Ndani ya 'klabu ya siri' ya mashabiki wa soka wanaoipinga serikali ya Iran

Chanzo cha picha, Getty Images
Mashabiki wengi wa kandanda wa Iran wanasusia Kombe la Dunia kama njia ya kuadhibu timu yao ya taifa inayoshiriki mashindano hayo.
Wanahisi timu haijafanya la kutosha kuunga mkono harakati za maandamano ya kukosoa serikali ambayo yamesababisha vifo vya mamia ya watu.
Lakini kundi la mashabiki wa Iran wanaoishi nje ya Iran wameamua kusafiri hadi Doha na kuwasha moto wa maandamano ndani ya uwanja.
"Nina furaha kuwa hapa na kwamba ninafanya hivi kwa sababu niliona hofu machoni mwao," anasema Tara, msichana mdogo wa Iran na mpenda soka.
Ananiambia viwanja vya Kombe la Dunia vimejaa wafuasi wa serikali wakati wa mechi za Iran.
Tara sio jina lake halisi. Kila mtu niliyezungumza naye angekubali tu mahojiano ikiwa wangeweza kuweka utambulisho wao kuwa siri.

Chanzo cha picha, Getty Images
Amir alisafiri kwenda Doha na mchumba wake Rana.
"Nilifikiri hili ndilo jambo ambalo serikali inataka, ili sisi tusije hapa ili wawe na watu wao tu [katika viwanja vya michezo]," anasema.
"Hii ilipaswa kuwa fungate yetu," anasema Rana.
Lakini kuhudhuria mechi huko Doha kumeibua hisia zinazokinzana kwake.
"Kiuhalisia najihisi niko kwenye maombolezo, kaka na dada zangu wamefariki. Ingawa ninafurahi kuwa hapa na ninafurahia mchezo huo, sina furaha," anasema.
'Waligeuza timu dhidi yetu'
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Iran imekumbwa na maandamano dhidi ya serikali tangu Septemba wakati mwanamke mwenye umri wa miaka 22 anayeitwa Mahsa Amini alipofariki akiwa mikononi mwa polisi.
Watu wamechanganyikiwa iwapo timu ya kandanda ya Iran iko pamoja na waandamanaji au serikali.
Timu ya kandanda - iliyopewa jina la utani la Team Melli - ilikutana na Rais Ebrahim Raisi kabla ya kusafiri kwenda Doha.
Picha za mkutano huo zilisambaa katika mitandao ya kijamii na kusababisha wapinzani wengi wa Jamhuri ya Kiislamu kuikosoa timu hiyo na kutoa wito wa kususia.
"Timu Melli ilikuwa ya watu. Watu ambao hawakuwa na sauti," anasema Tara. "Timu Melli ndio kitu pekee ambacho kingetuunganisha ... na waligeuza Timu Melli dhidi yetu."
Kila mmoja rohoilikuwa juu juuwakati wa mechi ya kwanza.
"Nilitaka Iran ishinde lakini pia sikukufurahia," anasema Rana.
Lakini kuwaona watu wakivalia fulana na kupaka rangi zenye maandishi 'wanawake, maisha, uhuru' kwenye kucha zao kwa kutumia lugha zote za Kiajemi na Kiingereza kuliwapa motisha waandamanaji.
"Ilikuwakama sirilakini sio klabu yasiri sana," anasema Rana. "Tilitiana moyo."

Timu ya kandanda ya Iran ilikataa kuimba wimbo wa taifa katika mechi ya kwanza.
Lakini mashabiki wa soka wanaoipinga serikali walitoa sauti zao.
Waliimba "Ali Karimi" katika dakika ya nane na 88 ya mechi, wakimtaja mwanasoka huyo wa zamani ambaye ni mmoja wa wakosoaji wakubwa wa Jamhuri ya Kiislamu.
"Kuna watu walizomea wimbo wa taifa," anasema Rana. "Kuna watu hakupiga makofi wakati majina ya wachezaji yalipotajwa."
Mechi kali ya pili
Lakini hali ilikuwa tofauti sana kwa mechi ya pili ya Iran.
Watatu hao walifanikiwa kupenyeza baadhi ya nyenzo za maandamano licha ya ukaguzi mkali wa usalama.
"Ilikuwa inatisha sana," anasema Tara. "Unahisi uko hatarini."
Rana, Tara na Amir wananiambia walihisi kulikuwa na wafuasi wengi wa serikali kwenye mechi hii.
"Mara tu tulipoanza kuimba, safu inayofuata ilianza kusema 'Wairan kwa heshima, Wairan kwa fahari'," anasema Tara. "Hiyo ni moja ya nyimbo walizotumia kutunyamazisha."
Wananiambia waliona baadhi ya watu ndani ya uwanja wakiashiria usalama na kuwataka waondoe nyenzo za maandamano kutoka kwa baadhi ya mashabiki.
"Wanaogopa kila mtu ambaye anasimamia 'wanawake, maisha, uhuru'…kwa sababu mara tu wanaposikia wimbo huo, wanaanza kuwa na wasiwasi," Tara anasema.
Niliwauliza jinsi walivyohisi wakati Iran ilipofunga bao lake lakwanza dhidi ya Wales.
"Hatukushangiliai sana. Mimi na marafiki zangu watatu tulipigana pambaja kisha tukaangua kilio," anasema Tara.
'Si salama'
Qatar imekuwa na uhusiano mzuri wa kidiplomasia na Iran kwa miaka mingi.
Mnamo 2017, Iran ilikuwa moja ya nchi chache za kikanda zilizounga mkono Qatar wakati Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ziliweka vikwazo dhidi ya nchi hiyo ya Ghuba.
Mashabiki wa Iran wanaopinga serikali wananiambia kuwa hawajihisi wakiwa salama kutoa maoni yao hapa, haswa kutokana na uhusiano wa karibu kati ya nchi hizo mbili.
"Sijihisi nikiwa salama hapa," anasema Tara. "tawi la Jamhuri ya Kiislamu liko hapa kukusumbua."

Chanzo cha picha, Getty Images
Licha ya hatari inayotokana na hatua hiyo, Tara, Rana na Amir bado watahudhuria mchezo wa tatu. Kwao kuwa hapa ni jukumu kama la kazi.
''Nasikia kwamba baadhi ya waandishi wa habari walinyimwa visa ya kuja hapa kwa hivyo hiyo inatufanywa sisi kuwa watu wa maana sana," Rana anasema.
"Sisi ni wanahabari sasa," anasema Tara.















