Bangili za sayari ya Zohali huenda zikapotea miaka milioni mia ijayo

jjj

Chanzo cha picha, CASSINI IMAGING TEAM/SSI/JPL/ESA/NASA

Zohali na bangili zake huenda ni maarufu zaidi katika Mfumo wa Jua, baada ya sayari yetu ya Dunia. Bangili za Zohali zinaundwa zaidi kwa barafu.

Chombo cha Cassini kilichotumwa kuchunguza sayari hiyo – kilitoa taarifa na picha ambazo zimewafundisha wanasayansi wa sayari mambo mengi kuhusu muundo wa kushangaza wa Zohali.

Tunapojifunza elimu ya anga za juu, tunajua kuwa hakuna kitu kitadumu milele, na bangili za Zohali zitatoweka.

Pia unaweza kusoma:

Lini bangili za Zohali zitatoweka?

Mtafiti, mwanasayansi wa sayari na mwanaanga anayefanya kazi katika Shirika la Ugunduzi wa Anga la Japan, James O'Donoghue – anasema.

Zohali ni 'sayari kubwa ya gesi' karibu mara 10 zaidi ya ukubwa wa dunia na imetengenezwa zaidi kwa hidrojeni. Ina mfumo wa bangili na inazunguka haraka kuzunguka jua. Siku kwenye Zohali ni saa 10 na nusu tu.

Ni sayari inayovutia sana kwa sababu ya bangili zake, ambazo zimekuwa nembo katika Mfumo wa Jua - unapotazama michoro ya kisayansi ya mfumo wa jua - lazima utaiona sayari ya Zohali.

Bangili za Zohali zimetengenezwa na nini?

KK

Zinaundwa na barafu na vumbi kidogo. Barafu hutengenezwa kwa vipande vidogo vidogo na vikubwa – vipande ambavyo huizunguka Zohali.

Vipande hivi vimezunguka Zohali katika mistari mingi. Bangili za ndani huizunguka Zohali kwa kasi Zaidi kuliko bangili nje.

Pia unaweza kusoma:

Bangili za Zohali zina umri gani?

.

Chanzo cha picha, NASA

Maelezo ya picha, Mchoro wa chombo cha NASA cha Cassini

Kuna mgawanyiko mkubwa kuhusu umri wa bangili hizi. Zimeundwa mamia ya milioni ya miaka iliyopita.

Wapo wanaosema zimejiunda karibu miaka bilioni nne iliyopita wakati Mfumo wa Jua unajiunda - migongano mikubwa ambayo hutengeneza bangili ilikuwa ya kawaida sana wakati huo.

Kwa upande mwingine, bangili za Zohali zinaonekana safi sana, karibu 99% ni maji safi, na hilo haliwezekani kwamba zina umri wa mabilioni ya miaka.

Bangili za Zohali zitatoweka?

OO

Chanzo cha picha, NASA/JPL-CALTECH/SPACE SCIENCE INSTITUTE

Tuligundua kwamba kuna vitu vinadondoka katika bangili za Zohali. Tukagundua vitu hivyo ni maji ambayo ndio yanaunda hizo bangili.

Lakini kuna uwezekano katika maji hayo kuna vipande vidogo vya miamba – na hutoa nishati ambayo hupuguza uzito wa vipande vya bangili.

Pia unaweza kusoma:

Bangili za Zohali zitadumu kwa muda gani?

Tunajua kiwango ambacho bangili zinatiririsha maji na tunajua wingi wake. Tunatabiri kwamba bangili zinaweza kudumu miaka milioni 100 hadi bilioni 1.1.

Lakini bado tunahitaji ushahidi mwingi zaidi - tafiti za hivi karibuni zilionyesha inaweza kuwa miaka milioni 100 au chini ya hapo. Nadhani tunaweza kusema tuna bahati ya kuwa hai wakati ambapo bangili za Zohali bado zipo.

Je, timu yako itachunguza nini siku zijazo?

A

Chanzo cha picha, DETLEV VAN RAVENSWAAY/SCIENCE PHOTO LIBRARY

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Tunataka kuona jinsi kuyeyuka kwa bangili hizi kunavyotofautina katika misimu. Kadiri Zohali inavyosonga mbele katika mwaka wake, bangili huelekea zaidi au kidogo kuelekea Jua, na bangili hizo hupigwa na mwanga zaidi au kidogo.

Tunafikiri bangili zinapaswa kutiririka maji kwa kasi pale bangili zinapokuwa zimeelekewa sana na Jua, kwa kuwa mwanga wa jua huchaji chembe za bangili.

Kila msimu wa Zohali huchukua miaka tisa. 2025 bangili hizo zitakuwa wazi kwa Jua na miaka saba baadaye zitakuwa wazi zaidi.

Tunatumai kuchukua vipimo katika mwongo ujao ili kufuatilia kiwango cha kuyeyuka kwake na kuzidisha mara nne ili kuelewa kinachotokea katika mwaka mmoja wa wa Zohali (miaka 29 ya Dunia).

Pia tunataka kutumia darubini ya anga ya juu ya James Webb ili kuona kama tunaweza kupata makadirio sahihi zaidi ya kuyeyuka kwa bangili za Zohali, ambayo yatatusaidia kuwa sahihi zaidi kuhusu kiwango cha mmomonyoko wa sasa wa bangili na maisha yajayo.