'Ingekuwa binti yangu': Maandamano yaenea katika miji 80 ya Iran
'Ingekuwa binti yangu': Maandamano yaenea katika miji 80 ya Iran
Machafuko nchini Iran yameenea katika miji zaidi ya 80, huku watu kadhaa wakiuawa, kwa mujibu wa mashahidi na mashirika ya kutetea haki za binadamu.
Miongoni mwa walioripotiwa kuuawa ni mvulana wa miaka 16. Ghasia hizo zinafuatia kifo akiwa chini ya ulinzi wa Mahsa Amini - msichana aliyekamatwa na polisi wa maadili kwa jinsi alivyokuwa amevaa hijabu yake.
Maandamano hayo yanayoongozwa na wanawake yameibua hisia kote duniani - ikiwa ni pamoja Marekani, ambayo imeiwekaa vikwazo Iran.



