyo, Israel haijasema lolote kuhusu suala hilo hadi sasa.

Iran ilishambulia nchi tatu kwa wakati mmoja

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

IRGC imemuua mfanyabiashara maarufu wa Kikurdi Peshrav Dizai katika shambulio lililofanyika kwenye makazi yake. Iran imeonesha kuwa imefanikiwa katika mashambulizi ya kigaidi.

Baada ya uvamizi wa Marekani nchini Iraq mwaka 2003, Dzay aliunda kampuni mbili, Falcon Group na Empire World. Shirika la habari la Reuters linasema kuwa Peshrao Dizai alikuwa karibu na familia ya Waziri Mkuu wa Kurdistan Barzani.

Makombora manne yalirushwa katika nyumba ya Peshrav Dizai. Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo, binti wa miezi 11 wa Dizai pia amefariki katika shambulio hilo.

Kikundi cha Falcon kinafanya kazi katika sekta za usalama, ujenzi, mafuta na gesi. Nchini Iraq, kitengo cha usalama cha Falcon Group kimekuwa kikitoa msaada kwa wawakilishi wa Marekani na nchi kadhaa za Magharibi pamoja na makampuni.

IRGC imejaribu kutuma ujumbe kupitia mashambulizi haya kwamba huenda sio tu kulenga vituo vya raia lakini pia kambi za kijeshi karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Irbil.

Kambi ya kijeshi ya muungano unaoongozwa na Marekani iko kilomita chache tu kutoka uwanja wa ndege wa Irbil.

Kwa nini ilifanya mashambulizi nchini Iraq?

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Bado kuna wanajeshi 2,500 wa Marekani nchini Iraq, baadhi ya wanajeshi hao wakiwa katika eneo la Irbil. Vikosi hivyo vimekuwa sehemu ya muungano unaoongozwa na Marekani dhidi ya kundi la Islamic State.

Marekani inasema wanajeshi wake wako huko kusaidia watu wa eneo hilo, ili kuizuia IS kufufuka. IS imekuwa ikishikilia msimamo wake katika eneo hili kwa muda mrefu.

Hata hivyo, mashambulizi haya pia yanaonekana kama ishara ya nguvu katika nyanja ya ndani ya Iran na kama jibu kwa mashambulizi ya Israeli nchini Syria.

Kamanda wa ngazi ya juu wa jeshi la IRGC aliuawa mwezi Disemba 25 katika viunga vya mji mkuu wa Syria, Damascus. Inaaminika kuwa kamanda wa Iran aliuawa katika shambulio hilo la Israel.

Mnamo tarehe 15 Januari, IRGC pia ilifanya shambulio la kombora la masafa marefu katika eneo la Idlib kaskazini magharibi mwa Syria.

Iran inasemekana kuwalenga IS na makundi mengine yenye msimamo mkali kwa mashambulizi hayo.

Idlib ni nyumbani kwa takriban raia milioni 3 wa Syria walioachwa bila makazi. Aliunga mkono uasi wa mwaka 2011 dhidi ya rais wa Syria Bashar al-Assad. Iran inamuunga mkono Bashar al-Assad.

Iran ni nchi yenye Waislamu wengi wa madhehebu ya Shia na Bashar al-Assad ni waziri mkuu wa madhehebu ya Sunni nchini Syria.

Ujumbe wa Iran ni upi?

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Nchi za Magharibi zilijaribu kadri ya uwezo wao kumuondoa Bashar al-Assad madarakani, lakini kwa msaada wa Iran na Urusi, Assad bado yuko madarakani.

Kundi la Kiislamu la Hayat Tahrir al-Sharm lina uwepo mkubwa katika mkoa wa Idlib.

Mbali na IS, al-Qaeda pia ina ushawishi.

Jeshi la IRGC limesema shambulio hilo la kombora mjini Idlib lililenga kujibu shambulio la kujitoa muhanga Kerman, kusini mwa Iran, tarehe 3 Januari.

Shambulio hilo la kujitoa muhanga lilitokea wakati umati mkubwa wa watu ulipokusanyika kutoa heshima kwa kamanda wa IRGC Qassem Soleimani mjini Kerman.

Jeshi la IRGC limesema kuwa lilitumia makombora ya Castor Buster katika shambulio la Idlib, ambayo yana uwezo wa kusafiri hadi kilomita 1,450.

IRGC imesema kuwa ilirusha makombora hayo kutoka Khuzestan kusini mwa Iran.

Hata hivyo, mashambulizi ya makombora yaliyofanywa na IRGC mjini Idlib yanaweza pia kufanywa kutoka mkoa wa Azerbaijan Magharibi karibu na Idlib.

Inaaminiwa kuwa mahali ambapo Iran ilirusha kombora hilo ni jaribio la kuuonyesha ulimwengu kwamba imefika katika maeneo kadhaa ya Israel.

Baada ya Iraq na Syria, Iran pia imeshambulia maficho ya kundi la itikadi kali katika eneo la Balochistan nchini Pakistan kwa makombora na ndege zisizo na rubani.

Pakistan imesema watoto wawili waliuawa na watu watatu kujeruhiwa katika shambulio hilo.

Pakistan imeliita shambulio hilo kuwa ni ukiukaji wa uhuru wake na kuonya juu ya madhara makubwa. Iran imewahi kuivamia na kuishambulia Pakistan kabla ya hapo.

Iran ilifyatua makombora katika eneo la Balochistan

f

Chanzo cha picha, Getty Images

Pakistan imedai kuwa watoto wawili waliuawa na watu watatu kujeruhiwa katika shambulio lililofanywa na nchi jirani ya Iran.

Iran imesema imeshambulia maficho ya kundi la kigaidi la Jaish-al-Adal. Madai hayo yalitolewa na shirika la habari linalohusishwa na jeshi la Iran.

Lakini Pakistan ilikanusha madai hayo, ikiitaja kuwa ni "kitendo kisicho halali" na kusema matukio kama hayo yanaweza kusababisha 'matokeo mabaya'.

Baada ya Iraq na Syria, Pakistan ni nchi ya tatu ambayo Iran imeishambulia katika siku chache zilizopita.

Kundi ambalo Iran imelilenga nchini Pakistan linaitwa Jaish al-Adal

Pakistan na Iran zimekuwa zikipambana na makundi ya waasi wenye silaha, ikiwemo Jaish-al-Adal kwa miongo kadhaa katika eneo hilo lenye watu wachache.

Mpaka kati yao ambao una urefu wa kilomita 900 (maili 559), usalama wake kwa muda mrefu umekuwa wasiwasi mkubwa kwa serikali zote mbili.

Tehran pia imelilaumu kundi hilo kwa mashambulizi karibu na mpaka mwezi uliopita. Zaidi ya maafisa 12 wa polisi wa Iran waliuawa katika mashambulizi hayo.

Wakati huo, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran Ahmad Vahidi alisema kuwa wapiganaji wenye msimamo mkali waliingia nchini humo kutoka Pakistan.

Kulingana na Idara ya Marekani ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Taifa, "Jaish al-Adal ni "kundi la kigaidi la Sunni lenye nguvu zaidi na lenye ushawishi" linalofanya kazi huko Sistan-Baluchistan.

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi