Maandamano Iran: Ni nani mwenye nguvu katika serikali ya taifa hilo?

Chanzo cha picha, Getty Images
Kifo cha msichana mdogo aliyezuiliwa na vikosi vya usalama vya Iran kimezusha wimbi la maandamano ambayo yamekandamizwa vikali na mamlaka na kuiweka nchi hiyo katika uangalizi wa kimataifa.
Mahsa Amini, 22, alikamatwa kwa kutofunika nywele zake ipasavyo na hijabu yake. Na hatimaye akafa; Kulingana na mamlaka ya Irani kwa sababu ya mshtuko wa moyo, lakini familia yake inasema kwamba aliuawa chini ya ulinzi wa polisi.
Matukio hayo yalitokea katikati ya mwezi Septemba na takriban watu 150 wameuawa katika maandamano hayo, mashirika ya kutetea haki za binadamu yanasema.
Matukio hayo pia yalifungua upya mjadala kuhusu ni nani aliye na neno la mwisho katika taifa hilo la mafuta.
Kwa kuzingatia hili, tunaichambua serikali ya Irani.

Chanzo cha picha, EPA
Je, mamlaka ya kiongozi Mkuu ni yapi?
Mtu mwenye nguvu zaidi nchini Iran ni Ayatollah Ali Khamenei, kiongozi mkuu wa nchi hiyo tangu 1989.
Khamenei ndiye mkuu wa nchi na kamanda mkuu wa Majeshi. Ana mamlaka juu ya Polisi wa Kitaifa na Polisi wa Maadili, ambao mawakala wake walimkamata Amini.
Ayatullah pia anadhibiti Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), linalosimamia usalama wa ndani wa nchi, na mrengo wake wa kujitolea, Basij Resistance Force. Basij wamerudia kukandamiza upinzani nchini Iran.
Ni mtu ambaye ana uwezo mkubwa wa kufanya maamuzi juu ya jinsi ya kukabiliana na maandamano.

Chanzo cha picha, Reuters
Je Rais ana jukumu gani?

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni Ebrahim Raisi, ambaye ndiye afisa wa juu kabisa aliyechaguliwa na wa pili kwa cheo baada ya kiongozi mkuu.
Raisi ndiye anayehusika na uendeshaji wa kila siku wa serikali na ana ushawishi mkubwa katika siasa za ndani na mambo ya nje.
Hata hivyo, uwezo wake ni mdogo, hasa katika masuala ya usalama.
Wizara ya mambo ya ndani chini ya usimamizi wa rais inaongoza rasmi jeshi la polisi la taifa ambalo limezima maandamano hayo. Walakini, kamanda wake aliteuliwa na kiongozi mkuu na anajibu moja kwa moja kwake.
Vivyo hivyo kwa kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi na Basij.
Ikiwa kiongozi mkuu anataka kumaliza maandamano hayo kwa nguvu, rais hana budi ila kumsujudia.
Madaraka ya rais pia yanaweza kudhibitiwa na Bunge, chombo chenye jukumu la kutunga sheria. Kwa upande wake, Baraza la Walinzi - ambalo linajumuisha washirika wa karibu wa kiongozi mkuu - lina uwezo wa kuidhinisha sheria mpya na kupiga kura ya turufu.
Polisi wa maadili ni akina nani?

Chanzo cha picha, Getty Images
Polisi wa maadili - au wa doria za Mwelekeo - ni sehemu ya Polisi wa Kitaifa. Tawi hili la wakala wa usalama liliundwa mwaka wa 2005 ili kuzingatia maadili ya Kiislamu na sheria "sahihi" za mavazi, ambazo zilianzishwa baada ya Mapinduzi ya Kiislamu ya 1979.
Ina makadirio ya maafisa 7,000, wanaume na wanawake, ambao w
amepewa mamlaka ya kutoa maonyo, kutoza faini au kukamata washukiwa. Rais Raisi, mwanasiasa mwenye msimamo mkali, alianzisha hatua kadhaa mpya msimu huu wa joto ili kutekeleza sheria za kuvaa hijabu.
Hatua hizo ni pamoja na kuanzishwa kwa kamera za uchunguzi kusaidia kugundua wanawake ambao hawajafunuliwa, na hukumu ya lazima gerezani ilitolewa kwa watu wanaopinga sheria za hijabu kwenye mitandao ya kijamii
Walinzi wa Mapinduzi ni akina nani?

Chanzo cha picha, Getty Images
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ndilo shirika kuu la Iran kwa ajili ya kudumisha usalama wa ndani na liliundwa baada ya mapinduzi ya kutetea mfumo wa Kiislamu wa nchi.
Walinzi hao sasa ni jeshi kubwa , kisiasa, na kiuchumi nchini Iran, lina idadi ya zaidi ya maafisa 150,000. lina vikosi vyake vya ardhini, majini na anga, na linasimamia silaha za kimkakati za Iran.
Lina tawi la kigeni kwa jina kikosi cha Quds, ambacho hutoa kwa siri pesa, silaha, teknolojia, na mafunzo kwa washirika wake kote Mashariki ya Kati.
Pia inadhibiti Kikosi cha Upinzani cha Basij.
Je Basij ni nini?
Kikosi cha Upinzani cha Basij, kilichojulikana rasmi kama Shirika la Uhamasishaji wa Wanyonge, kiliundwa mnamo 1979 kama shirika la kujitolea la kijeshi.
Lina matawi katika majimbo na miji yote ya Iran, na katika taasisi nyingi rasmi za nchi.
Wanachama wake wanaume na wanawake, wanaoitwa "basijis", ni waaminifu kwa mapinduzi na wako chini ya amri za Walinzi.
Shirika hili linaaminika kuwa na wanachama wapatao 100,000 wanaofanya kazi za usalama wa ndani.
"Basiji" wamehusika pakubwa katika kukandamiza maandamano dhidi ya serikali tangu uchaguzi wa rais wa 2009 uliokumbwa na utata.












