'Heche anakabiliwa na mashtaka mawili ya ugaidi' – Wakili wake
'Heche anakabiliwa na mashtaka mawili ya ugaidi' – Wakili wake
Naibu mwenyekiti wa chama cha upinzani cha Chadema nchini Tanzania John Heche, ambaye alikamatwa siku kumi na nne zilizopita leo alisafirishwa kutoka dodoma hadi mji mkuu wa Dar es Salaam, ambako amehojiwa na maafisa wa polisi kuhusiana na tuhuma kadhaa.
Wakili wa bwana Heche, Hekima Mwasipu ameiambia BBC kuwa Heche anazuiliwa katika kituo kimoja cha polisi baada ya kufahamishwa kuwa anakabiliwa na mashtaka mawili ya ugaidi.
Hekima amesema kuwa tayari wamewasilisha kesi mahakamana ili Heche ambaye anaugua aachiliwe kwa dhamana. Muda mfupi uliopita Mwandishi wetu Roncliffe Odit amezungumza na wakili Hekima.